Lipumba: Usaliti unaitafuna CHADEMA, nikirudi watakwisha

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyefutwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama hicho, amesema usaliti uliofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wake Dkt. Wilbroad Slaa na kukiuka makubaliano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kipindi cha kampenzi za uchaguzi mkuu wa 2015 utakigharimu chama hicho.

Lipumba ameyasema hayo Novemba 26, 2016 katika mkutano wake na baadhi ya viongozi wa kata za Jimbo la Temeke kwenye Ukumbi wa Sunrise ulioko Tandika jijini Dar es Salaam.

“Usaliti wa Chadema kwa Dkt. Slaa utaendelea kuigharimu na ndio maana hawataki nirudi katika wadhifa wangu na nikirudi watakwisha,” amesema.

Amedai kuwa, usaliti wa Chadema umesababisha upinzani kupokonywa ajenda yake ya ufisadi na kuruhusu Rais John Magufuli kuitumia ajenda hiyo kumaliza nguvu ya upinzani.

“Rais Magufuli ametunyang’anya ajenda ya kusimamia ufisadi, leo hii Chadema hawana ajenda ya kupinga ufisadi kwa sababu ya kumuasi Slaa,” amesema.

Kuhusu Ukawa Lipumba amedai kuwa, baadhi ya viongozi wa Chadema wanautumia umoja huo kuiua CUF Bara huku akituhumu baadhi ya viongozi wa CUF kuwa wananjama za kukiuza chama hicho.

Aidha, amesema alifikia hatua ya kujizulu mwezi Agosti mwaka jana uenyekiti wa CUF kwa madai ya kutokubaliana na hali ya kuwa mpiga debe wa Edward Lowassa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chadema na mwamvuli wa Ukawa.

“Nilikataa kuwa mpigadebe wa Lowassa, niligombea urais mara nne leo hii nisimame kumpigia debe Lowassa? Ambaye kwenye orodha ya majina ya mafisadi jina lake lilikuwa namba nmoja. Nisingeweza fanya hivyo nikaona bora kujiudhuru,” amesema.
 
Sasa huyu Pro Pesa naona kaishiwa kabisa , anajitafutia umaarufu kupitia CHADEMA anafikiri ataweza , alishindwa enzi hizo akiwa na nguvu ni sasa anapepesuka ndio ataweza ? Mzee Mnafiki sana Maalim kamuumbua jana kumbe alimwambia Lowassa aende NCCR-Mageuzi ...kwa sababu ya wivu wake dhidi ya CHADEMA .....
 
Chadema ina mpango kubaki chama Pekee cha upinzani

By the way CUF walishindwa nini kuidhinisha Huyu Pro pesa kujiuzulu kipindi kile
 
“Nilikataa kuwa mpigadebe wa Lowassa, niligombea urais mara nne leo hii nisimame kumpigia debe Lowassa? Ambaye kwenye orodha ya majina ya mafisadi jina lake lilikuwa namba nmoja. Nisingeweza fanya hivyo nikaona bora kujiudhuru,” Profesa Lipumba
 
nilipomuona anasukuma toroli la takataka nikaelewa wapi.Nikatamani yeye ndio angekuwa amepakiwa pamoja na mzigo uluokuwa kwenye toroli na kwenda kuwekwa mahali husika

Kama maprofesa wana akili za hivi,kuna haja ya kuwachunguza,hasa huyu profesa!

analala ofisini na taulo,ndala,mswaki,dawa ya meno msomi wa ngazi ya profesa!! tena wa uchumi!!

kwa mara ya kwanza ma Dk na ma Prof wamerundikwa serikalini,ndio wanaongoza kwa kutema mapumba
 
Back
Top Bottom