Lipumba: Mimi bado ni Mwenyekiti wa CUF, sitambui kikao cha Zanzibar

Hii, ni kwa mujibu wa gazeti la Uhuru la leo tar 30 augost 2016. Hivi ni kweli kwamba professor anatarajia kuigawa CUF iwe na matawi tofauti yaani CUF bara na CUF zanzibar? Nini itakua hatma ya CUF chama ambacho wakati fulani kilikua chama kikuu cha upinzani! na nani hasa atakua mnufaika wa gawanyiko hili? CHADEMA au CCM?
Leteni maoni.
 
Pamoja na kumuheshimu sana Prof. Lipumba kama mwalimu wangu kwa hili limenisikitisha sana na mbele ya macho yangu amepoteza heshima. Alilofanya wakati huo (2015) ni kama kumpa talaka mke wake akiwa labor ward na sasa mtoto anatambaa na hivyo sasa anataka kumrudia mke wake!! Hakuna watu wenye akili timamu wanaweza kukurudisha kwenye cheo chako wakati uliwatupa mkono katika wakati mgumu. Yeye na Dr. Slaa historia itawahukumu.
 
Posho imeisha na wajua wajanja sasa hv hawamthamini mana walifanikiwa walichokitaka. Mbona Slaa katulia naye awe vvyo hivyo.
 
Nadhani mtakuwa mmelewa tatizo la ajira mtaani sasa,lipumba kakomaa miezi kadhaa bila kazi sasa anataka kurudi kazini kwake
 
Mtatiro kijana amekubali kutumiwa na Seif......

Huyu Seif amelaaniwa maana ana uzoefu wa fitna...alimfitini Jumbe
Lipumba Mzee amekubali kutumiwa na CCM,
Hawa CCM wamelaaniwa maana wana uzoefu na fitina, wamewafitini wengi tu
 
Habari JF,

Pro Lipumba umeonyesha kuwa we ni mmoja ya viongozi mlioko kwa ajili ya maslahi tu. Leo hii sasa nimeelewa kwa nin watanzania wamekuwa wakikataa kukupa dhamana ya kuiongoza nchi hii.

Hufai kuwa hata kiongozi wa kitongoji , Tanzania nzima leo inakuangalia unavyoliliaa uongozi ambao mwaka mmoja nyuma uliukataa na kuapa kutokurudi tena , lakin leo uko radhi hata kulala jela ili mradi tu urudi pale juu ulipokuepo .

We ni sawa na mwanajeshi aliyekimbia jeshi lake vitani, huna sifa tena ya kuitwa mpiganaji.

"A true leader has the confidence to stand alone, the courage to make tough decisions, and the compassion to listen to the needs of others. He does not set out to be a leader, but becomes one by the equality of his actions and the integrity of his intent." --Douglas MacArthur
Huyo hana nia ya kubaki CUF. Ila anataka kuacha amekivuruga chama ndipo aondoke.
 
Habari JF,

Pro Lipumba umeonyesha kuwa we ni mmoja ya viongozi mlioko kwa ajili ya maslahi tu. Leo hii sasa nimeelewa kwa nin watanzania wamekuwa wakikataa kukupa dhamana ya kuiongoza nchi hii.

Hufai kuwa hata kiongozi wa kitongoji , Tanzania nzima leo inakuangalia unavyoliliaa uongozi ambao mwaka mmoja nyuma uliukataa na kuapa kutokurudi tena , lakin leo uko radhi hata kulala jela ili mradi tu urudi pale juu ulipokuepo .

We ni sawa na mwanajeshi aliyekimbia jeshi lake vitani, huna sifa tena ya kuitwa mpiganaji.

"A true leader has the confidence to stand alone, the courage to make tough decisions, and the compassion to listen to the needs of others. He does not set out to be a leader, but becomes one by the equality of his actions and the integrity of his intent." --Douglas MacArthur
Lipumba=Mbowe=Seif=Mbatia=Lowassa=????
 
