Lipumba kukutana na wanachuo Dodoma..kuzungumzia uchumi wa Taifa na Dunia karibuni wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba kukutana na wanachuo Dodoma..kuzungumzia uchumi wa Taifa na Dunia karibuni wote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Topical, Mar 11, 2012.

 1. T

  Topical JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma wameomba kukutana na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF), Prof Ibrahimu Lipumba ili kujadili kuyumba kwa uchumi wa taifa na kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
  Hayo yalibainishwa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alipokuwa akizungumza na wanafunzi kutoka katika chuo kikuu cha Dodoma (Udom), Chuo cha biashara (Cbe), Chuo cha Mipango pamoja na Chuo cha Mtakatifu John.Naibu Katibu Mkuu huyo alisema baada ya kuzungumza na wanafunzi hao wa vyuo vikuu na kutambua umuhimu wa uchumi wa taifa maombi hayo wameyapokea na kwamba Prof Lipumba atafanya kongamano na wanafunzi hao kujadili masuala ya kuyumba kwa uchumi na mfumuko wa bei uliopo sasa.“Baada ya kusikiliza maombi ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kwa kuona jinsi hali ya uchumi ilivyo mbaya kwa sasa tumeamua kuandaa kongamano ambalo Prof Lipumba atazungumza na wanafunzi hawa ili kulitafutia ufumbuzi suala hili,” alisema Mtatilo na kuongeza “Suala hilo linatarajiwa kufanyika hivi karibuni baada ya mtaalamu huyo wa uchumi kulejea nchini hivi karibuni kutoka Marekani,” alisema.Mtatilo alisema kwa sasa hali ya uchumi inazidi kuwa mbaya baada ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei jambo ambalo linazidi kufanya maisha ya watanzania kwa magumu.“Kiukweli suala la uchumi na mfumuko wa bei linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi kwani jinsi hali ilivyo sasa inatisha ndio maana hata wasomi wameliona jambo hili na kutaka kutafutiwa ufumbuzi wa haraka,” alisemaKatika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo alisema wanafunzi hao pia wameomba kukutana na Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ilikuwapa mafunzo ya siasa na utawala bora.“Wanafunzi hao pia wameoma kukutana na Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ili kuwapa mafunzo ya siasa na utwala bora jambo ambalo ni la msingi kwa maendeleo ya Taifa,” alisemaKatika Mkutano huo ambao ulihuhuliwa na wanafunzi 60, wanafunzi 23 walichukua kadi za chama hicho.20 february,2012
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  tunahitaji kujikita kwenye ujasiriamali kabla ya kuingia kwenye macro economics

  michicha na kisamvu vimekosa masoko
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  JF tusikose kupata up dates ni muhimu kujua prof anazungumzia nini kuhusu uchumi.
   
 4. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  anaenda kutoa kadi za wanachana wao wapya
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Prof njoo umwage madini maana mchumi mwenzako wa GPA 2.0 anatuzingua!
   
 6. Magu

  Magu Senior Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Vizuri lakini liwe kongamano la uchumi na siyo la siasa za kibongo zinazoishia vurugu na maandamano yasiyo na tija na kupoteza dhana nzima ya kongamano. Hivi prof amekuwa mpya au ni yuleyule tunaemjua aliyemshauri Mzee mwinyi na kushindwa kabisa katika nyanja ya uchumi kwa kuingia katika trade liberalization pasipo kuwa na control ys inflation uchumi wenye udalali?
   
 7. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,682
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Prof. amerudi kwa kasi....:wink2:
   
 8. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mawazo mgando badala akakutane na kikwete amshauri kuhusu uchumi wetu
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Atakutana na Islamic University ya Morogoro lini?
   
 10. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Karibu Prof lupumba,ila isiwe kichama liwe kongamano huru
   
 11. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,557
  Trophy Points: 280
  Akajenge chama chake asituletee lecture hapa! Of course ni Prof wa uchumi na anajua kuelezea uchumi kweli! Lakini ukombozi tunaoutaka si lecture zake za uchumi!
   
 12. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280

  Ha ha haaaa!Mkuu kumbuka huyo ni Rais wako na taifa zima lakini!!
   
 13. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Eti wamemuomba!!!!!!!!! makamu wa pili wa rais nchi jirani ya zanzibar@ kwiii kwiiii kwii kwiii
   
 14. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Yaan vyuo vyote hivyo alipata wanachuo 60 walioenda kumsikiliza...kwel RIP CUF
   
 15. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  huo ndo wajibu wake kwenye siasa alijichanganya..ubovu ni kwamba kwenye siasa hatumii hata robo ya utalamu wake zaidi ya kuwarubuni wananchi...
   
 16. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Sisi hatutaki u prof wakuandika vitabu na ku publish paper ambao utekelezaji wake ni zero kama lipumba ndiye aliyekuwa anamshauri mzee mwinyi na wote tuliyaona madudu ya kipindi kile hali ilivyokuwa mbaya kwa serikali huo uchumi wake wa kwenye vitabu hauna maana bora aende akafundishe vijana wetu hafai kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi pamoja na hayo ma gpa yake yeye ni kilaza tu kwenye implementation
   
 17. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #17
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK anzid kuua uchumi wa nchi yetu bora aondoke haraka.KARIBU DOM.PROF.
   
Loading...