Lipumba: Kazi ya Makamba ni kuisambaratisha CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: Kazi ya Makamba ni kuisambaratisha CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, May 13, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amewapuuza wanasiasa wanaobeza hatua yake ya kutangaza nia ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba.

  Akizungumzia kauli iliyotolewa na Bw. Yusufu Makamba dhidi yake kuwa kusimama kwake kugombea kazi itakuwa ni rahisi kwa CCM, Prof. Lipumba alisema kuwa tangu Bw. Makamba achaguliwe kuwa Katibu Mkuu amekuwa akiwasaidia (wapinzani) kukisambaratisha chama tawala.


  "Katika kazi ambayo anatusaidia Bw. Makamba ni kukisambaratisha chama chake, karibu viongozi wote wa CCM ukiwauliza Makamba ana kazi gani kwenye chama wanakwambia kabisa kwamba hana lolote, wanashindwa tu kuwa wawazi na kusema ukweli, lakini Makamba hatakiwi CCM.


  "Tangu alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu chama kimekuwa katika hali ya mapandemapande, amechangia kwa kiasi kikubwa kukisambaratisha," alisema.


  Alisema kuwa Rais Kikwete asipokuwa makini na Bw. Makamba na kuendeleza usanii wake utasambaratisha nchi nzima.


  Mwishoni mwa wiki hii, Prof. Lipumba alitangaza nia yake ya kuwania tena urais, lakini baadhi ya watu wakiemo viongozi na wanasiasa walimkejeli kwa uamuzi huo.


  Chanzo: Majira
   
 2. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Sielewi baadhi ya watu wanaolalamikia kitendo cha watu kugombea urais mara nyingi...Kumbukeni rais was sasa wa Senegal, Wade - aligombea urais kupitia upinzani tangu miaka ya 1979 na kufanikiwa kushinda in late 1990's. Na kuna mifano mingi duniani na watu wameishia kushinda.
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kama Makamba anaisambaratisha CCM basi LIPUMBA anatakiwa kumsifu na si kumkejeli
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  simwungi lipumba mkono lakini aliyosema kuhusu makamba ni kweli
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Makamba alipopewa ukatibu mkuu wa CCM na swahiba wake alikuwa na mtazamo w kizamani wa kutumia "MKONO WA CHUMA" kuendesha chama kama alivyofanya akiwa mkuu wa mkoa, yaani kuuliza watu maswali mbele ya raia na kuwatoa nishai na hata kuwafuta kazi, kitu ambacho kimemshinda CCM na kujikuta akiwa katikati ya njia panda mguu huu upo kwa mafisadi na huu upo kwa wazalendo matokeo yake kawa mdooooooogoooo na porojo zake za kukopi biblia na misahafu zimekwenda na maji.
   
 6. G

  Godwine JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  lakini kwa upande wa lipumba kusema madhaifu ya makamba . je anataka ccm wachague katibu mwingine
  mzuri atayekiimarisha chama na kufanya upinzani upungue kasi? tulipenda siku moja tuone uwiano wa wawakilishi
  katika bunge, unajua kila anayelitakia mema taifa hili anatakiwa kuomba siku moja kuwe na uwiano wa wawakilishi
  katika bunge, kwani kutawezesha kuwa na sheria bora urais si muhimu kusema achukue nani kwani kama kutakuwa
  na wawakilishi bora basi na rais atakuwa makini pia
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mwacheni Lipumba agombee URAIS hata mara mia kwani ATAFUTAE HACHOKI UKIONA AMECHOKA UJUE AMEPATA!!
   
 8. k

  kaiya Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Bwana Lipumba, Usimuamshe alielala......
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hakumkejeli kamwambia ukweli kuwa kwa kukisambaratisha chama chake anawasaidia wapinzani
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Umesema kweli alipokuwa mkuu wa mkoa Dar alikuwa akiwaendesha watu hata viongozi wenzake kijeshi utakuta anamdhalilisha hadharani mkuu wa wilaya kwa kumwomyesha kidole bila aibu.
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hiki kizee kimesema kikifika miaka 74 kitakufa kiacheni tu
   
 12. S

  Selemani JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  What would you expect Lipumba to say about Mzee Makamba? That he is doing a good job? He should be more concerned and asking himself hivi CUF hakuna vichwa vingine vya kugombea urais? This guy has been on a ballot with Mkapa (twice) and now with JK twice. I'm thinking there are more ground for self awareness and democracy in CCM than in CUF.

  Maybe he is a career presidential candidate, not necessarily he want to become a President. He just enjoys the perks and marupurupu that comes with the campaign. This says a lot about a party (CUF) that wants us to trust them to lead the country, but they can't even get rid of their career presidential candidates, that is Maalim Seif included.
   
 13. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa wetu bwana! Sasa profesa wa uchumi uliyebobea katika fani na mwanasiasa mahiri unatakiwa uombe makamba aendelee hivyo hivyo ili arahisishe wewe kuingia ikulu AU ndiyo hadithi ya sungura na zabibu?????????????
   
 14. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Lipumba Gombea Mkuu. Hiyo ndo demokrasia halisi. Atafutaye hachoki!
   
 15. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #15
  May 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Jamani wacheni wivu kwani huyu mzee alikubaliwa na mkutano mkuu wa chama chake [ambacho wengi tunakiponda]. Kwa wale waliomteua wanaona anafaa kwa kazi hiyo kwa vigezo ambavyo mimi na wewe hatuvijui na kama tukitaka kumpima uwezo wake kwa kutumia chaguzi ndogo zilizofanyika katika kipindi chake majibu yako wazi na kama mnasema uzee wake ni liabilitiy kwa ccm basi inatakiwa wale wapinzani wa chama tawala wafurahi maana kwa vile siasa zake zimepitwa na wakati basi kushindwa kwa ccm itakuwa rahisi.
   
 16. M

  Mutabora Member

  #16
  May 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Makamba hana jipya kama walivyo hao wanaomtuhumu.....hivi ni kweli CUF haikusambaratika Tz Bara.Big up Lwakatare!
   
 17. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Lipumba anamtuhumu Makamba kwa kuwasaidia wapinzani na hapohapo yeye anafanyakazi ya kuwasidia ccm kwa kumwonyesha Kikwete, Makamba hafai.
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Siri hii alipaswa kubaki nayo LIPUMBA lakini kwa kuwa yeye yupo upinzani kuisaidia CCM basi ameamua kuiweka wazi.
  Hii inaonesha between lines how most upinzanis are in line na chama tawala na wapo huko kuhakikisha wanatoa upinzani bandia. Ndo maana haachi kugombea huyu hataki kumpisha mwingine kuchukua kijiti.

  Tuna wapinzani wa kweli wachache mno nakwambia
   
 19. M

  MC JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mkuu RE,
  Umemuunga Lipumba mkono!
   
 20. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kaenda Iringa kwa kazi hiyo hiyo kuwachanganya vijana lakini wamemuonya asijaribu kuegemea upande wowote
   
Loading...