Lipumba anatafuta nini? Mbona anaiandama CHADEMA kiasi hiki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba anatafuta nini? Mbona anaiandama CHADEMA kiasi hiki?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ecolizer baba, Apr 3, 2011.

 1. e

  ecolizer baba Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 40
  Wakuu habari za weekend?

  Leo asubuhi nilikuwa nasikiliza dondoo za gazeti la Mwananchi na nikasikitishwa na habari moja.Ni kwamba huyu jamaa wa CUF aliyegombea urais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania mara nne mfululizo bila mafanikio kaibukia tena mkoa wa Lindi na safari hii amewaambia wakaazi wa huko kwenye mkutano wa hadhara kuwa CHADEMA ni chama cha kuogopwa kama ukoma kwa vile kinawagawa watanzania kwa misingi ya dini zao, makabila yao na kanda zao.

  Hakuishia hapo bali alienda mbali zaidi na kuapa kwa mara nyingine kuwa chama pekee kinachopendwa na watanzania wa rika zote wakiwemo mafisadi wa CCM na hata hao CUF, CHADEMA, hakitachukua dola.

  Sasa naomba tuliangalie hili kwa mapana na marefu; huyu Lipumba karogwa au amekubali makusudi kununuliwa kwa bei chee na chama cha mafisadi (CCM)?

  WAKUU NAOMBA KUWASILISHA
   
 2. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Anatekeleza muafaka kwa vitendo .

  Ajue kuwa kuna siku zitawekwa hapa taarifa zake za kikao kilichofanyika Bagamoyo siku ambayo alikuwa na mkutano Tabora mjini na akalazimika kurejea DSM Kwa ndege ya serikali na baada ya hapo alienda Bagamoyo na kukutana na JK na viongozi kadhaa wa dini , na alirejeshwa uwanja wa ndege saa saba na nusu mchana na kusafirishwa kwa ndege ya serikali hadi Tabora.

  Nitamwaga data zake hapa ndipo mtajua kuwa anafanya kazi gani mpaka sasa.

  kwa leo naishia hapo.
   
 3. i

  ibange JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  :angry:Nimesoma mwananchi ya leo Lipumba yupo Lindi anasema Chadema ni chama cha kidini ni kikabila. Hizi pumba zinachukiza sana. Kama kuna chama cha kikanda na kidini ni CUF. Ni chama cha Wapemba na Waislamu wachache. Hata ziara zake anafanya huko maeneo ya waislamu hathubutu kwenda maeneo ya mchanganyiko. Nashindwa kumwelewa Prof anazungumza kama mwendawazimu? Hata kama amepewa pesa, pesa usinunue utu. Chadema ina wabunge hadi Mpanda na Kigoma kwa waislamu, ni dini gani anazungumzia?. Kina wabunge na madiwani kanda ya kaskazini, mashariki, ziwa, nyanda za juu kusini nk. Ni kabila gani analizungumzia? Yeye atuambie CUF ina wabunge wangapi wakristo? Nimemdharau sana huyu mzee wa pumba.:angry::angry::angry::angry::angry:
   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  yeye ndio mwenye kuwagawa watanzania kwani kwa sasa serikali iliyopo madarakani ni ya ccm, na madhara tunayopata kwa sasa yanatokana na utawala wa ccm, kuwasema cdm, kwa sasa jimbo ambalo linaweza kufanywa na mtu mwenye hila mbaya, mbaguzi, fisadi, aliyefirisika kisiasa na kiuchumi, na hata aliye filisika kitabia kwani mtu muadilifu hawezi hata siku moja kukubali kuuza utu wake kwa kipande cha kanga au fedha
   
 5. mka

  mka JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hakuna haja ya kumjadili lipumba ameshaishiwa na mambo ya kufanya so anaongea upupu tu kama jina lake
   
 6. H

  HYDROCHLORIC Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kaka tuletee data kamili............
   
 7. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Anatekeleza ilani ya uchaguzi kwani yeye si ni mtawala ?
   
