Lipumba: Polisi pekueni mafisadi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,082
Lipumba: Polisi pekueni mafisadi

na Esther Mbussi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi nchini kuvamia na kufanya upekuzi katika ofisi za gazeti la MwanaHalisi na nyumbani kwa mkurugenzi wa gazeti hilo, badala ya kufanya hivyo kwa mafisadi ambao serikali imeendelea kuwalinda.

Mwenyekiti wa chama hicho, Ibarahim Lipumba, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kitendo cha polisi, kina nia ya kuvitisha vyombo vya habari na waandishi wake ili waogope kuandika taarifa za ufisadi na kula rushwa vilivyojikita ndani ya serikali ya CCM, inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

Alisema vyombo vya habari vimelisaidia taifa kubaini tatizo sugu na kubwa la rushwa, linalowaongezea wananchi gharama na ukali wa maisha na kuwaacha katika dimbwi la umaskini.

"Vyombo vya habari ni mhimili muhimu wa demokrasia na ulinzi wa haki za binadamu katika nchi na pia ni askari wa mstari wa mbele katika vita dhidi ya rushwa, Watanzania wote tunaokerwa na kuumizwa na ufisadi ambao ukiachiwa kuendelea kushamiri, unaweza kuliangamiza taifa letu, tunawajibika kuvitetea na kuvilinda ili vifanye kazi bila woga," alisema Lipumba.

Lipumba alisema vyombo hivyo hivyo vya habari vilifichua uozo wa mikataba mibovu ya Kampuni hewa ya Richmond ambao umeisababishia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi, mkataba mbovu wenye gharama kubwa wa IPTL, mikataba ya uchimbaji wa madini ukiwemo wa Buzwagi na kuongezwa muda wa Kampuni ya TICTS bila kufuata taratibu na kuzingatia sheria ya ununuzi wa umma (Public Procurement Act) na gharama kubwa wanayolipa NSSF kununua majengo ya Quality Group.

"Kuna uozo mwingi ambao vyombo vya habari vimefichua lakini wahusika hawachukuliwi hatua wala kupekuliwa na polisi kama ilivyokuwa kwa Kubenea, ukiangalia Rais mstaafu Benjamin Mkapa, alikiuka sheria ya maadili ya viongozi kwa kuitumia Ikulu kufanya biashara zake binafsi, ikiwa ni pamoja na kujiuzia kwa bei poa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira. Vijisenti vya Chenge ambavyo pia vimekiuka sheria ya rushwa na ya maadili ya uongozi ya kujilimbikizia mali isiyoelezeka kwa kipato halali cha mtumishi wa serikali na mengine ya kulichafua taifa, cha ajabu watu hawa wameendelea kukumbatiwa na serikali," alisema.

Alisema chama chake kinavipongeza vyombo vya habari vinavyochunguza na kutoa taarifa ya vitendo vya ufisadi na kutoa wito kwa Watanzania wote hususan wabunge wote bila kujali chama chochote cha siasa, kusimama kidete kuvitetea vyombo vya habari vilivyo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa.

Ijumaa jioni wiki iliyopita polisi waliovaa kiraia, walipekua ofisi na kompyuta za gazeti la MwanaHalisi zilizoko Kinondoni, na kupekua nyumbani kwa Mkurugenzi wa gazeti hilo, Saed Kubenea, kwa madai ya kutafuta taarifa ya siri ambayo waliamini Kubenea, anayo.
 
Hawa mapolisi wenyewe mafisadi wakubwa.Wangepekuana wenyewe kwa wenyewe kabla hawajaanza kupekua mafisadi.Maana wanapenda rushwa kama nini!
 
Yaani hizo ni kasi za Zombe na Mahita kumbe wao ndio wakubwa wa ujangili wao ndio wenye kitiya mimba ,haya Kikwete anza kwa Mahita maana kesi inazunguushwa mahakamani wakati jamaa ndie tena amenasa vibaya sana na kila siku zikizidi ndivyo mtoto anavyozidi kumshabihi baba yake anaelukaluka.
 
Polisi hawapo kwa ajiri ya ustawi wa taifa la tanzania. Wao wapo kwa ajiri ya kuwalinda mafisadi. Si mliona walivyoshughulikia vijana waliodhubutu kumusema Mzee wa utandawazi na dhama za wizi wa uwazi wazi?.

Lipumba nafikiri anajua mafisadi ndio watawala hivyo polisi hawezi kuwakamata mabosi wao.

Wala takukuru hawawezi kuwashitaki mabosi wao. Polisi nafikiri waendelee na kazi za kuwatafuta wapika gongo, kubambika kesi pale inapobidi, na wale wanaofichua mambo ya kifisadi, hizi kazi wanaziweza vizuri nk.

Lipumba nafikiri asaidie kuwaelimisha wananchi kuhusu watawala wetu hili waweze kujua jinsi watawala wetu wasivyokuwa na nia ya kuondoa maovu nchini.

Hili itakapofika 2010 tuchukue hatua mbadala kwa kuwakataa na kuwazomea watawala wabovu pale watakapokuja kutuomba kura huku vijijini.
 
“Kuna uozo mwingi ambao vyombo vya habari vimefichua lakini wahusika hawachukuliwi hatua wala kupekuliwa na polisi kama ilivyokuwa kwa Kubenea, ukiangalia Rais mstaafu Benjamin Mkapa, alikiuka sheria ya maadili ya viongozi kwa kuitumia Ikulu kufanya biashara zake binafsi, ikiwa ni pamoja na kujiuzia kwa bei poa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira. Vijisenti vya Chenge ambavyo pia vimekiuka sheria ya rushwa na ya maadili ya uongozi ya kujilimbikizia mali isiyoelezeka kwa kipato halali cha mtumishi wa serikali na mengine ya kulichafua taifa, cha ajabu watu hawa wameendelea kukumbatiwa na serikali,” alisema.

Alisema chama chake kinavipongeza vyombo vya habari vinavyochunguza na kutoa taarifa ya vitendo vya ufisadi na kutoa wito kwa Watanzania wote hususan wabunge wote bila kujali chama chochote cha siasa, kusimama kidete kuvitetea vyombo vya habari vilivyo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa.

Maneno mazito sana haya kutoka kwa kiongozi wa upinzani, wengine hatujawasikia, lakini ingawa simuamini kabisa Lipumba, bado hapa anastahili heshima kwa kusimama na kuhesabiwa na haya maneno, this ni the way to go!

Bravo Lipumba!
 
Mafisadi Wana Uwezo Hata Kutumia Chombo Chochote Cha Dola...ili Matakwa Yao Yatimie..maana Wako Juu Ya Sheria..nani Anabisha?wamefanywa Nini Tangu Sakata Lianze...ndio Kwanza Wanajipanga Kujisafisha.....ila Hope Yetu Iko Kwa Wafadhili....wakibana Ku Support Bajeti,,,,tutatafutana Sasa Hivi..............
 
Back
Top Bottom