Lipumba amwangukia Maalim Seif arudi CUF

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemuomba aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad kurejea tena na chama hicho ili washirikiane kudai haki.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwakumbuka wanachama wa CUF waliopoteza maisha Januari 26 na 27 mwaka 2001 wakati wa maandamano ya amani, Profesa Lipumba aliwaomba wanachama wote waliohama CUF kurejea katika chama hicho ili kwa pamoja waweze kudai haki.

“Hata Maalim Seif karibu, unaweza kubaki ACT Wazalendo kulinda umakamu wa Rais, lakini tunakukaribisha katika chama cha kudai haki. Wanachama wenzangu kwa sababu moja ama nyingine iwe kwa uongo uliozidishwa, rejeeni katika chama chetu kudai haki,” alisema Lipumba.

Maalim Seif ambaye ni makamu wa kwanza wa rais Zanzibar na mwenyekiti wa ACT-Wazalendo aliondoka CUF Machi 2019 baada ya a mgogoro wa uongozi kutokana na Profesa Lipumba ambaye alijiuzulu mwaka 2015 kurejea kwenye uongozi Julai 2016.

Mvutano huo wa uongozi ulihamia mahakamani lakini baada ya Lipumba kushinda kesi, Maalim Seif na kundi kubwa la wanachama wa CUF walihamia ACT-Wazalendo ambako makamu huyo wa kwanza wa rais alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Baadhi ya viongozi waliotimka CUF na kumfuata Maalim Seif ni Joram Bashange, Nassoro Ahmed Marzui na Juma Haji Duni.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo ikiwa imepita miaka miwili ya malumbano baina yake na Maalim Seif.

Machi 2019, akizungumza katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya CUF Buguruni, msomi huyo alimtaka Maalim Seif asiwaharibie chama chao.

Alisema Maalim anawafarakanisha watu waliokuwa pamoja, akidai ni mbinafsi na mtu hatari kwa kuwa aliwashawishi waliokuwa wabunge wa CUF kukihama chama hicho.

Machi 18, 2019 Lipumba alizungumza na Mwananchi na kueleza kuwa uamuzi wa kumfukuza Maalim Seif na wafuasi wake CUF ulikuwa ni wa kusikitisha lakini haukuwa na budi kwa sababu kiongozi huyo aliwasababishia matatizo.

Uamuzi wa Seif na timu yake ulikiathiri pakwa chama hicho, hasa Zanzibar ambako mbali na kupoteza maelfu ya wanachama, pia ofisi za chama hicho zilibadilishwa na kuwa za ACT Wazalendo.

Jana, msomi huyo hakurejea kauli hizo badala yake alisema huu ni wakati wa kujenga chama imara na kujenga mtandao mzuri wa chama kwa sababu chama imara ndicho kitakachosikilizwa kwamba madai yake ni ya msingi.

“Tutaendelea kutoa hoja za kudai haki kwa kutumia mbinu za amani tukiwa humuhumu Tanzania hatuna utaratibu wa kukimbia nchi, tutapambana kudai haki kwa amani tukiwa humuhumu,” alisema.

Kuhusu wanachama waliopoteza maisha mwaka 2001, Profesa Lipumba aliwataka wanachama kusamehe yote yaliyotokea lakini wasisahau.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Magdalena Sakaya alisema chama hicho kitaanzisha vuguvugu ya kudai Katiba Mpya nchi nzima ili kupata Tume huru itakayosimamia haki za wapigakura.

“Hilo si jukumu letu CUF pekee yetu, tunaomba wananchi wote, taasisi mbalimbali tudai Katiba Mpya ili nchi yetu iwe na Tume huru ya uchaguzi itakayosaidia kuondoa malalamiko baada ya uchaguzi,” alisema.
 
Bora angebaki kufundisha USA,elimi kubwa lakini anayumbishwa na vilaza wa ccm
Imefika wakati sasa hata watu mtaani wanamuona ni kituko kabisa
 
Moja ya mifano Bora ya ukatili wa Ccm kwa wapinzani na siasa za uchumia tumbo hapa ulimwenguni ni CUF ya Lipumba na mfano Bora wa mwanasiasa mwenye Elimu ya makaratasi anayeteswa na njaa Kali ni Lipumba. Wanachama wa Lipumba wanategemea ujinga wao kichwani kubaki chamani
 
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemuomba aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad kurejea tena na chama hicho ili washirikiane kudai haki.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwakumbuka wanachama wa CUF waliopoteza maisha Januari 26 na 27 mwaka 2001 wakati wa maandamano ya amani, Profesa Lipumba aliwaomba wanachama wote waliohama CUF kurejea katika chama hicho ili kwa pamoja waweze kudai haki.

