Lipumba, it is time to hang the gloves up!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
Profesa Haruna Ngunguri Lipumba,

Nakuandikia waraka huu wa kiuchungaji ilhali najua marafiki zangu wa CUF watacharuka na kudai naingiia mambo ya ndani.

Leo hii nimewaandikia Chadema, Nimewaandikia CCM na sasa nakuandikia wewe.

Kwa maoni yangu binafsi, nafikiri sasa ni wakti muafaka wa wewe kutafuta mtu mwingine wa kushika hatamu za kuongoza CUF. Kama vile nilivyomtaka Freeman Mbowe aachie manyanga ya Uenyekiti Chadema, naomba nitangulize mkono wangu wa shukrani na kukuomba sasa upumzike, tafuta damu mpya na yenye nguvu yenye uwezo wa kukijenga CUF upya na kwa ushirikiano wa wenzi kutoka Zanzibar.

Sijasema usigombee tena Urais, bali ujivue Uenyekiti wa CUF.

Chama chako kimejitahidi sana kupata viti vya kutosha kwenye TAMISEMI, lakini nafikiri ni wazi ili kuata majimbo mengi ya Ubunge hasa Tanzani aBara, kunahitajika sauti mpya ambayo itafnya kazi ya kuchuana na Msekwa na Makamba na hata pendekezo lango kuwa Sr. Slaa na Lwakatare wawe dynamic duo ya Chadema.

Je umeshawahi kukaa chini na kutafakari ni nani ndani ya Chama chako ambaye unamjenga na kumuandaa awe Mwenyekiti na kukiongoza chama?

Ukirudi kuangalia matokeo ya Ubunge, utabaini kuwa unahitaji mtu mwenye nguvu kubwa huku Bara, swa na Maalim kule Unguja ili kuweza kuongeza uwakilishi wa CUF katika kila mkoa. Njua Chama chako kimegombea Tonge na Chadema na wote mnataka kumpokonya CCM, lakini kwa mwendo huu wa kukosa nguvu nzuri kuongoza Chama kiutendaji kila siku, ni wazi 2015 matokeo yatakuwa yale yale, pamoja na matunda mazuri ya Muafaka kule Zanzibar.

Labda nikuulize, je CUF kuna CUF Zanibar na CUF Tanzania bara? Je Muafaka ni wa upande mmoja tuu wa Muungano?

Je kama Msomi n Mchumi aliyebobea, unapimaje matokeo ya Uongozi wako?

Mwaka 2015, tunahitaji ushndani mzuri, CUF imefanya vyema kujikita katika TAMISEMI na niliona juhudi zenu 2009 na hata mwaka huu. Lakini nafikiri Chama kinahitaji nguvu moya na sura mpya kukiongoza. Mara nyingine mabadiliko husaidia kuleta mwamko mpya na ndio maana kwako nakuomba utafute mpya na kule Chadema nawaambia wana mtu mwenye uwezo wa kukijenga upya Chama.

Miaka hii mitano inayokuja, inahitaji mtu achacharike kila siku kujenga Chama na kufika kila kona. Najua una majukumu makubwa sana ya kikazi ambayo si ya CUF kwa kutokana na umashuhuri wako kama Mchumi kufahamika duniani.

Basi fanya hima uachie mtu mwingine ashikilie usukani akusaidie kukijenga Chama na ikifika 2015, kazi yako iwe ni kuchukua fomu kugombea Urais.

Ni hayo tuu, kutoka kwa Mchungaji Kishoka.
 
