Lipumba - Anayewagawa Watanzania hatakiwi CUF! (Mbona Jussa yupo?) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba - Anayewagawa Watanzania hatakiwi CUF! (Mbona Jussa yupo?)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Mar 25, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Prof Lipumba katoa kali ya mwaka alipokuwa anawahutubia wananchi wa visiwani Zanzibar na kusema wamwogope mtu anayewagawa watanzania kiunguja, kiupemba na kiutanganyika kuwa ahitajiki CUF na aogopwe kama ukoma cha ajabu Jusa naye yupo na kahutubia.

  Hivi kweli yanatoka miyooni mwao au ndo ngozi ya kondoo?

  Source ITV
   
 2. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  wa kwanza jussa na ubaguzi wa udini na uzanzibari
   
 3. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Ndo ujue viongozi wetu hawa wanaotoa matamko bila ya kuyafanyia utafiti, kwa nini kwenye mikutano kama hii watu hawaruhusiwi kuhoji jamani?
   
 4. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  umemtazama usoni mwake wakati anaogea statement hii?
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..amesema anayetaka kuwagawa wa-ZANZIBARI.

  ..Prof hawezi kwenda Zanzibar na kuthubutu kutamka "anayetaka kuwagawa wa-Tanzania..."

  .."wa-Tanzania" ni sisi wa-Tanganyika, wa-Zanzibari wamebakia na identity yao.
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Another obsession with UMOJA wa zanzibar, wazanzibar wakiwa wamoja kitu unapungukiwa wewe?
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Topical,

  ..obssession yangu ni muungano uvunjike. hilo wala silifichi.

  ..mimi napenda wa-Zanzibar wawe kitu kimoja, zaidi nawaombea wafanikiwe kuuvunja muungano.

  NB:

  ..hivi mbona Lipumba hazungumzii umoja wa wa-Tanganyika??
  ..
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni haki yako kutaka muungano kuvunjika lakini unajua unatakiwa ufanye kazi kama mtanganyika kwanini unataka wazenj ndio wakusaidie kuuvunja? kama siyo ujinga ni nini? peleka mawazo yako chadema huko etc..

  CUF tangu ianzishwe haina mpango wa kuvunja muungano ila kuwa na serikali tatu; na umoja wao ni muhimu kufikia lengo hilo ambalo ccm wanaona ni threat kwao..

  Kuhusu Tanganyika kuna mgawanyiko gani?
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,271
  Trophy Points: 280
  Tanganyika mgawanyiko ni mkubwa sana, mikoa ya pwani watu wake ni maskini sana na hawana elimu ya kutosha, na waislamu wanalalamika wanaonewa na mfumo kristo. huu kama sio mgawanyiko wewe unaupa jina gani?
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Topical,

  ..It is easier kuwaunganisha wa-ZNZ ambao ni mil 1 na kuuvunja muungano, kuliko kuwaunganisha wa-Tanganyika mil 35+ for the same purpose.

  ..Zaidi, wa-ZNZ tayari wanauchukia muungano, wakati wa-Tanganyika hawana hata habari kama upo.

  ..huku Tanganyika kuna mgawanyiko kati ya CDM,CCM,CUF etc etc, kuna tensions za Waislamu vs Wakristo, kuna mambo ya ukabila unaorudi kwa kasi, etc etc.

  ..kwa mtizamo wangu UMOJA wa WATANGANYIKA na jambo linalipaswa kupewa kipaumbele.
   
 11. T

  Topical JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tatizo hilo ni dogo; HAKI SAWA KWA WOTE..sera mama inayotakiwa kutekelezwa na kuenziwa na wananchi wote wapenda amani na walio tayari kutetea wanyonge.

  Besides kama mfumo kristo unalalamikiwa ni kuuondoa na kuweka mfumo wa kitaifa na si wa kikristo..simple
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Anabwabwaja tu........ Kama ana ubavu aanze na Maalim
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  a. kama ni easier go ahead and convice them to withdraw from union; lakini CUF wao wanataka serikali tatu na wanaanda wananhi kubadilisha muundo wa Muungano hawajawahi kuficha hiyo objectives from day one..

  b. Hivi CUF , CDM CCM ni mgawanyiko huo you must be kidding, mbona wazenj wengi wako kwenye vyama hivyo lakini bado ni wazanzibar..

  Tension za waislamu na wakristo Tanganyika zinaletwa na kanisa kwa kutoa michapisho ya kichochezi na ubaguzi kila inapokaribia uchaguzi .issue ni kuwatisha viongozi wa serikali wasithubutu kuondoa upendeleo wanaopewa kutoka kwenye mfuko wa umma through MoU..wamefanikiwa..
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Topical,

  ..kuna masuala ya KITAIFA na masuala ya Vyama. nadhani wakati mwingine wa-Tanganyika tunashindwa kutofautisha masuala hayo.

  ..hizi tensions za Waislamu vs Wakristo zinapaswa kushughulikiwa kwasababu zikiachwa zinaweza kuisambaratisha nchi.

  ..njia moja ya kushughulikia tensions hizo ni kujenga UMOJA miongoni mwetu ambapo kila mmoja wetu atajisikia ana haki na wajibu wa kuilinda na kuitetea jamhuri.
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,271
  Trophy Points: 280
  Haki sawa kwa wote itawezekana vipi kama mtu anashinda kwenye baraza la msikiti kuanzia Alfajili mpaka saa 2 usiku!..... halafu mimi ninayefanya kazi kwa bidii na kupeleka watoto wangu shule sijui ni usawa gani hapo unaouzungumzia wewe.
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndio maana ya HAKI SAWA KWA WOTE
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  wewe unajidai tu hufahamu na kuleta kejeli kwa waislamu..

  Mimi huwezi kuni-provoke kwa hizo maneno niko above that..

  Kwasababu nilianza kusikia hizo ngojera toka nikiwa sekondari..

  Waislam Tanzania wana hoja kama ni mpenda haki na mpenda amani utakaa chini nakufanya analysis, ili kama taifa tusije ingia kwenye matatizo..

  NB. Kejeli zako hazizuii tatizo ila waislam wanazidi kuwa imara na kuwa wanaharakati day by day..iko siku haki sawa kwa wote itapatikana kwa shari au kwa amani..
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,271
  Trophy Points: 280
  Uzuri haya unayaongelea beyond the keyboard, nenda front ukakutane na lile rungu lililoandikwa MAMA MKANYE MWANAO!.......By the way nashukuru kwa kunifumbuwa macho kwamba CUF ni chama cha waislamu ndio maana slogan yenu ni moja HAKI SAWA KWA WOTE.
   
 19. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Kila siku tumezoea kusoma na imekuwa kawaida kwako kutumia misemo kama "sisi", "Waislamu" n.k. Hivi nikuulize, una maana gani haswa na kauli zako kama hizi? Ni nani alikuteua au kukupa mamlaka ya kuzungumza on behalf ya hao "wengine" kupitia kauli zako kama unavyojifanya kwenye michango yako? Ni Mke, familia au labda basha lako?
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Haki sawa kwa wote inawakera sana waliozea kupendelewa!

  Poleni tutafika tu, asiyependa Haki aelimishwe
   
Loading...