Lipumba: CCM inaendesha nchi kibabe

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
10
Points
0

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 10 0
Tanzania Daima

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaendesha nchi kibabe bila kuheshimu uhuru wa mahakama.
Akihutubia mkutano wa hadhara juzi katika viwanja vya Kiwalani, Dar es Salaam, baada ya kuwashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kuwachagua Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kupitia CUF, Profesa alisema CCM imeshindwa kuonyesha demokrasia kwa vile imekuwa ikiingilia mambo mengi ya kisheria.
Lipumba alisema Mahakama Kuu iliamua kuwepo na mgombea binafsi lakini kutokana na uoga CCM imekataa kwa vile inahofia kupoteza madaraka.
“Kama kungekuwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) huru na yenye haki hata chaguzi ndogo sita zilizowahi kufanyika ilitakiwa mgombea binafsi aruhusiwa kugombea!” alisema Lipumba.
Kuhusu suala la ufisadi, alisema anashangazwa na jinsi wabunge wachache waliojiita wapambanaji walivyoshindwa kumaliza suala la kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond hadi Bunge kuamua kufunga mjadala huo.
Kuhusu sakata la rada, Profesa Lipumba alisema aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge ndiye anayehusika lakini katika hali ya kushangaza ameendelea kushika madaraka ndani ya CCM badala ya kufikishwa mahakamani.
 
Baraghash

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Messages
2,717
Likes
1,726
Points
280

Baraghash

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2012
2,717 1,726 280
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaendesha nchi kibabe bila kuheshimu uhuru wa mahakama.
Sahihisho:MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF),anaetambuliwa na Msajili, Profesa Ibrahim Lipumba amesema ............
Profesa alisema CCM imeshindwa kuonyesha demokrasia kwa vile imekuwa ikiingilia mambo mengi ya kisheria
Hivi kuvamia ofisi za CUF na kuvunja kufuli ndio njia sahihi za Profesa kuonyesha demokrasia kwa vile amekuwa hakuingilia mambo ya kisheria
hali ya kushangaza ameendelea kushika madaraka ndani ya CCM badala ya kufikishwa mahakamani.
Hali ya kushangaza Profesa Lipumba ameendelea kushika madaraka ndani ya CUF licha ya kujiuzulu na kuufukuzwa, badala ya kujiunga na chama kinachomfadhili?
 
sayoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Messages
1,482
Likes
1,210
Points
280

sayoo

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2014
1,482 1,210 280
Tanzania Daima

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaendesha nchi kibabe bila kuheshimu uhuru wa mahakama.
Akihutubia mkutano wa hadhara juzi katika viwanja vya Kiwalani, Dar es Salaam, baada ya kuwashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kuwachagua Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kupitia CUF, Profesa alisema CCM imeshindwa kuonyesha demokrasia kwa vile imekuwa ikiingilia mambo mengi ya kisheria.
Lipumba alisema Mahakama Kuu iliamua kuwepo na mgombea binafsi lakini kutokana na uoga CCM imekataa kwa vile inahofia kupoteza madaraka.
“Kama kungekuwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) huru na yenye haki hata chaguzi ndogo sita zilizowahi kufanyika ilitakiwa mgombea binafsi aruhusiwa kugombea!” alisema Lipumba.
Kuhusu suala la ufisadi, alisema anashangazwa na jinsi wabunge wachache waliojiita wapambanaji walivyoshindwa kumaliza suala la kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond hadi Bunge kuamua kufunga mjadala huo.
Kuhusu sakata la rada, Profesa Lipumba alisema aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge ndiye anayehusika lakini katika hali ya kushangaza ameendelea kushika madaraka ndani ya CCM badala ya kufikishwa mahakamani.
Ahhhhhhhhhh nikajua habar ya leo kumbe toka 2010 basi sawa
 
kipumbwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Messages
2,018
Likes
4,306
Points
280

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2015
2,018 4,306 280
Nilitaka kushangaa,maana ubabe wa CCM ndio umempa chama ikiwemo kumsaidia kuvunja ofisi,kulala ndani ya ofisi,ruzuku na hata kwenda ikulu kuteta na Magu kila akijisikia!!
 
Forum statistics

Threads 1,204,034
Members 457,093
Posts 28,138,891