Haki

JF-Expert Member
Jan 14, 2009
356
0
Lipumba siyo tatizo la CUF kutokuwa na washabiki wengi bara. Siasa za Tanzania zinaubaguzi wa Kidini. Sababu kubwa ambayo imeibadilisha CUF ktk kipindi alichokuwa JK ni Udini. Wakati wa Mkapa, CUF iliweza kuwa na washabiki wengi sana kwa sababu Waislamu wengi walikuwa wanaamini kwamba Mkapa hawatendei haki.
Alipochukua JK, Waislamu wengi hawakuona umuhimu wa CUF. Kwa mujibu wa sheria za CCM, Rais atakaekuja lazima awe Mkristo. Mwaka 2015 utaona Waislamu wengi wataanza kukipigia kura CUF. Especially,ukiangalia Chadema inatawaliwa zaidi na Wakristo.
Siasa za TZ zinamwelekeo wa Kidini zaidi. Angalia kura za Chadema, zimetawaliwa zaidi na sehemu ambazo kuna Wakristo wengi, na angalia kura za CUF, utaona zinatawaliwa zaidi na sehemu zenye Waislamu zaidi.
 
Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727

Mods wa JF ondoeni hii posti, haina maslahi ya kitaifa
 
WABUSH

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
285
0
Mkuu nadhani umeandika sana leo, kaa chini u-reflect, otherwise naona umeanza chai tupu tena bila sukari
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,693
1,250
Lipumba siyo tatizo la CUF kutokuwa na washabiki wengi bara. Siasa za Tanzania zinaubaguzi wa Kidini. Sababu kubwa ambayo imeibadilisha CUF ktk kipindi alichokuwa JK ni Udini. Wakati wa Mkapa, CUF iliweza kuwa na washabiki wengi sana kwa sababu Waislamu wengi walikuwa wanaamini kwamba Mkapa hawatendei haki.
Alipochukua JK, Waislamu wengi hawakuona umuhimu wa CUF. Kwa mujibu wa sheria za CCM, Rais atakaekuja lazima awe Mkristo. Mwaka 2015 utaona Waislamu wengi wataanza kukipigia kura CUF. Especially,ukiangalia Chadema inatawaliwa zaidi na Wakristo.
Siasa za TZ zinamwelekeo wa Kidini zaidi. Angalia kura za Chadema, zimetawaliwa zaidi na sehemu ambazo kuna Wakristo wengi, na angalia kura za CUF, utaona zinatawaliwa zaidi na sehemu zenye Waislamu zaidi.
The Following User Says Thank You to Haki For This Useful Post:

Mchukia Fisadi (Today)​
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,693
1,250
Lipumba siyo tatizo la CUF kutokuwa na washabiki wengi bara. Siasa za Tanzania zinaubaguzi wa Kidini. Sababu kubwa ambayo imeibadilisha CUF ktk kipindi alichokuwa JK ni Udini. Wakati wa Mkapa, CUF iliweza kuwa na washabiki wengi sana kwa sababu Waislamu wengi walikuwa wanaamini kwamba Mkapa hawatendei haki.
Alipochukua JK, Waislamu wengi hawakuona umuhimu wa CUF. Kwa mujibu wa sheria za CCM, Rais atakaekuja lazima awe Mkristo. Mwaka 2015 utaona Waislamu wengi wataanza kukipigia kura CUF. Especially,ukiangalia Chadema inatawaliwa zaidi na Wakristo.
Siasa za TZ zinamwelekeo wa Kidini zaidi. Angalia kura za Chadema, zimetawaliwa zaidi na sehemu ambazo kuna Wakristo wengi, na angalia kura za CUF, utaona zinatawaliwa zaidi na sehemu zenye Waislamu zaidi.
Originally Posted by Haki Mods wa JF ondoeni hii posti, haina maslahi ya kitaifa
Ni sura ya ukweli kabisa Moderator naomba usiiondoe
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,978
2,000
Alichosema Haki ni lazima kitiliwe maanani. Tuanze kujiuliza tumefikaje hapa kama tutakuja kukubaliana nae. Hoja yake ni legitimate mno.

Amandla........
 
Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
1,195
Profesa Haruna Ngunguri Lipumba,

Nakuandikia waraka huu wa kiuchungaji ilhali najua marafiki zangu wa CUF watacharuka na kudai naingiia mambo ya ndani.

Leo hii nimewaandikia Chadema, Nimewaandikia CCM na sasa nakuandikia wewe.

Kwa maoni yangu binafsi, nafikiri sasa ni wakti muafaka wa wewe kutafuta mtu mwingine wa kushika hatamu za kuongoza CUF. Kama vile nilivyomtaka Freeman Mbowe aachie manyanga ya Uenyekiti Chadema, naomba nitangulize mkono wangu wa shukrani na kukuomba sasa upumzike, tafuta damu mpya na yenye nguvu yenye uwezo wa kukijenga CUF upya na kwa ushirikiano wa wenzi kutoka Zanzibar.

Sijasema usigombee tena Urais, bali ujivue Uenyekiti wa CUF.

Chama chako kimejitahidi sana kupata viti vya kutosha kwenye TAMISEMI, lakini nafikiri ni wazi ili kuata majimbo mengi ya Ubunge hasa Tanzani aBara, kunahitajika sauti mpya ambayo itafnya kazi ya kuchuana na Msekwa na Makamba na hata pendekezo lango kuwa Sr. Slaa na Lwakatare wawe dynamic duo ya Chadema.

Je umeshawahi kukaa chini na kutafakari ni nani ndani ya Chama chako ambaye unamjenga na kumuandaa awe Mwenyekiti na kukiongoza chama?

Ukirudi kuangalia matokeo ya Ubunge, utabaini kuwa unahitaji mtu mwenye nguvu kubwa huku Bara, swa na Maalim kule Unguja ili kuweza kuongeza uwakilishi wa CUF katika kila mkoa. Njua Chama chako kimegombea Tonge na Chadema na wote mnataka kumpokonya CCM, lakini kwa mwendo huu wa kukosa nguvu nzuri kuongoza Chama kiutendaji kila siku, ni wazi 2015 matokeo yatakuwa yale yale, pamoja na matunda mazuri ya Muafaka kule Zanzibar.

Labda nikuulize, je CUF kuna CUF Zanibar na CUF Tanzania bara? Je Muafaka ni wa upande mmoja tuu wa Muungano?

Je kama Msomi n Mchumi aliyebobea, unapimaje matokeo ya Uongozi wako?

Mwaka 2015, tunahitaji ushndani mzuri, CUF imefanya vyema kujikita katika TAMISEMI na niliona juhudi zenu 2009 na hata mwaka huu. Lakini nafikiri Chama kinahitaji nguvu moya na sura mpya kukiongoza. Mara nyingine mabadiliko husaidia kuleta mwamko mpya na ndio maana kwako nakuomba utafute mpya na kule Chadema nawaambia wana mtu mwenye uwezo wa kukijenga upya Chama.

Miaka hii mitano inayokuja, inahitaji mtu achacharike kila siku kujenga Chama na kufika kila kona. Najua una majukumu makubwa sana ya kikazi ambayo si ya CUF kwa kutokana na umashuhuri wako kama Mchumi kufahamika duniani.

Basi fanya hima uachie mtu mwingine ashikilie usukani akusaidie kukijenga Chama na ikifika 2015, kazi yako iwe ni kuchukua fomu kugombea Urais.

Ni hayo tuu, kutoka kwa Mchungaji Kishoka.
Lazima apigwe vita tuu humu ukizingatia chama chake kimekuwa cha pili!
 
MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,566
1,195
Lipumba siyo tatizo la CUF kutokuwa na washabiki wengi bara. Siasa za Tanzania zinaubaguzi wa Kidini. Sababu kubwa ambayo imeibadilisha CUF ktk kipindi alichokuwa JK ni Udini. Wakati wa Mkapa, CUF iliweza kuwa na washabiki wengi sana kwa sababu Waislamu wengi walikuwa wanaamini kwamba Mkapa hawatendei haki.
Alipochukua JK, Waislamu wengi hawakuona umuhimu wa CUF. Kwa mujibu wa sheria za CCM, Rais atakaekuja lazima awe Mkristo. Mwaka 2015 utaona Waislamu wengi wataanza kukipigia kura CUF. Especially,ukiangalia Chadema inatawaliwa zaidi na Wakristo.
Siasa za TZ zinamwelekeo wa Kidini zaidi. Angalia kura za Chadema, zimetawaliwa zaidi na sehemu ambazo kuna Wakristo wengi, na angalia kura za CUF, utaona zinatawaliwa zaidi na sehemu zenye Waislamu zaidi.

Mkuu Haki ulicho sema kina ukweli ndani yake japo Watanzania wengi ni wanafiki na hawawezi kukubali kamwe kwamba wana kipigia chama au mgombea kwa misingi ya dini. Aidha kuna wale wanaofanya hivyo kwa makusudi au kuna wali ambao huji kuta wanampenda mgombea wa dini yao bila kujua kwamba dini zinazo fanana ndizo zime wavuta kwa huyo mgombea.

Angalia hata humu JF. Kuna watu wanaomtetea JK (angalia kiundani uta kuta wanamtetea kwa sababu ni dini moja) na Mwinyi kwa nguvu zote lakini linapo fika swala la kumuongelea Mwl Nyerere au Mkapa angalia majibu yao. Ukiangalia kiundani kabisa una kuta kabisa kwamba huyu mtu anamtetea fulani kwa sababu ya dini zao zinazo fanana ila kamwe huyo mtu hawezi kukubali ukweli huo.

Na nisionekane naonea ndugu zangu Waislamu. Kuna Wakristo wako hivyo hivyo pia. Kuna watu wana kipinga CUF simply because kina onekana ni chama cha Waislamu hata bila hoja za msingi. Mtu halazimishwi kupenda chama fulani ila kwa maongezi tu ya kawaida unaona kabisa kwamba fulani anampinga au kumtetea fulani kwa sababu ya dini.

In reality dini ni kifaa kikubwa sana kwenye siasa. Njia moja wapo kubwa ya kutafuta support ni kulazimisha watu wajihisi kwama ni "us against them". Sasa kwa Tanzania ukiangalia makabila yapo mengi mno na hata yale makubwa ukichukua ratio kwa kulinganisha na Watanzania wengi unakuta wao sio big majority. Kenya ambapo kuna makabila ambao ni wazi wana asilimia kubwa ya watu ndiyo unaona ukabila lakini kwa Tanzania huwezi. Sasa nini kinacho fuata? Ni dini. Na ukiangalia Waislamu na Wakritso Tanzania ni almost 50/50 kwa hiyo kutumia udini ina make sense zaidi.

Siyo siri CCM are smart. Ukiangalia CCM ni vigumu sana kusema kwamba kina tawaliwa zaidi na watu wa dini fulani. Huwezi kusema kwamba ni Waislamu au Wakristo ndiyo wenye nguvu ndani ya CCM. Na ukiangalia kiundani zaidi wao wana pokezana siyo kiZanzibar na Kitanganyika bali kwa kuangalia dini. Haswa kwenye uraisi hawa taki kuweka wagombea wa dini moja tu mpaka ionekane wana upendeleo. Ndiyo maana CCM ina nguvu kwa maana wale wapiga kura radicals wata pigia kura vyama wanavyo ona ni vya dini yao lakini wale moderates ambao kwa nchi yoyote ile ndiyo wengi zaidi wata pigia kura chama kinacho onekana hakiegemei upande mmoja. CUF wanaonekana Waislamu, Chadema wanaonekana Wakristo, mpiga kura moderate mnadhani ata kimbilia wapi?

