Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
LIPUMBA ASHIRIKIANA NA JAJI FRANCIS MUTUNGI NA CCM ZANZIBAR KUMVUA UKATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD ILI KUNUSURU JAHAZI:
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
THE DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Imetolewa leo Tarehe 05/3/2017
Na. Kurugenzi ya Habari na Uenezi–CUF Taifa
LIPUMBA AITISHA KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA ‘FAKE’ KATIKA MUENDELEZO WA MPANGO WA KUHUJUMU CHAMA ASHIRIKIANA NA JAJI FRANCIS MUTUNGI NA CCM ZANZIBAR KUMVUA UKATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD ILI KUNUSURU JAHAZI:
Kwa mara ya kwanza toka afanye uvamizi wa Ofisi Kuu ya Chama Buguruni tarehe 24/9/2016 hivi sasa ni takribani miezi mitano (siku 155) Lipumba na kundi lake wameendelea kuikalia ofisi hiyo kwa msaada wa vyombo vya Dola kama ambavyo barua ya Jaji Francis Mutungi aliyomuandikia IGP Ilivyoeleza. Tumeeleza mara kadhaa kuwa Lipumba alisimamishwa uanachama na wenzake 11 na baadae kufukuzwa uanachama na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa kilichofanyika tarehe 27/9/2016. Lipumba si mwanachama wa CUF. Tarehe 10/2/2017 katika muendelezo wa mradi wa kukiharibu/kukivuruga Chama (Party Destruction Project-PDP) alifanya ziara ya siri/ kificho kisiwani Unguja na kukutana na wahafidhina viongozi wakuu wa CCM na mmoja wa ADC kupanga njama za kuihujumu CUF kama ilivyoripotiwa na mtoa taarifa Mzalendo Juma Mrisho Pandu-almaarufu Mapweza. Katika mazungumzo hayo walijadiliana na Lipumba kuona ni jinsi gani ya kushirikiana kwa pamoja kumsambaratisha Maalim Seif Sharif Hamad ndani ya CUF ambaye wamedai kuwa ndiye kikwazo kikubwa cha utulivu wa CCM Visiwani-Zanzibar na hilo linatokana na 'wazungu' Taasisi mbalimbali za Jumuiya ya Kimataifa ambazo zilishiriki katika uangalizi, ufuatiliaji na kushuhudilia uchaguzi huru na wa haki wa Oktoba 25, 2015 uliompa ushindi Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Rais wa Zanzibar wamechachamaa Lazima haki irejeshwe kwa mshindi wa uchaguzi huo.
Mara baada ya kikao hicho utekelezaji ulianza wa kutuma barua rasmi kwenda kwa Katibu Mkuu Mtendeni, Zanzibar kwa kuwatumia mawakala wa DHL/EMS ambao hata hivyo hawakuweza kufanikiwa. Jana tarehe 4/3/2017 Magdalena Sakaya mmoja wa waliosimamishwa uanachamà na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na baadae yeye mwenyewe kuyakatia RUFAA kwa Mkutano Mkuu wa Taifa maamuzi hayo, ametuma ujumbe mfupi (SMS) kwa njia ya simu akitoa taarifa ya kuitisha kikao eti alichokiita cha Kamati ya Utendaji ya Taifa-KUT, kitakachofanyika tarehe 6/3/2017 saa 3 asubuhi Ofisi Kuu Buguruni na kwamba eti kikao hicho kitaongozwa/kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Taifa.
Tunapenda kuchukua fursa hii kumjulisha Lipumba na wenzake kuwa kwa Mujibu wa katiba ya CUF Ibara ya 84 (1) ikisomwa pamoja na Ibara ya 93 (1)(d) inaeleza kuwa; “kutakuwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo itakutana mara moja kwa kila miezi miwili. Isipokuwa kwamba ikitokea dharura kamati hiyo inaweza kufanya kikao cha dharura wakati wowote ambao MWENYEKITI WA KAMATI HIYO ATAAMURU HIVYO.”
Kwa mara ya mwisho kikao cha kawaida cha Kamati ya Utendaji ya Taifa kilifanyika tarehe 2/2/2017 katika ofisi ndogo ya Chama Vuga, Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad. Mwenye mamlaka ya KUAMURU kuitishwa kwa Kamati ya Utendaji ya Taifa ni Mwenyekiti wa kamati hiyo pekee na kwa vyovyote vile mamlaka hayo hayakasimiwi kwa kuwa mwenyewe yupo na anatekeleza wajibu wake na maagizo yote ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa. Katika utekelezaji bora wa kifungu cha 84(4) hii maana yake ni kwamba TAMKO la kuitishwa kwa kikao LAZIMA litoke kwa Mwenyekiti na kikao hicho kinaweza kuongozwa na walioelezwa katika kifungu hichi pale “Mwenyekiti=Katibu Mkuu” asipoweza kuhudhuria. Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad hajaitisha kikao chochote mahala palipotajwa na kwamba wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya Taifa mnatakiwa kuendelea na majukumu mliyojipangia/ kupangiwa kwa siku hiyo.
