Lipumba na Zitto: Taulo la kufutia udhaifu wa CHADEMA

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
1,002
1,146
CHADEMA huwa wanapata taabu sana kuhusu Zitto na Lipumba. Kila wanavyojaribu kuwapa "brand" ya usaliti ndivyo wanavyozidi "ku-prove wrong". Wanajaribu kuonesha kuwa wapinzani wa kweli ni wanasiasa walioko Chadema peke yao, lakini matendo na harakati za viongozi na makada wa Chadema hayana "impact" yoyote katika "kuwavusha" wananchi.

Ukweli ni kwamba kwa hali ilivyo sasa viongozi wa Chadema ni dhahiri kuwa wamefilisika kisiasa. John Mnyika anajaribu "kuitoa" Chadema kwa avenda ya tume huru; bila shaka anajaribu kutekeleza agenda iliyokuwa inalalamikiwa na Prof. Safari. Mnyika anafanya kwa "kumuomba" Rais apeleke mswada wa tume huru bungeni kwa hati ya dharura. Vilevile Mbowe naye anajaribu kuipaisha Chadema kwa "kumuomba" Rais afanye maridhiano ya kitaifa.

Wote wawili, Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu wake Mnyika, ingawa mambo wanayoyapigania ni muhimu, bado yanakosa mvuto kutokana na "approach" wanayoitumia ya "kumuomba" Rais atelekeleze. Hawakutakiwa kumuomba, bali "kumshinikiza" Rais atekeleze. Staili ya kumuomba Rais ibaki kutumiwa na viongozi wa dini tu.

Tofauti ya Chadema na Zitto ni kama alivyosema Zitto mwenyewe kuwa siasa ya Tanzania sio ile tena ya "kuombaomba", bali inahitaji "siasa kali". Ikumbukwe kuwa kilichoipaisha Chadema ni siasa za kiharakati na hata CUF ilikuwa hivyo hadi ikabatizwa jina la "Ngangari". Leo Chadema wanapojitia "ustaarabu" dhidi ya uhuni wa wapinzani wao CCM ni wazi kuwa wanapoteza mvuto na ushawishi kwa wananchi.

Tunamuona Lipumba akichapa kazi kwa kufanya ziara vijijini. Ingawa anapata changamoto ya kukamatwa na polisi lakini anasonga mbele. Viongozi wa Chadema wamepoa kisiasa kiasi kwamba hawezi tena kufanya hata kile kinachofanywa na Lipumba. Matokeo yake makanda wa Chadema wanapata husda dhidi ya harakati za Lipumba na kuendeleza nnema zao dhidi yake eti Lipumba ni msaliti na anachokifanya ni maigizo na hadaa tu.

Kuamimishana hivi ni ujinga wa hali ya juu sana. Kwanini Mbowe ambaye ndo mpinzani wa kweli hafanyi ziara vijijini? Tena anashindwa kufanya mikutano hata kwenye jimbo lake licha ya ruhusa aliyonayo kama mbunge tofauti na Lipumba. Tulitegemea kuona au kusikia msafara wa Mbowe umekamatwa na polisi kwa kufanya ziara bila taarifa. Hi ni nani ataamini kwamba Chadema ni wapinzani wa kweli wakati wamekaa tu huko waliko bila kuwafikia wananchi na kuwapa hamasa?

Zitto kwa upande wake anaichachafya serikali kwa kila namna. Tumesikia aliandika barua kwa WB iliyochangia kucheleweshwa kwa mkopo dola 500M. Tumesikia Zitto amefungua kesi kupinga utenguzi na uteuzi wa CAG na mengine mengi tu. Chadema wao kila jambo wanapiga kimya tu lakini wakati huo huo hawaamini macho yao kuona Zitto hapoi badala yake wanajaribu kuwakatisha watu tamaa kwamba Zitto ni mtu wa system na anachokifanya ni maigizo na hadaa tu.

Yule Mwenyekiti wa CCM wilaya kule Kilolo alipokosoa mbele ya Naibu Waziri sera ya chama chake ya kununua ndege kuwa haina faida moja kwa moja kwa wananchi wa Kilolo ukilinganisha na kiwanda, angalau ilileta "attantion" na ikawa ni "habari" kwavile hicho ndicho kitu wananchi wanataka kuona; kuikosoa serikali kwa "jicho la kauzu" ambayo ni jukumu la wapinzani na sio kuombaomba.
 
X-bar, CHADEMA wakishinikiza mtakuja hapa kusema ni chama cha kiuanaharakati, siasa za harakati haziwezi kuchukua dola. Wakitumia diplomasia mtakuja tena CHADEMA ni wapole mnaomba maridhiano. Wewe sema tu huipendi CHADEMA
 
Zitto ashawahi kuichachafya serikali kwa lipi japo ungeonyesha hata moja tu.Lipumba anapiga kazi ipi hiyo?Ya kwenda Tanga na kukamatwa.

CHADEMA ni mpango wa Mungu hao ccm B tushawajulia hatuna time nao.CCM pambaneni na halinyenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto na Lipumba wawape CHADEMA tabu kwa lipi hasa?!

Unataka siasa za kibabe sio, ukiambiwa leo asubuhi ukiamka usiende kazini kwako patakuwepo na maandamano utatakiwa kushiriki utakuwa tayari chini ya utawala huu?

Unadhani CHADEMA wajinga "kuomba", ni kwasababu hawataki kuwaumiza wanachama na wapenzi wao kwa kitakachowapata wakilazimisha km unavyotaka.

Na CHADEMA wangekuja na mikakati hiyo mngeanza tena kuwaponda wanapenda fujo, ni wanaharakati, now wamekuja tofauti bado mnalia lia, sijui mnataka nini nyie watu!

Hivi unaweza vipi kufanya siasa za kiharakati/ nguvu mbele ya mpinzani wako anaepata support ya polisi na mabomu yao ya machozi na maji ya kuwasha? wakati wewe huna kitu, huoni km huo ni ujuha!

Unaona issue ya maana sana m/kiti wa CCM Kilolo kuikosoa serikali sio, hao CHADEMA wameshaikosoa serikali mara ngapi na ushauri wao ukapuuzwa?! tena wengine wamekimbia nchi kwa kuhofia usalama wao sababu tu ya kuikosoa hiyo serikali wakaambulia kuitwa wasaliti!.

Different approach is the best kwa wakati huu, huwezi shindana kwa nguvu na mtu asiejali au kutambua maana ya uwepo wa wapinzani katika uongozi wake, anaewaona wapinzani ni maadui, ni sawa na kuwatafutia matatizo wanachama wako bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom