Lipumba Huyu Ndiye Aliyesifiwa sana na CUF

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
M. M. Mwanakijiji

Kwa muda mrefu Profesa Ibrahim Lipumba alisifiwa sana na kuinuliwa miongoni mwa wanasiasa wa upinzani. Alisifiwa kiasi kwamba ilikuwa ni kama nyota ya jaha aliposimama mbele ya wana CUF. Alikuwa ni alama ya CUF, alikuwani "msomi aliyebobea" na alisifiwa kwa mafanikio yake mbalimbali ya kitaaluma ndani na nje ya nchi.

Tuliambiwa kuwa kutokana na ujuzi wake uliobobea katika uchumi Tanzania ilimhitaji sana; ilimhitaji kwa kuwa alikuwa ni mbobezi katika ushauri wa mambo mbalimbali ya uchumi. Ni kwa sababu hiyo CUF walimsimamisha mara nne kugombea Urais! Hawakuwa na mwingine na haikuonekana uwezekano wa kuwa na mwingine. Lipumba hakuwa pumba!

Alionekana kuwa ni mwanasiasa mahiri kwa jinsi ambavyo alishiriki kuwavutia wasomi wengi kwenye chama cha CUF na wakati huo huo alionekana kubeba matumaini ya kundi moja nchini ambalo lilimuona kama alama ya uwezo na kufanikiwa kwa mwana kundi hilo (rejea video yake "ile").

CUF ilikuwa inahusishwa na Lipumba huku Bara na Seif Hamad kule Zanzibar na hawa wawili kwa kweli ndio walikuwa CUF hasa. Leo hii kugawanyika kwa hawa wawili tu tayari kumeigawa CUF katika vipande ambavyo hatujaona mwisho wake bado. Mgawanyiko uliotokea si wa kidini bali ni wa kisiasa na tena ni siasa ambazo ni ngumu mno kuzielezea kwani siyo suala la kiitikadi au kimsimamo bali zaidi ni maslahi ya aina fulani.

Lipumba huyu huyu ambaye alisifiwa sana na alitaka hata kugombea Urais - mara nne! Anatuonesha uwezo wake (au kukosa uwezo kwake) kutatuta tatizo la kisiasa ndani ya chama chake na badala yake kama wanasiasa wengine wa zama zetu naye ameamua kuwa gangwe tu.

Zile sifa zile... zimejaribiwa... na watu wanaweza kuamua kama kweli zilimfaa kweli au la. Au ndio kusoma kwingi...
 
Msaliti anapojidhihirisha hadharani basi hakuna sababu yoyote ya kumuogopa bali ni kumpa za uso tu kuhusu usaliti wake wa kutumika na chama cha wahuni na mafisadi ili kuusambaratisha upinzani nchini.
 
Lipumba ameshindwa kutumia akili zake badala yake anatumia akili ya wana ccm wanaotaka nchi hii iwe ya mazezeta wa kukubali kila jambo. matumizi ya li- yaani wakati ulopita maanayake ni kwamba enzi zake zimepita pale alipohongeka (kutongozwa) na ccm.
 
Ni wewe pia uliekuwa ukiiponda sana CCM katika makala zako kwenye magazeti na mitandaoni.
Mkuu inategemea CCM ilikuwa inafanya nini wakati huo na sasa inafanya nini. Ni kama vile ambavyo CDM walimponda sana Mzee Edward Lowassa na baade wakaja kumsifia sana, hadi sasa wanamuheshimu na kumsifia. Hizo ndio siasa na watu wanaozifanya siasa hubadilika kitabia na misimamo kulingana na mabadiliko ya nyakati au matukio.
 
Kwa mfano ni kipi kilichobadilika katika ccm ?
 
Lipumba ameacha kuwa mwanasiasa kwa sasa ni mtendaji mkuu na wakala wa shetani kuharibu na kubomoa nguvu ya CUF kule zanzbar,kwani inajulikana wazi kivumbi cha 2015 CCM hawatataka kukumbana nacho.
Lakini kwa anaetizama mbele ataona kuwa hili ni kosa kubwa kiufundi kwani siku ikitokea CUF zanzibar ikiungana rasmi na CHADEMA wamekwisha!
 
Mkuu inategemea CCM ilikuwa inafanya nini wakati huo na sasa inafanya nini. Ni kama vile ambavyo CDM walimponda sana Mzee Edward Lowassa na baade wakaja kumsifia sana, hadi sasa wanamuheshimu na kumsifia. Hizo ndio siasa na watu wanaozifanya siasa hubadilika kitabia na misimamo kulingana na mabadiliko ya nyakati au matukio.
Adui yetu mkubwa ni CCM na mfumo wake hivyo yoyote atakaesaidi kuiondo CCM madarakani nitamuunga mkono.

Lowassa alieko CHADEMA ni bora mara 100 kuliko bwana yule alie CCM leo hii.

Silaha yoyote ya kisiasa na ambayo ni ya kikatiba itakyoweza kuiondoa CCM madarakani nitaiunga mkono hata kama itakuwa ni silaha ya maangamizi kama alivyokuwa Lowassa.
 
Sasa huku kumtumia kwao Lipumba ili aisambaratishe CUF na UKAWA kusije kukawatokea puani kwa chama kingine kuneemeka zaidi kule Zenj kuliko hata ilivyokuwa CUF.

Back
Top Bottom