“Hata Maalim Seif karibu, unaweza kubaki ACT Wazalendo kulinda umakamu wa Rais, lakini tunakukaribisha katika chama cha kudai haki. Wanachama wenzangu kwa sababu moja ama nyingine iwe kwa uongo uliozidishwa, rejeeni katika chama chetu kudai haki,” alisema Lipumba.

Maalim Seif ambaye ni makamu wa kwanza wa rais Zanzibar na mwenyekiti wa ACT-Wazalendo aliondoka CUF Machi 2019 baada ya a mgogoro wa uongozi kutokana na Profesa Lipumba ambaye alijiuzulu mwaka 2015 kurejea kwenye uongozi Julai 2016.

Mvutano huo wa uongozi ulihamia mahakamani lakini baada ya Lipumba kushinda kesi, Maalim Seif na kundi kubwa la wanachama wa CUF walihamia ACT-Wazalendo ambako makamu huyo wa kwanza wa rais alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Baadhi ya viongozi waliotimka CUF na kumfuata Maalim Seif ni Joram Bashange, Nassoro Ahmed Marzui na Juma Haji Duni.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo ikiwa imepita miaka miwili ya malumbano baina yake na Maalim Seif.

Machi 2019, akizungumza katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya CUF Buguruni, msomi huyo alimtaka Maalim Seif asiwaharibie chama chao.

Alisema Maalim anawafarakanisha watu waliokuwa pamoja, akidai ni mbinafsi na mtu hatari kwa kuwa aliwashawishi waliokuwa wabunge wa CUF kukihama chama hicho.

Machi 18, 2019 Lipumba alizungumza na Mwananchi na kueleza kuwa uamuzi wa kumfukuza Maalim Seif na wafuasi wake CUF ulikuwa ni wa kusikitisha lakini haukuwa na budi kwa sababu kiongozi huyo aliwasababishia matatizo.

Uamuzi wa Seif na timu yake ulikiathiri pakwa chama hicho, hasa Zanzibar ambako mbali na kupoteza maelfu ya wanachama, pia ofisi za chama hicho zilibadilishwa na kuwa za ACT Wazalendo.

Jana, msomi huyo hakurejea kauli hizo badala yake alisema huu ni wakati wa kujenga chama imara na kujenga mtandao mzuri wa chama kwa sababu chama imara ndicho kitakachosikilizwa kwamba madai yake ni ya msingi.

“Tutaendelea kutoa hoja za kudai haki kwa kutumia mbinu za amani tukiwa humuhumu Tanzania hatuna utaratibu wa kukimbia nchi, tutapambana kudai haki kwa amani tukiwa humuhumu,” alisema.

Kuhusu wanachama waliopoteza maisha mwaka 2001, Profesa Lipumba aliwataka wanachama kusamehe yote yaliyotokea lakini wasisahau.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Magdalena Sakaya alisema chama hicho kitaanzisha vuguvugu ya kudai Katiba Mpya nchi nzima ili kupata Tume huru itakayosimamia haki za wapigakura.

“Hilo si jukumu letu CUF pekee yetu, tunaomba wananchi wote, taasisi mbalimbali tudai Katiba Mpya ili nchi yetu iwe na Tume huru ya uchaguzi itakayosaidia kuondoa malalamiko baada ya uchaguzi,” alisema.
Kwa kawaida tamaa na unafiki unamalipo yake,Alishaaamua hicho kiwe chako japo Nate ameona isiwe tabu na uzee wake.
 
Lipumba kwa sasa ni sawa na ganda la muwa tu.

Aliamua kujishushia hadhi yake mwenyewe kwa kukubali kutumiwa na wapinga mageuzi.

Amwache Maalim ajilie kuku wake na ACT yake.
Mimi hao na wengine wote wa aina yake,ndio waliotufikisha hapa kama taifa, nitamlaumu hata kesho kwa kilealicho kifanya kama msomi mbobezi
 
Lipumba finished., kule kwetu kuna ule mchezo wanasema “ametolewa kapa” sasa amekuwa mfia chama, CCM is not a good frend, leo ccm wenyewe waliokuwa na hadhi na wanywa maji ya bendera na wana mapinduzi kule Bara na Zanzibar sasa hawana thamani tena, wamebaki kutazama tu itakuwa yeye?? Kwisha kabisa Lipumba kifo cha Mende, ndembe ndembe
 
Back
Top Bottom