Lipumba: Katiba ndio iwe kumbukumbu ya Jakaya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: Katiba ndio iwe kumbukumbu ya Jakaya Kikwete

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by nngu007, Mar 24, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha kuwa suala la katiba mpya linafanikiwa wakati wa utawala wake ili kujiwekea historia ya
  kukumbukwa na Watanzania.

  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ametoa kauli hiyo wakati akihutubia wananchi wa mji wa Muheza katika mwendeleza wa mikutano ya 'kuwazindua Watanzania kukiunga mkono chama hicho'.

  Profesa Lipumba alisema pamoja na Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru, ni vema katiba mpya itakayozaa Tume Huru ya Uchaguzi ipatikane wakati wa utawala wake.

  "Mtani wangu Kikwete pamoja na kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi katika miaka 50 tangu uhuru, walau hili la katiba mpya lifanikiwe chini ya utawala wako ili Watanzania wakukumbuke kuwa ulileta mabadiliko makubwa ya demokrasia," alisema Profesa Lipumba.

  Alisema CUF kina dhamira ya dhati ya kuwaletea ukombozi wa kweli Watanzania ndio maana kinafuata misingi ya kikatiba kutaka kuingia madarakani tofauti ya baadhi ya vyama vinavyotaka kuingia madarakani kwa njia ya maandamano.

  "Katika ilani ya uchaguzi ya CCM, hakuna kipengele chochote kilichozungumzia mabadiliko ya katiba lakini sisi CUF tuliwasilisha rasimu ya katiba ili tuweze kupata tume huru ya uchaguzi na wananchi waweze kutoa ridhaa ya kuwachagua viongozi wanaowataka," alisema Prof. Lipumba

  Alisema baada ya rasimu hiyo ya katiba, Rais Jakaya Kikwete alikubali na kuliambia bunge kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuandikwa katiba mpya, sasa ni vema akahakikisha anasimamia mchakato mzima wa katiba ufanikiwe chini ya utawala wake ili kujiwekea historia kwa Watanzania.

  "Vinginevyo Mheshimiwa Kikwete ukishindwa hili katika utawala wako, basi utakuwa ndio msanii wa kwanza kuwa rais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Profesa Lipumba.

  Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema hali ya maisha ya Watanzania imezidi kuwa mbaya huku wanafunzi wakiishia kula mlo mmoja kwa siku.

  Bw. Mtatiro alisema hayo baada ya mtoto wa darasa la tatu kuitwa jukwaani na kuulizwa alikula nini tangu alipoamka asubuhi, naye akajibu kuwa alikuwa hajala kitu.

  "Watoto wa aina hii hawako Muheza peke yake ni Tanzania nzima wanakwenda shule na kula mlo mmoja jioni, watoto wa aina hii hawafundishiki darasani ndio maana matokeo ya mitihani yanakuwa mabovu, mtoto anamaliza darasa la saba hajui kusoma kitabu cha darasa la pili," alisema Bw. Mtatiro.
   
Loading...