Lipumba: Nikiingia Ikulu elimu chekechea hadi chuo kikuu bure

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,297
33,082
Main%2819%29.jpg

Mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akimtambulisha kwa wananchi mgombea ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Salum Bar`wani wakati wa mkutano wa kampeni ulofanyika kwenye viwanja vya Ilulu, mjini Lindi juzi.

Prefesa Ibrahim Lipumba anayewania urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) amesema kama akichaguliwa kuwa Rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, serikali yake itaondoa gharama za elimu katika ngazi zote.

Lipumba alitoa kauli hiyo juzi wakati akijinadi katika mikutano tofauti ya kampeni za uchaguzi huo iliyofanyika mjini hapa.

Akiwa katika maeneo tofauti ya jimbo la Lindi Mjini, Profesa Lipumba alisema CUF imeazimia kuweka suala la elimu ya bure katika vipaumbele vyake, kwa vile sekta hiyo ni mkombozi wa umaskini uliokithiri kwa wananchi wengi.

"Ndugu zangu mkinipa ridhaa ya kunichagua kuwa Rais, nitahakikisha elimu kwa vijana wetu inakuwa bure," alisema.

Pia Profesa Lipumba alisema ilani ya uchaguzi ya CUF inaelekeza kuwa, kilimo kinaboreshwa na kuwa cha kisasa.

Alisema kama CUF ikishinda, suala la upatikanaji wa maji safi na salama litakuwa miongoni mwa vipaumbele vyenye lengo la kuboresha maisha na kuistawisha jamii.

Aliwataka wakazi wa mkoa wa Lindi kuondokana na tofauti za kiitikadi, badala yake waungane katika kuwachagua viongozi watakaoleta ukombozi halisi wa maisha bora, ustawi na maendeleo.

Akiwahutubia wakazi wa vijiji vya Likong'o, Mingoyo na Lindi Mjini, Profesa Lipumba alisema mkoa huo umejaliwa ardhi nzuri yenye rasilimali asilia, lakini wananchi wake wanaishi katika umaskini uliokithiri.

Profesa Lipumba alisema pamoja na kuwa na rasilimali hizo, zikiwemo madini, gesi, bahari ya Hindi na fukwe nzuri, hakuna jitihada zilizofanywa na serikali ya CCM kuwaletea mageuzi ya kiuchumi.

Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, alisema licha ya mji wa Lindi kuwa halmashauri tangu mwaka 1936 na manispaa kwa mwaka huu, maendeleo yake yanashuka huku viongozi wakiwemo wabunge wa CCM wakijinufaisha.

Alisema CUF kinatambua matatizo yanayowakabili wakazi hao, hivyo kama wagombea urais, ubunge na udiwani wake wakichaguliwa, kitahakikisha kinashirikiana na wananchi kuziondoa kero hizo.

"Hakuna sababu ya kuwepo kwa makundi wala matabaka ya kisiasa, kinachotakiwa ni kushikamana kwa ajili ya kuijenga nchi yetu, tuweze kuondokana na umaskini unaotukabili kwa miaka mingi sasa," alisisitiza.

Aliutumia mkutano huo kuwanadi mgombea ubunge wa Lindi Mjini kupitia CUF, Salum Khalfani Baruani na wagombea udiwani katika kata 18 za jimboni humo.

CHANZO: NIPASHE
 
Huyu naye nimemchoka bwana, nadhamini upinzani, ila tunahitaji sura mpya, CUF karibu watafulia
 
Upande wa Tanganyika bado hakuna umakini haswa Lipumba alikuwa apumzike na amuunge mkono Dk.Slaa.Nimesikitishwa sana kumuona tena kwenye uliongo wa CUF kugombania urais.

Kusema elimu itakuwa bure nadhani ni kutuchanganya, sote ni watu wazima hii haingii akilini mwangu...Anyways, the story is different in Zanzibar...I still love M.Seif:becky:
 
Huyu bwana, anaposema kuingia ikulu anamaanisha nini? Hata ushauri wa manufaa huwa anaruhusiwa kushauri? Ninachojua safari zake za huko huwa ni kupiga deal juu ya kuvuruga harakati za ukombozi. Au anaomba aitwe alizopewa zimeisha?
 
Upande wa Tanganyika bado hakuna umakini haswa Lipumba alikuwa apumzike na amuunge mkono Dk.Slaa.Nimesikitishwa sana kumuona tena kwenye uliongo wa CUF kugombania urais.

Kusema elimu itakuwa bure nadhani ni kutuchanganya, sote ni watu wazima hii haingii akilini mwangu...Anyways, the story is different in Zanzibar...I still love M.Seif:becky:

Na ndicho kilichomtoa UKAWA. Siku zote huwa ana uroho wa kuwa raisi. Sijui raisi wa nani.
 
Back
Top Bottom