Lipumba: UKAWA hawatarudi Bunge la Katiba hadi waambiwe nini kitajadiliwa

Ukawa wakawie kufika kwenye Bunge maalum la Katiba mpya, mjadala wa Katiba Mpya hautakuwepo. Mjadala wa Katiba Mpya usipofanyika, Katiba ya zamani itaendelea kutumika hadi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hii itakuwa na maana kwamba UKAWA kwa namna moja au nyingine watakuwa wameridhia serikali mbili ambazo ndiyo kiini cha kujiondoa Kwenye Bunge Maalum la Katiba Mpya. Ukawa watakuwa wamekuwa. Katiba Mpya itakuja kuanza kujadiliwa awamu ya pili ya Awamu ya Tano tena kwa kuunda Bunge Maalum la Katiba jipya litakalo kuwa na sura mpya ukiondoa Prof. Lipumba, Tundu Lisu William Lukuvi Hamadi Rashidi na wengine wengi. Tutapata Katiba bora kabisa ya kizazi cha Whatssap. CCM watakuwa wamewafunga UKAWA goli la kisigino au la toboa tobo. Macho ya kuona umbali huo UKAWA hawana ni faida kwa CCM ambao wako mchekea hivi sasa

Ni bora goli la kisigino hili unalosema kuliko wanalolazimishwa kwa kurudi bungeni.

Kwa hali ilivyo hawana uwezo wa kubadili lolote pale bungeni ila kinachotakiwa ni uwepo wao ili ionekane kwamba wamekuwapo na wameridhia.

Kwa jinisi mazingira yalivyotengenezwa, si uzuri wa hoja utakaopata nafasi bali nini kinachoungwa mkono na wengi, na unajua wengi ni kina nani na bahati mbaya wamekwisha patana wanachotaka. Hata ukawa wakirudi hawatawabadi, kwani ndio kazi waliyopewa kuhakikisha wanashinda.

Nilichotegemea kwa uelewa wangu mdogo kuwa rasimu itakuwa na mwenyewe, ambaye atakuwa akichukua hoja na zile zinazotakiwa majibu kuja kujibu baadaye. Lakini haina mwenyewe wajumbe wanatoa hoja tu ziingie kwenye kumbukumbu za bunge, iwe nzito iwe nyepesi hakuna wa kujibu hakuna wa kuipokea hatima inapatikana kwa kura. Hii haina maana, ni wazi waliowengi watashinda, si kwa hoja bali kwa wingi wao na ndicho watu walichojipanga kukifanya na ndio wanachowalazimisha wenzao warudi.

Ili ukawa warudi mfumo mzima wa uendeshaji wa hili bunge inabidi ufumuliwe na kuundwa upya.
Kama ni serekali ndiyo yenye rasimu, ichukue nafasi yake na kupokea hoja ili hoja ndio ziongoze mjadala na wala si kura.
La kama rasimu haina mwenyewe kama inavyoonekana basi iundwe kamati itakayosimamia hoja na ni hoja tu ndio ziongoze mjadala na wala si wingi, hii itasaidia hoja za msingi kupewa uzito wake.

Lakini kwa hali ilivyo sasa haitasaidia hata kama ukawa watarudi, ni bora wasirudi ili maslahi ya nchi yake kwanza na vyama vifuate.
 
UKAWA, warudi, wasirudi, bado katiba mpya ya watanzania itapatikana tu! Hawa wapinga maendeleo hawapaswi kubebelezwa!

Hahaha umefulia kweli, sasa kama UKAWA hawana umuhimu hata wasiporudi...ni kwanini magamba mnaweweseka? Mara mtume viongozi wa kanisa,mashekhe, ili wawaambi e warudi bungeni?
Umefulia kijana jipange upya!
 
kwani wewe unaishi nchi gani mpaka hujui malengo ya ukawa?

Ukweli UKAWA wamejenga vizuri hoja, waambiwe kwanza mada itakayotawala mjadala kama ni rasimu yenye mawazo ya wananchi au ya wanasiasa? Ukweli hata mimi na elimu yangu chache naunga mkono UKAWA kwa kauli yao hiyo.

Chanzo: RFA taarifa ya saa 2 usiku.
 
Cha ajabu huko Manyara leo muungano wa makanisa 17 ya ki kristo wanawaomba UKAWA kurudi bungeni!! eti watakuwa wamewasaliti wananchi!!! kwani wao hawajui kiini cha tatizo kama sio unafiki?!! na mgeni rasmi ni Dr.MARY NAGU!!! Nyie viongozi wa dini acheni unafiki kama mko hapo kumtumikia Mungu wa kweli unganeni ni waumini wenu kutetea haki na sio kijibembeleza kwa watawala, kwani tumeshawachoka sasa.Na hapo kesho ndio itakuwa habari nzito nzito kwenye yale magazeti ambayo yanasubiria habari yoyote ile inayowaponda ukawa, hata kama imetolewa na chizi.

Hakuna viongozi wa dini nchii wote wanafiki wauza podaa kibao kwa mgongo wa dini
 
Chochote kitakachojadiliwa na kijadiliwe, mwisho wa siku ni serikali mbili tuuuuuuuuuuu! ama kwa katiba mpya au ya zamani, ama kwa amani au Vinginevyo

duniani wamepita watu wengi sana wa aina yako wanao angalia masilahi binafsi kuliko Nchi kwa ujumla wake.lakini utapita na historia itakusahau kabisa pale KWELI ITAKAPO JIDHIHIRISHA! siku hiyo itafika tu! kuna mtu alijua Hitller angeshindwa vibaya vile? sadam Hussein je? kuna mtu alijua siku moja KANU ingekufa nA watu kuisahau kabisa? zamu yenu na ccm yenu kufa imekaribia na hiyo vinginevyo unayo itaka itaanza na wewe
 
Katika mfumo wa uendeshaji mambo kwa kufuata demokrasia hatua zifuatazo ni muhimu. Kwanza pawepo na hoja.Hatua ya pili ni majadiliano. Hapa ndipo hoja hupimwa ubora wake. Hatua ya tatu ni maamumuzi yanayofikiwa kwa njia ya kura. Kwa kawaida waliowengi ndiyo wanaopewa.
Mtawala mmoja wa Misri (Farao) aliwahi kusema 'Demokrasia ni njia mbaya sana ya kufikia maamuzi, kwa sababu ya kuangalia uwingi wa watu.' Katika jamii yoyote wenye hekma ni wachache kuliko wasiokuwa nayo. Tunaposema tuwape walio wengi, tuna maanisha tuwasikilize wasio nahekma ambao ndiyo walio wengi. Mwenye hekma ndiye mwenye uwezo wa kuiona hoja yenye hekima pia. Asiye na hekma hawezi kupambanua ipi hoja ya hekima na ipi siyo. Lakini uongozi bora unataka maamuzi yenye hekma.
Kwa kuwa tumeaamini katika utawala wa kufuata demokrasia hakuna jinsi ya kukwepa kukubali maamuzi ya wengi hata kama hoja zao ni za kuchumia tumbo tu. Ilitakiwa ndani ya CCM kuwe na watu wachache wenye hekma wanaoweza kuangalia maslahi ya Taifa kwa mapana yake. Nachelea kusema ndani ya CCM watu hao hawapo. Ndani ya CCM viongozi walio wengi huangalia mwisho juu ya vitovu vya matumbo yao na namna watakavyojishibisha kupitia uchaguzi. Wanafikiria jinsi ya kushika badaraka kwa nia ya kujishibisha sio kujenga nchi.
Hakuna jinsi ukaepuka ushindi wa kutegemea uwingi wa wana CCM ndani ya BMK bILA KUWAKOMBOA KWANZA CCM aliofungwa na minyororo ya nja na uwoga wa kushindwa
Ni bora goli la kisigino hili unalosema kuliko wanalolazimishwa kwa kurudi bungeni.

Kwa hali ilivyo hawana uwezo wa kubadili lolote pale bungeni ila kinachotakiwa ni uwepo wao ili ionekane kwamba wamekuwapo na wameridhia.

Kwa jinisi mazingira yalivyotengenezwa, si uzuri wa hoja utakaopata nafasi bali nini kinachoungwa mkono na wengi, na unajua wengi ni kina nani na bahati mbaya wamekwisha patana wanachotaka. Hata ukawa wakirudi hawatawabadi, kwani ndio kazi waliyopewa kuhakikisha wanashinda.

Nilichotegemea kwa uelewa wangu mdogo kuwa rasimu itakuwa na mwenyewe, ambaye atakuwa akichukua hoja na zile zinazotakiwa majibu kuja kujibu baadaye. Lakini haina mwenyewe wajumbe wanatoa hoja tu ziingie kwenye kumbukumbu za bunge, iwe nzito iwe nyepesi hakuna wa kujibu hakuna wa kuipokea hatima inapatikana kwa kura. Hii haina maana, ni wazi waliowengi watashinda, si kwa hoja bali kwa wingi wao na ndicho watu walichojipanga kukifanya na ndio wanachowalazimisha wenzao warudi.

Ili ukawa warudi mfumo mzima wa uendeshaji wa hili bunge inabidi ufumuliwe na kuundwa upya.
Kama ni serekali ndiyo yenye rasimu, ichukue nafasi yake na kupokea hoja ili hoja ndio ziongoze mjadala na wala si kura.
La kama rasimu haina mwenyewe kama inavyoonekana basi iundwe kamati itakayosimamia hoja na ni hoja tu ndio ziongoze mjadala na wala si wingi, hii itasaidia hoja za msingi kupewa uzito wake.

Lakini kwa hali ilivyo sasa haitasaidia hata kama ukawa watarudi, ni bora wasirudi ili maslahi ya nchi yake kwanza na vyama vifuate.
 
Katika mfumo wa uendeshaji mambo kwa kufuata demokrasia hatua zifuatazo ni muhimu. Kwanza pawepo na hoja.Hatua ya pili ni majadiliano. Hapa ndipo hoja hupimwa ubora wake. Hatua ya tatu ni maamumuzi yanayofikiwa kwa njia ya kura. Kwa kawaida waliowengi ndiyo wanaopewa.
Mtawala mmoja wa Misri (Farao) aliwahi kusema 'Demokrasia ni njia mbaya sana ya kufikia maamuzi, kwa sababu ya kuangalia uwingi wa watu.' Katika jamii yoyote wenye hekma ni wachache kuliko wasiokuwa nayo. Tunaposema tuwape walio wengi, tuna maanisha tuwasikilize wasio nahekma ambao ndiyo walio wengi. Mwenye hekma ndiye mwenye uwezo wa kuiona hoja yenye hekima pia. Asiye na hekma hawezi kupambanua ipi hoja ya hekima na ipi siyo. Lakini uongozi bora unataka maamuzi yenye hekma.
Kwa kuwa tumeaamini katika utawala wa kufuata demokrasia hakuna jinsi ya kukwepa kukubali maamuzi ya wengi hata kama hoja zao ni za kuchumia tumbo tu. Ilitakiwa ndani ya CCM kuwe na watu wachache wenye hekma wanaoweza kuangalia maslahi ya Taifa kwa mapana yake. Nachelea kusema ndani ya CCM watu hao hawapo. Ndani ya CCM viongozi walio wengi huangalia mwisho juu ya vitovu vya matumbo yao na namna watakavyojishibisha kupitia uchaguzi. Wanafikiria jinsi ya kushika badaraka kwa nia ya kujishibisha sio kujenga nchi.
Hakuna jinsi ukaepuka ushindi wa kutegemea uwingi wa wana CCM ndani ya BMK bILA KUWAKOMBOA KWANZA CCM aliofungwa na minyororo ya nja na uwoga wa kushindwa

Tatizo langu si nani kashinda au kashindwa, wala nani anataka kutawala. Tatizo langu tunaipoteza nafasi nzuri ya kurekebisha kasoro zinazotusumbua kwa muda mrefu. Muungano wetu una matatizo, katiba yetu ina kasoro nyingi sisi tunaangalia nani kashinda/kashindwa. Hailipi mkuu!

Umeeleza vema kwenye maelezo yako, inaanza hoja, lakini hoja ni lazima iwe na mwenyewe. Hapa nani mwenyewe?, yaani nani owner?

Ngoja nieleze kwa mfano itakuwa rahisi kunielewa, kunapotakiwa kuwa na marekebisho ya sheria fulani waziri mwenye dhamana ndiye anayewakilisha kwa niaba ya serekali (huyu ndiye owner), analeta hoja na kuiwakilisha. Inaingia kwenye majadiliano, waziri kazi yake kufuatilia majadiliano ili penye ufafanuzi apate kuja toa ufafanuzi kwa niaba ya serekali (hata kama yeye hakubaliani nayo inabidi asimame nayo). Kazi nyingine ni kuchukua hoja zote zinazojenga ili kuona kama walioverlook mahali, hapa nani owner?

Wengi wanafikiri tatizo ni serekali 2/3, kwa upande wangu naona hapana. Tatizo ni mjadala usio na owner, nani atacontrol rythm ya hoja zinazotolewa. Maana hapa ni kama waliowengi wako upande A wa shilingi na walio wachache wako upande B wa shilingi, nani mwenye shilingi?

Unategemea aliyeupande mmoja wa shilingi ndiye aisimamie hiyo shilingi haiwezekani. Hata wakiahirisha mjadala wa muundo wa muungano watakuja kukwama tu huko mbele, sababu mjadala hauna mwenyewe. Kama hakuna waunde hata kamati itakayokuwa mmiliki na kuisimamia hii shilingi.

Nani mmiliki wa hii shilingi?
 
Mheshimiwa Shedafa, mwenye hoja anajulikana kuwa ni mwananchi lakini labda tuulize pia ni nani mwananchi? Mwananchi asiyekuwa mwanasiasa ni mwananchi, Mwana ccm ni mwananchi, Mwana Ukawa ni mwananchi, Kiongonzi wa kisiasa ni mwananchi, asiye kuwa wa kisiasa ni mwananchi. Tukitafuta mwenye hoja tutakuta hakuna anayehusika. Kufuatia swali lako inaelekea mwenye hoja ya Katiba Mpya ni Tume ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya, Tume ya Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba ambaye pia ni mwananchi. Lakini baada ya kuiweka hoja mezani watu wote wameichangamkia wameipokea (own) na kuifanya ni hoja ya kila mtu. Lakini nyuma ya pazia kila mtu anaangalia manufa binafsi au ya kikundi chake. Ni kama watu 100 kunyang'anyana kipande cha kanga mwisho wa kunyang'anyana utakuta hakuna aliyepata kanga bali kila mtu atabakia na kipande ambacho hakiwezi kumsitiri yeyote. Kila mtu si Ukawa walaCCM ameikamia kupata Katiba itakayosaidia kutimiza matamanio yake, lakini Shedafa nikukumbushe 'Mkamia maji hayanywi'.
Tatizo langu si nani kashinda au kashindwa, wala nani anataka kutawala. Tatizo langu tunaipoteza nafasi nzuri ya kurekebisha kasoro zinazotusumbua kwa muda mrefu. Muungano wetu una matatizo, katiba yetu ina kasoro nyingi sisi tunaangalia nani kashinda/kashindwa. Hailipi mkuu!

Umeeleza vema kwenye maelezo yako, inaanza hoja, lakini hoja ni lazima iwe na mwenyewe. Hapa nani mwenyewe?, yaani nani owner?

Ngoja nieleze kwa mfano itakuwa rahisi kunielewa, kunapotakiwa kuwa na marekebisho ya sheria fulani waziri mwenye dhamana ndiye anayewakilisha kwa niaba ya serekali (huyu ndiye owner), analeta hoja na kuiwakilisha. Inaingia kwenye majadiliano, waziri kazi yake kufuatilia majadiliano ili penye ufafanuzi apate kuja toa ufafanuzi kwa niaba ya serekali (hata kama yeye hakubaliani nayo inabidi asimame nayo). Kazi nyingine ni kuchukua hoja zote zinazojenga ili kuona kama walioverlook mahali, hapa nani owner?

Wengi wanafikiri tatizo ni serekali 2/3, kwa upande wangu naona hapana. Tatizo ni mjadala usio na owner, nani atacontrol rythm ya hoja zinazotolewa. Maana hapa ni kama waliowengi wako upande A wa shilingi na walio wachache wako upande B wa shilingi, nani mwenye shilingi?

Unategemea aliyeupande mmoja wa shilingi ndiye aisimamie hiyo shilingi haiwezekani. Hata wakiahirisha mjadala wa muundo wa muungano watakuja kukwama tu huko mbele, sababu mjadala hauna mwenyewe. Kama hakuna waunde hata kamati itakayokuwa mmiliki na kuisimamia hii shilingi.

Nani mmiliki wa hii shilingi?
 
Mheshimiwa Shedafa, mwenye hoja anajulikana kuwa ni mwananchi lakini labda tuulize pia ni nani mwananchi? Mwananchi asiyekuwa mwanasiasa ni mwananchi, Mwana ccm ni mwananchi, Mwana Ukawa ni mwananchi, Kiongonzi wa kisiasa ni mwananchi, asiye kuwa wa kisiasa ni mwananchi. Tukitafuta mwenye hoja tutakuta hakuna anayehusika. Kufuatia swali lako inaelekea mwenye hoja ya Katiba Mpya ni Tume ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya, Tume ya Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba ambaye pia ni mwananchi. Lakini baada ya kuiweka hoja mezani watu wote wameichangamkia wameipokea (own) na kuifanya ni hoja ya kila mtu. Lakini nyuma ya pazia kila mtu anaangalia manufa binafsi au ya kikundi chake. Ni kama watu 100 kunyang'anyana kipande cha kanga mwisho wa kunyang'anyana utakuta hakuna aliyepata kanga bali kila mtu atabakia na kipande ambacho hakiwezi kumsitiri yeyote. Kila mtu si Ukawa walaCCM ameikamia kupata Katiba itakayosaidia kutimiza matamanio yake, lakini Shedafa nikukumbushe 'Mkamia maji
hayanywi'.

Nakubaliana nawe "mkamia maji hayanywi"

Kimsingi nakubaliana nawe, ila hii dhana ya kuwa hoja ni mwananchi naona kama watu wanatafuta pa kujifichia. Mwenye hoja amekusanya mawazo ya wananchi, ila lazima awepo mwenye hoja. Yaani aliyeyakusanya mawazo ya wananchi, ila apate kueleza jinsi alivyo yakusanya na kwa nini ameyakusanya.

Bado kiza kimetanda, hata kama Ukawa watarudi hatutapata kile tunachotamani mpaka pale itakapokuwapo nia ya kweli.

Asante mkuu!
 
mie sio mpenzi wa mambo ya siasa, lakini kwa hili haliitaji elimu ya juu sana kujua nini kinapaswa kufanyika
ninachofahamu katiba inatokana na maoni ya wananchi na ndio hayo ambayo yamewekwa ktk rasimu, sasa CCCM tena hapa namaanisha wabunge wa CCCM krb wote(ambapo ni ajabu wakawa na msimamo mmoja wakati wana vichwa tofauti)wanapopotaka serikari 2, wameyapata kutoka katika tume ipi iliyokusanya hayo maoni yao ya serikali 2?
halafu ajabu wanataka UKAWA warudi , aisee hii ni ajabu. mbali ya hili nataka kuwarudisha nyuma kidogo kuna suala pia la kura ya siri na ya wazi hili pia CCCM nafikiri walipiga hatua ktk agenda yao ya kuwalazimisha wabunge wao wasiwasariti na kwa hakika walifanikiwa, ila kwa hili la serikali 2 au 3 nafikiri watakwama unless JK inteferes.
 
Back
Top Bottom