Kwa mtazamo wangu mimi nadhani taifa lina hitaji some sort of nation building again kama vile tulivyo kuwa nayo baada ya uhuru. Ni wakati wa kujaribu kuwaonyesha Watanzania kwamba wao ni wamoja. Tuweke utaifa mbele ya udini. Tukazania vile vinavyo tuunganisha badala ya kutu tenganisha. Tukatae au tukubali kuna elements za udini kwenye siasa zetu. Na ni jukumu la vyama kujaribu kuonyesha uiano kwa kadri ya uwezo wao. Tanzania chama cha siasa kikionekana tu kinaelemea upande fulani wa dini iwe ni kweli au la basi hicho chama kisha commit political suicide.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
..mbona mimi naona kama udini unakuwa exaggerated humu kwenye mitandao.

..kwa mtizamo wangu wa-Tanzania walio wengi hawana imani kali ya kidini kiasi cha kuweza kumbagua mtu wa imani tofauti.

..kuna Waislamu kibao wanakunywa pombe, na wa-Kristo lukuki wenye wake zaidi ya mmoja.

..mimi nadhani wapinzani wameangushwa na suala la MAANDALIZI na RESOURCES.

..Dr.Slaa na Prof.Lipumba wamefanya mikutano michache na kutumia fedha na resources kidogo kulinganisha na JK.
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
6,258
2,000
HAKIKA, HAKIKA, ni barua njema kabisa na imfikie mlengwa basi. ama hamjamualika Jamvini? Demokrasia ya kweli ndio hii, na jumbe kama hizi ndizo zinahitajika. Ni kweli faida za usomi ni kutafiti na kutathmini, msomi yoyote asiyeamini na kutembea katika hayo si msomi ni bubusa:glasses-nerdy: BIIIG UP

MJADALA MZURI SANA HUU -KUNA POINTS NYINGI NA ZAIDI YA UKWELI TOKA KWA WALIOCHANGIA INAPENDEZA SANA.
 
Zion Train

JF-Expert Member
Jun 5, 2008
503
195
Lipumba siyo tatizo la CUF kutokuwa na washabiki wengi bara. Siasa za Tanzania zinaubaguzi wa Kidini. Sababu kubwa ambayo imeibadilisha CUF ktk kipindi alichokuwa JK ni Udini. Wakati wa Mkapa, CUF iliweza kuwa na washabiki wengi sana kwa sababu Waislamu wengi walikuwa wanaamini kwamba Mkapa hawatendei haki.
Alipochukua JK, Waislamu wengi hawakuona umuhimu wa CUF. Kwa mujibu wa sheria za CCM, Rais atakaekuja lazima awe Mkristo. Mwaka 2015 utaona Waislamu wengi wataanza kukipigia kura CUF. Especially,ukiangalia Chadema inatawaliwa zaidi na Wakristo.
Siasa za TZ zinamwelekeo wa Kidini zaidi. Angalia kura za Chadema, zimetawaliwa zaidi na sehemu ambazo kuna Wakristo wengi, na angalia kura za CUF, utaona zinatawaliwa zaidi na sehemu zenye Waislamu zaidi.
nakubaliana na wewe kabisa, udini unatawala sana katika siasa za tanzania, ni mfano mdogo tu ambao nimeshuhudia mwenyewe, nilienda kuswali swala ya eid ktk msikiti wa magomeni,nilikuwa na mwanangu wa miaka 5, baada ya swala kabla haijaanza hotuba ya eid yule imam wa msikiti niliosali akasema: ndugu zangu waislam tusome duwaa ya pamoja tuwaombee wale wote waislam katika uchaguzi huu washinde,haijalisha huwezo wake wala ni nani mradi tu muislam, nilichukia sana na mimaneno yake, lakini asilimia kubwa ya waliokuwepo pale wakasoma hiyo duwaa, embu angalieni upumbavu huu wa kidini. mimi nasema uislam na ukristo hupo sana kwenye siasa za hapa kwetu, waheshimiwa wanaotoongoza badala ya kuondosha hizo itikadi wao ndiyo wanapalilia
 
Top Bottom