Lipumba ataka wataalamu wa nje wakague makombora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba ataka wataalamu wa nje wakague makombora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohammed Shossi, Feb 19, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Lipumba ataka wataalamu wa nje wakague makombora Send to a friend Friday, 18 February 2011 21:23 0diggsdigg

  Elizabeth Ernest
  MWENYEKITI wa Chama cha Wanananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameishauri serikali iwalete wataalamu wa nje ya nchi, ili wakague silaha zilizoko katika kambi za jeshi, ili kujiridhisha kuhusu usalama wa silaha hizo na kuepuka matukio ya kulipuka.

  Rai hiyo wa chama hicho cha upinzani, inafuatia kulipuka kwa makombora katika maghala 23 ya kuhifadhia silaha katika kambi ya JWTZ, Gongo la Mboto, usiku wa kuamikia Alhamisi wiki hii.

  Habari za awali zilisema watu 40 wamekufa na wengine 300 kujeruhiwa katika tukio hilo, lilitokea miaka miwili baada ya milipuko iliyotokea Mbagala, Aprili mwaka juzi.

  Profesa Lipumba alitoa rai jana jijini Dar es Salaam, baada ya ziara ya kuwajulia hali majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Amana, katika Manispaa ya Ilala.

  "Waletwe wataalamu ili wafanye uchunguzi wa kina kuhusu silaha zilizobaki, ili hali kama hii isitokee tena. Ni jambo la kusikitisha kwa yaliyotokea,"alisema.

  Alisema ili matukio kama hayo yasiendelea kujirudia, kuna haja ya kuyatambua mapema na kuyaangamiza kitaalamu, mabomu ya muda mrefu na ambayo yamechoka.

  Profesa Lipumba alisema tukio kama hilo liliwahi kutokea mwaka 2004 katika kambi ya JWTZ Gogolamboto na baadaye mwaka 2009 lilijirudia katika kambi ya JWTZ Mbagala.

  Mwenyekiti huyo wa CUF pia alitaka wananchi wapewe elimu kuhusu namna ya kujihami na milipuko ya aina hiyo, ili kupunguza maafa.

  "Katika tukio hili, tumejifunza mengi ikiwa ni pamoja kwamba idadi kubwa ya majeruhi waliofikishwa hapa ni wale ambao wameumia wakati wakikimbia, ili kujihami na mlipuko na si majeraha ya mabomu ya moja kwa moja," alisema.

  Alisema kama wananchi wataelimishwa kwamba wasikimbie au waende katika maeneo ya wazi wakati milipuko inapotokea, hakutakuwa na madhara makubwa.

  Profesa Lipumba pia alisema si vizuri kuweka hifadhi ya silaha karibu na makazi ya watu .
   
 2. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  My take:

  Aliyoyasema Lipumba nakubaliana nayo kwa maana hakuna raia wa kawaida ajuae kujihami na milipuko ya mabomu, na kuna umuhimu Serikali yetu ifanye kila liwezekanalo ili kuweza kufanya ukaguzi wa silaha zilizopo kwenye makambi ya jeshi maana sie wengine tunafanya kazi karibu na kambi za jeshi yaani tunaishi roho zetu zikiwa juu......
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwa vyovyote hakuna atakayeweza kutoa guarantee kwamba maghala ya silaha ni salama katikati ya miji. Maghala yanatakiwa kuhamishiwa maporini - na wawe na ardhi kubwa, mfano hata pande la bomu likiruka km 20 lisikute raia au mali zao. Hili linatakiwa kufanywa mara moja.
   
Loading...