LIREKEBISHWE HILI: Polisi barabarani na Waendensha Pikipiki (BodaBoda)

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,743
2,000
Naanza na Polisi wa Barabarani

Najua Polisi kuna baadhi ya mambo mnayofanya yanaisaidia jamii lakini kuna baadhi mnaiangusha jamii.

Siku za hivi karibu nilisafiri kutoka mikoa ya pwani kuelekea mikoa ya kati mwa Tanzania kwa msaada wa usafiri wa gari dogo la mizigo. Njiani tulisimamishwa mara kwa mara na askari barabarani kwa ajili ya kukaguliwa. Katika kukaguliwa huko hawakukosa lolote la kumkwanyua ela dereva kwa kisingizio cha faini. Kwa kawaida ukipatikana na kosa unaandikiwa risti kwa jaili ya kulipa faini ya kosa hilo. Katika safari hii dereva alikuwa anatishiwa kuandikiwa faini hivyo alichokifanya alikuwa "anawapoza".

Lengo hasa la kueleza haya nikuwa nilishidwa kuwatambua askari polisi wote waliopozwa na dereva kwa sababu walikuwa wamevaa visibau/vikoti (Reflective jackets) ambavyo vilikuwa vimeficha namba zao za uaskari na wengine ambao hawakuwa na visibau walikuwa wameng'oa namba zao za uaskari kifuani au begani.

Hili nashauri lirekebishwe kwa kuhakisha kila kisibau cha askari kinawekwa namba yake ya uaskari, pia S.Mwema aruhusu madereva kutokukubali kumsikiliza askari polisi yeyote ambaye haonyeshi jina na namba za uaskari kifuani au begani.

Namalizia na Waendensha Pikipiki (BodaBoda)Wakati naendelea na safari yangu kuelekea mikoa ya kati hasa mwa Tanzania nili bahatika kupumzika Morogoro kwa muda wa wiki mbili. Niligundua yafuatayo hapa Morogoro.

Kama nilivyosema mwanzo polisi wa barabarani kuna mambo ambayo wanafanya yanawasidia jamii.Mojawapo ni hili la askari wa Morogoro kuhakikisha madereva wote wa bodaboda wanakuwa na kofia ngumu (helmet) mbili kwa ajili yake na abira atakeyebebwa na pikipiki hiyo. Jambo hili limetekelezwa kwa kiwango cha hali ya juu.Ni nadra kukutana na dereva wa bodaboda asiye na kofia hizi mbili.

Tatizo lipo kwa hiyo "helmet" ya abiria. Karibu asilimia 95 ya pikipiki 67 nilizozikagua katika maeneo mbalimbali ya mji wa Morogoro, nimegudua kofia za abiria ni chafu kupindukia kiasi kwamba abiria wengi wanashurutishwa kuzivaa kutokana na amri ya askari polisi kuhakiksha umevaa helmet pindi unapokuwa umepanda pikipiki. Na madhara ya kutumia kofia hizi ni kuambukizwa maradhi ya ngozi kama kuota/kutokwa na mapunye kichwani, usoni shingoni na kuwashwa. madhara haya yemeisha watokea wakazi wengi wa Morogoro wanaotumia kofia hizi chafu.

Pia na hili nashauri lirekebishwe kwa kuhakisha kila dereva wa bodaboda anasafisha kofia ya abiria mara kwa mara. Hili linaweza kufanikiwa ikiwa abiria watasusia kupanda pikipiki ambazo zina kofia chafu. Vilevile askari wa barabarani wakati wanafanya ukaguzi wa dereva na pikipiki yake wahakikishe pia wanakagua kofia za zinazotumiwa ziko katika hali ya usafi.


--Na MpigaKelele safarini kuelekea mikoa ya kati.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom