Lipumba: Tumkumbuke Mwalimu Nyerere Siku ya Kuzaliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: Tumkumbuke Mwalimu Nyerere Siku ya Kuzaliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 16, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,571
  Likes Received: 82,056
  Trophy Points: 280
  Lipumba: Tumkumbuke Mwalimu Nyerere Siku ya Kuzaliwa

  Mwandishi Wetu Oktoba 15, 2008
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  Asema aliowaamini ndio waliovuruga nchi

  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba anasema kwamba inasikitisha kwamba taifa limeshindwa kumuenzi Mwalimu Nyerere kupiga vita rushwa, uozo ambao alisimama kidete kuupiga vita katika kipindi chake chote cha uongozi.

  Ameiambia Raia Mwema katika mahojiano kwamba anamkumbuka Mwalimu kama mtu aliyekuwa anachukia mno rushwa akifuata kwa dhati moja ya ahadi za Mwana TANU iliyokuwa ikisema kwamba "rushwa ni adui wa haki, sitapokea, wala kutoa rushwa".

  Anasema kwamba suala la kupiga vita rushwa sasa limeachwa huku Taifa likionekana wazi kwenda kombo katika vita hiyo na hasa baada ya awamu ya tatu iliyokuwa ikiongozwa na watu ambao Mwalimu Nyerere mwenyewe alidhani ni waadilifu.

  Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, maovu mengi yanayohusiana na rushwa na ufisadi yalijitokeza katika kipindi cha mwisho cha awamu ya tatu chini ya aliyekuwa Raism, Benjamin Mkapa na kwamba awamu ya nne ya sasa inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete imeshindwa kutatua uozo huo ulioanzia wakati wa Mkapa.

  Anasema mwaka 1999 wakati Mwalimu anafariki ndio wakati ambao ilisajiliwa kampuni ya Anben, inayodaiwa kuwa ya watu walioko karibu na Mkapa, iliyokopa dola milioni 500,000 na kuzilipa bila ya mapato yake kujulikana yanatoka wapi.

  Anasema pia kwamba ndani ya awamu ya tatu ndimo mwaka 2002 lililopozuka sakata la rada ambalo gazeti la Guardian la Uingereza liliripoti ya kuwa Kampuni ya BAE System lililipa dola milioni 12 kama rushwa.

  Kashfa nyingi za ufisadi ukiwamo wa EPA (Akaunti ya Nje ya Benki Kuu) zilitokea wakati wa uongozi wa Rais Mkapa, mtu ambaye Mwalimu alikuwa na imani naye sana," alisema Prifesa Lipumba akiongeza kwamba uongozi wa awamu ya tatu ulishindwa kufuata maadili ya Mwalimu kuhusu rushwa hiyo ikionyesha kwamba " tumeshindwa kumuenzi kama inavyopaswa".

  Je, anasemaje kuhusu maadhimisho ya siku ya kifo cha Mwalimu? Kwa maoni yake, ni makosa kumkumbuka siku aliyofia. Alisema ingekua bora Taifa lingekuwa linamkumbuka siku aliyozaliwa.

  "Ingekuwa vizuri tungekuwa tunamkumbuka siku aliyozaliwa kwa sababu Mwalimu alikufa kwa kifo cha kawaida. Siku ya kuzaliwa kwake ingekuwa na maana zaidi," anasema.

  Lakini alisema pia kwamba binafsi anamkumbuka Mwalimu Nyerere kwa mengi na kumbukumbu ya Mwalimu isiyofutika katika kichwa chake ni ya mwaka 1962 alipokuwa mdogo Mwalimu alipohutubia mkutano wa TANU.

  Alisema kwamba Mwalimu alikuwa na mvuto mkubwa mno na anakumgbuka jinsi alivyoubadilisha wimbo wa Kinyamwezi wa "Ohoo sase zabela mitwe" (Ohoo risasi zavunja kichwa) kuwa "Ohoo TANU yajenga nchi".
   
 2. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Dola milioni 500,000! Hizi hata Bill Gates na Warren Buffett hawana. Uandishi wa bongo bwana!
   
 3. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I agree with mr lipumba, we should celebrate his life not his death so his birthday would be more appropriate. By the way, does someone else think that the end is near looking at what's hapening locally and globally?
   
 4. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli,naona mwandishi kajichanganya between kuandika figure in shillings na dollars....kaweka vyote
   
 5. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Yes, we remember the day Mwalimu was born, but not into the 70 years that he had on this valley of tears, but into eternal life!

  An umbilical chord was cut when the baby Julius was ejected into mother earth, but that was about it! However, when Mwalimu breathed his last, a whole nation shook. Indeed, the whole world took note of it. We remember that day, as we really have no memories of the other day!

  Is it possible for us to remember the day Mwalimu became one of us? How could we possibly remember what we have no memories of? Is it not entirely natural, even among secularists, to recall a person’s life on the day that life ended?

  I submit that we should continue to honor Mwalimu on the day he was born into life everlasting.
   
Loading...