Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,492
- 92,970
Jamani wakuu mwenye kujuwa maana haambiwi maana, hapa Lipumba anaonesha wazi kwamba yeye ni mwenyekiti jina tu hana mamlaka yote ndani yya Cuf isipokuwa Maalim Seif. ebu jisomee mwenyewe.
Lipumba ammaliza Hamad
na Nasra Abdallah | Tanzania Daima
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameunga mkono uamuzi wa kumvua uanachama Mbunge wa Wawi Hamad Rashidi Mohamed.
Akizungumza na waandishi habari jana ofisi za makao makuu ya chama hicho, Buguruni Dar es Salaam, Profesa Lipumba, alisema analazimika kuunga mkono maamuzi hayo kutokana na ukweli kwamba yalitolewa Mkutano wa Halmashauri Kuu.
Hata hivyo Lipumba ambaye kauli yake ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wanachama kuhusiana na suala hilo, alikiri kutopendezwa na kukubaliana na baadhi ya maamuzi yanayofanyika ndani ya chama, lakini kwa kuwa yameafikiwa na wengi yeye hana budi kuungana nao.
Japokuwa mwenyekiti huyo hakuwa wazi kutaja ni maamuzi gani ambayo hayakumpendeza alisema anawajibika kuyaheshimu kwa kuwa yalifuata katiba.
Alisisitiza kwamba ndani ya chama lazima kuwe na nidhamu hivyo ambaye anaona hawezi kufuata yale yaliyokubaliwa na chama ni vyema akajiondoa mwenyewe.
Alisema jambo la msingi kwao ni kujenga chama imara na chenye nidhamu na kuongeza kwamba siasa haiko makao makuu ya CUF ila iko katika maeneo ambayo watu wanatoka.
Alipoulizwa swali kama haoni chama chake kimekataa mabadiliko kama yale ambayo yalijaribu kufanywa na vijana wa chama cha Kikoministi cha China mwaka 1989 cha kutaka vijana kushika uongozi ambapo walitishwa kutokana na jaribio hilo.
Profesa huyo anasema kwa CUF mabadiliko hayo ni tofauti na hayo ya China kwa madai kwamba hao wanaotaka kugombea uongozi ndani ya chama hicho wana umri sawa na yeye na sio vijana.
Katika hili alisisitiza kwamba ni vyema wanaotaka kugombea wasubiri muda ukifika wa kufanya hivyo kujitokeza kwani uongozi uliopo sasa bado haujamaliza muda wake.
Jamani muda ukifika wa kufanya hivyo hakuna mtu atakayekataliwa kwani ni haki ya kikatiba, mbona katika kuelekea uchaguzi mkuu uliopita kuna baadhi ya wanachama walijitokeza kugombea nafasi ya urais kwenye kura za maoni na hakuna aliyepingwa? alihoji Profesa Lipumba.
Kuhusu kujiengua kwa baadhi ya wanachama katika chama hicho na kuanzishwa kwa chama kipya cha Alliance Democratic for Change (ADC), Lipumba alisema jambo hilo halimpi wasiwasi kwa kuwa kila mtu ana uhuru wake na wananchi ndiyo watakaoweza kupima chama kipi wanachoona kina uwezo wa kuwaongoza.
Safari yake nchini Marekani
Akizungumzia safari yake ya Washington nchini Marekani, ambayo alikaa huko kwa takriban miezi mitano, alikokwenda kwa ajili ya kufanya utafiti kuhusu demokrasia na maendeleo, utafiti ambao ulilenga kuleta demokrasia itakayoleta maendeleo na ajira katika nchi za Afrika, alisema katika utafiti alipata nafasi ya kutoa mjadala kuhusu miaka 50 ya Uhuru Tanzania na hatua ya maendeleo ambayo nchi imeifikia.
Kwa mujibu wa profesa huyo, miaka 200 ndiyo miaka ya maendeleo ya kisiasa, lakini cha kushangaza sasa hivi nchi iko katika robo ya miaka hiyo 200 ya maendeleo lakini asilimia 70 ya wananchi wake wanatumia chini ya dola moja huku mkazi wa Dar es Salaam ambaye anahesabiwa ndiye tajiri ana uwezo wa kupata sh 650 kwa siku.
Alisema suala la kuendelea uchumi na demokrasia linaenda pamoja hii ikiwa ni pamoja na wananchi kupata fursa ya kuikosoa serikali, kuchagua viongozi wanaowataka na kuwawajibisha.
Mapendekezo yaliyofikiwa katika utafiti huo wa uchumi duniani, Profesa Lipumba alisema aliona kuna haja ya kuwa na asasi muhimu zitakazowezesha uhuru wa wananchi kujieleza na kuikosoa serikali.
Pia mapendekezo mengine ni kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi na asasi huru ya kupambana na rushwa kwa kuwa Takukuru haina uwezo ikizingatiwa kwamba haiwezi kumpeleka mtuhumiwa wa rushwa mahakamani mpaka Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai atie saini jambo linalorudisha nyuma juhudi za kupambana na rushwa.
Vilevile utafiti huo ulitaka kuwepo kwa asasi huru ya kukusanya fedha itakayofanya kazi kwa uwezo na uwazi zaidi na kuwa na matumizi mazuri ya fedha zitakazopatikana katika makusanyo hayo.
Katika hili wananchi wa Tanzania wanaweza kufunguliwa kila mmoja akaunti yake bila kujali ni mtoto au mkubwa ambapo rasilimali zote kama gesi, mafuta na madini kiasi cha mapato yake kinagawiwa kwa kuweka katika kila akaunti ya mwananchi na makato ya kodi yanatolewa humohumo hali itakayofanya kila Mtanzania kufaidika na rasilimali zilizopo badala ya sasa hivi rasilimali hizo kufaidiwa na wachache.