Imebainika kuwa Lengo la kikao hicho kwa mujibu wa taarifa rasmi toka ndani ya Ofisi Kuu Buguruni ni kuwa Moja; kujadili zuio na kunyimwa kupatiwa fedha za ruzuku toka Hazina (serikalini). Pili, Tamaa na uchu wa kukimbizana na kutaka kupata nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki kutoka miongoni mwao. Tatu, kutaka kuziba ombwe la ukosefu wa vikao vya kikatiba lililopo kwa upande wa Lipumba na kundi lake toka afanye uvamizi, Nne; Kusudio na jaribio la kutaka kuivunja Kamati ya Utendaji Taifa ili eti aunde Kamati ya Utendaji ya Taifa mpya itakayomtii na baadae waitishe Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ‘FAKE’ watangaze eti kumsimamisha na au 'kumfukuza Chama' Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na baadae kuelekea kuivamia ofisi ya Makao Makuu, Mtendeni, Unguja-Zanzibar. Tano; ni kutaka kumsaidia Jaji Francis Mutungi kunusurika na kesi ya madai/wizi wa fedha za ruzuku ya CUF shilingi 369 milioni. Tuishie hapa mipango mingine tutaiweka wazi wakati muafaka. Huu ndio mradi wa PDP. Hayo ndio makubaliano ya Lipumba na viongozi wa CCM Zanzibar ili 'kunusuru Jahazi' na kuharibu mchakato wa kupata Mamlaka kamili na Neema kwa wote Zanzibar. Lipumba na wenzake wamekuwa na hoja nyepesi wakidai kuwa sababu za kufanya hivyo eti Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad hafiki Ofisini kwake Buguruni na kwamba eti ndani ya CUF hakuna mgogoro baada ya Msajili kumtambua Lipumba !!! Ukiwauliza kwa nini wao hawafiki Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Mtendeni, Zanzibar? ambako shughuli zote za Chama zinaratibiwa hapo, Hawana majibu yanayojitosheleza. Maalim Seif hatokwenda afisi Kuu Buguruni kwa kutekeleza maagizo ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na kuheshimu taratibu za kisheria zilizochukuliwa na Bodi ya Wadhamini ya CUF kwa kufungua shauri la madai Namba 23/2016 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupata tafsiri ya kisheria juu ya uhalali wa maamuzi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kuingilia shughuli za utendaji wa Chama na maamuzi halali ya vikao vyake. Lakini pia itakumbukwa kuwa Lipumba amekata Rufaa kwa Mkutano Mkuu wa Taifa juu ya maamuzi ya Baraza Kuu la uongozi la Taifa kumsimamisha uanachama tarehe 28/8/2016 kabla ya hapo baadae kufikia maamuzi ya kumfukuza Uanachama.
WITO WETU KWA ‘ALHAJI’ PROFESA LIPUMBA;
Tunamtahadharisha kuwa wanachama na viongozi wa CUF wamechoshwa na HAWATAKUBALI vitendo na mwenendo wa makusudi wa kutaka kukiyumbisha Chama. Lipumba na wenzake waheshimu Katiba ya CUF na maamuzi halali ya vikao vya Chama. Mchezo huu anaojaribu kutaka kuufanya utaamsha hasira za wanachama na kusababisha machafuko na maafa makubwa ndani ya Chama na nchini kwa ujumla. Lipumba atalazimika kubeba dhima ya madhara na maafa hayo. Pamoja na njama hizo tunaendelea kuwahakikisha wapenzi, viongozi na wanachama wa CUF kuwa, viongozi wenu wapo madhubuti kupambana na njama zote ovu dhidi ya Chama na viongozi wake.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Taifa wanaotambulika na Bjaraza Kuu la Uongozi la Taifa ni hawa wafuatao:
1. Maalim Seif Sharif Hamad -Mwenyekiti
2. Joran Lwehabura Bashange -Kaimu Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi
3. Nassor Ahmed Mazrui -Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar Zanzibar
4. Abdallah Khamis - Naibu Mkurugenzi wa fedha na Uchumi
5. Mustafa Wandwi -Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama
6. Yussuf Salim - Naibu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama.
7. Umar Ali Sheikh - Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi
8. Shaweji Mketo - Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi
9. Ismail Jussa Ladhu -Mkurugenzi wa mambo ya nje na Mahusiano ya Kimataifa.
10. Abdallah Mtolea - Naibu Mkurugenzi wa mambo ya nje na mahusiano ya Kimataifa
11. Salim Bimani - Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
12. Mbarala Maharagande - Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
13. Kulthum Mchuchuri -Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu.
14. Pavu Abdallah - Naibu Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu.
CUF NI TAASISI IMARA YENYE VIONGOZI MAKINI
HAKI SAWA KWA WOTE
----------------------------------------------
MBARALA MAHARAGANDE
K/NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA- CUF TAIFA
MAWASILIANO: 0784 001 408/0715 062 577