 8. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 513
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Mkuu heshima mbele kani unaonyesha ni kwa jinsi gani unaelewa kwa upana kile kinachofanywa na Prof Lipumba. Kumbuka this is the forum where we dare to talk openly provided that you have supportive data. Nashauri uzimwage ili ziwafumbue wengi wasiojua makubaliano hayo yaliyofanyika Bagamoyo. Na kama alikuwa anasafirishwa kutoka Tabora hadi Dar then to Tabora nadhani napo kuna kitu cha kuhoji. Kwanza kwanini ghafla hivyo huku wakijua yupo Tabora kwenye ziara lazima kuna kitu walitaka kuficha kwamba ikigundulika wasingizie kuwa alikuwa ziarani Tabora. Lakini pia ninaona kuwa ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Kuna kitu tutahitaji kujua zaidi. Kiranja mwaga data hapa kwenye forum.
   
 9. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni kati ya waajiriwa wa RA na JK, lakini akumbuke mficha maradhi kifo kitamuumbua.
   
 10. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu tunaomba hizo data zitatufaa sana kwa mstakabili wa taifa letu.Ningependa utoe mapema ili aumbuliwe kwani tukiendelea kumwacha wakati tunafahamu fika anachofanya atakuwa amewadanganya wengi wasiojua.So i beg you release the the data
   
 11. mwanapolo

  mwanapolo Senior Member

  #11
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kazi kweli kweli. Mti wenye embe nzuri hupigwa na mawe mengi
   
 12. H

  Hamuyu Senior Member

  #12
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwenye Red mimi ni nimezaliwa kisiwa cha Pemba na ni muislam siko CUF, rekebisha bandiko lako please
   
 13. LWAKAPISI

  LWAKAPISI Member

  #13
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lipumba ni mpumbavu anatema big j kwa karanga za kuonjeshwa!anavokiandama cdm ndo umaarufu waongezeka
   
 14. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Akili za WATANZANIA.... ZINAISHIA PALE MACHO YA NJE YANAPOONA!
  Wengi wetu hatutumii macho yetu ya ndani kuona visivyoonwa....
  KILA SIKU TUTASEMA HAPA MPAKA LINI?

  HAKUNA UPINZANI TANZANIA.... HIVI VYAMA VYENU VYOOOTE VILIVYOPO NI KIINI MACHO, NI VYA MSIMU TU!

  KWA KUWASAIDIA...

  VYOTE VINAELEKEA KABURINI KWA MAANA WOTE WANAANDAMANA....

  HILI LINAANSHIRIA KUFUFUKA KWA NCCR...
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,057
  Trophy Points: 280
  Zimwage kama vipi na iwe vipi
   
 16. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nitaziweka kwani ile documentary haipo hapa nilipo kwa sasa so hadi keshokutwa ili niweke vitu vyenye ushahidi kamili.
   
 17. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,175
  Trophy Points: 280
  Mwaga kungali mapema ili tuidilute sumu yake. Twambie ili tumuanike na unafiki wake.
   
 18. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Kiranja tunasubiri kwa hamu hiyo documentary Mungu akubariki!
   
 19. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  lipumba analaana ya makamba ni zao chafu ndani ya nchi na uprofesa wake hana mana
   
 20. w

  wikolo JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Najaribu kukumbuka wakati ule tunaambiwa chama chake cha CUF ni cha kigaidi na tukaonyeshwa na mapanga yaliyosemwa kwamba ni yao. Haya yote yalifanywa na watawala ambao leo hii yeye prof na akiwa katika nafasi ya uenyekiti wa chama cha CUF anawatetea!!Pamoja na kukipa chama chake majina yote yale bado leo hii kaamua kuwa nao. Hapambani na chama tawala tena isipokuwa anapambana na chama cha upinzani. Ni vigumu sana kulielewa hili na sidhani kama anaitendea haki hata CUF yenyewe anayoiongoza.
   
Loading...