Profesa Lipumba Mtanzania, mtaalam wa uchumi mwenye heshima ya Kimataifa anayumbisha yumbiasha chama chake kilichompa heshima kubwa ndani na nje ya Nchi yake, mtu ambae jamii ilimuamini ikamsikiliza na kumfuata leo ameigeukia jamii iliyomuamini. Kama Profesa anayafanya haya, vipi kwa wasiona elimu ya kutosha? nini tofauti yake na ya std 7? Tanzania ya viwanda kwa Maprofesa/wasomi hawa itawezekana?
 
Mwenzie kaomba kapewa, sasa hivi anatesa tu na V6 la parole, cha msingi amwandikie Rais barua ya kuomba kazi, maana wachumi wazoefu bado wanahitajika hasa kuelekea kwenye uchumi wa viwanda wa awamu hii ya tano. Prof waache CUF hawahitaji huduma yako kwa sasa.
 
Kama aliandika barua kuwaomba ajiuzuru wakakubali akajiuzuru ,ameandika barua kutengua uamuzi wake ina maana asubiri majibu kwa sababu alijivua mamlaka na kuwakabidhi wengine na hata walivyomsimamisha hana mamlaka ya kujiita mwenykiti msomi gani mbumbumbu hivi?
 
Jamani, ngoma sasa inogile. Prof. leo kakomaa hataki kabisa kuambiwa amesimamishwa uanachama.

Hii safi sana maana maalim anaendesha chama kama mali yake.

===========

Akihojiwa na mtangazaji Spencer Lamerk wa ITV usiku huu, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali wa CUF.

Prof. Lipumba amesema kuwa kufuatia kutengua barua yake ya kujiuzulu Uenyekiti, aliandika barua kwa Katibu Mkuu wake kutaka kurejea kazini kama Mwenyekiti. Katibu Mkuu alimjibu kuwa anatafuta ushauri wa kisheria.

Kuhusu kikao cha Baraza Kuu la CUF kilichomsimamisha uanachama, Profesa Lipumba amesema kuwa kikao hicho hakikuwa halali kwakuwa hakukuwa na akidi ya Wajumbe wa kutoka Tanzania Bara. Amesema kuwa Katibu Mkuu hamshirikishi Naibu Katibu Mkuu Bara na kuonekana akiendesha chama kiimla.

Prof. Lipumba amesema kuwa Katibu Mkuu asipotaja tarehe ya yeye kurejea kazini kama Mwenyekiti, atasubiri barua ya Msajili wa Vyama ili aanze kazi tena kama Mwenyekiti wa taifa wa CUF.

Bado anajua kuwa atasaidiwa na dola kama mwaka jana alipojiuzulu na kupigwa mpunga na kukimbilia kigali.
Kwenye ule mkutano juzi wapamba walikuwa polisi.
Msajili ataridhika (kwa maelekezo ya ikulu) arudi kuwa mwenyekiti. WanaCUF msikubali kuwa na mwenyekiti wa aliyesimikwa na dola.
Multifaced hypocrisy
 
Hivi huyo jamaa kakosa kazi zingine za kufanya hadi ang'ang'ane na siasa?

SIJUI njaa au tuseme nn kinamsumbua, maana na amini uwezi kufikia ngazi ya kuwa na kiwango cha PHD ukawa na njaa au maisha magumu,,,labda ukubari tu kununulika,,,kwa ufupi huyu mzee anajitia aibu
 
Mwenzie kaomba kapewa, sasa hivi anatesa tu na V6 la parole, cha msingi amwandikie Rais barua ya kuomba kazi, maana wachumi wazoefu bado wanahitajika hasa kuelekea kwenye uchumi wa viwanda wa awamu hii ya tano. Prof waache CUF hawahitaji huduma yako kwa sasa.
Alienda kumsalimia (kujipendekeza) Ikulu JPM akajifanya hamkumbuki alivyosaidia chama tawala kuangamiza upinzani. Too late!! wanafiki watakufa njaa mwishoni tu
 
Back
Top Bottom