Lipumba amtaka Kikwete amfukuze Ngeleja uwaziri

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,153
30,872


lipumba nec.jpg
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya Mahakama Kuu kusajili tuzo ya malipo ya Sh111 bilioni kwa kampuni ya Dowans, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amemshauri Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na watendaji wake kwa kuisababishia nchi hasara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema kwamba Ngeleja na watendaji walioko chini yake ndio waliosababisha hasara hiyo ambayo sasa Serikali inapaswa kulipa hivyo ni lazima wawajibishwe mara moja.

“Wakati huu ambao Serikali imeshindwa kutatua tatizo la umeme, tunaongezewa gharama za kesi. Hili ni ombwe la uongozi ndani ya Serikali ya CCM, tangu Rais, mawaziri na watendaji wake. Nashangaa bado viongozi waliosababisha yote haya wako madarakani,” alisema Profesa Lipumba.Juzi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilibariki malipo kwa Dowans baada ya kusajili tuzo iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), dhidi ya Tanesco na kampuni hiyo ya kufua umeme.Kwa uamuzi huo, Tanesco sasa inatakiwa iilipe Dowans kiasi cha Sh 111 bilioni badala ya Sh 94 bilioni za awali kwani inatakiwa kuilipa fidia hiyo na riba ya asilimia 7.5.

Profesa Lipumba alisema tukio hilo ni matokeo ya ufisadi ndani ya Serikali kwa sababu Dowans ilitokana na mkataba wa Richmond ambao tangu mwanzo, Tanesco waliupinga, lakini baadhi ya viongozi wa Serikali wakashinikiza.
.. Aishukia kampuni ya Rex Attorney
Vilevile, Profesa Lipumba aliilaumu kampuni ya uwakili ya Rex Attorney ya jijini Dar es Salaam kwa kile alichoeleza kuwa ilicheza mchezo wa kimaslahi pale ilipoishauri Tanesco kuvunja mkataba na Dowans kwa madai kuwa haukuwa halali huku ikiisaidia kampuni hiyo kupata mkopo katika benki ya Stanbic.

“Tanesco waliitumia Rex Attorney kupata ushauri wa kuvunja mkataba wa Dowans na Tanesco, lakini Rex hao wakaandika tena barua kwa Benki ya Stanbic ikitaka Dowans ikopeshwe Dola 20 Milioni za Marekani. Hawa ndiyo waliosababisha tushindwe kesi,” alisema Profesa Lipumba.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema hatma ya Tanzania sasa iko mikononi mwa wananchi hivyo, wanapaswa kutambua kuwa nchi inanyonywa na watu wachache.

“Haya ni matokeo ya ubinafsi wa viongozi, wanafanya mambo kwa manufaa yao wenyewe na wala sio kwa faida ya taifa,” alisema Makulilo.Alisema kama wananchi wataamua kusimamia rasilimali za taifa, viongozi wataongoza kwa umakini katika kusaini mikataba ya kibiashara.Profesa Peter Maina alisema hakuna haja ya Dowans kulipwa fedha hiyo kwani tangu mwanzo, mkataba wa Tanesco na Richmond, ulikuwa wa mashaka.

Alisema uzoefu umeonyesha kuwa kumekuwapo na mikataba mingi mibovu nchini hivyo, kukubali kuilipa Dowans, ni kuingia gharama zisizokuwa za lazima.
Mvungi ataka Dowans wasilipwe

Naye kiongozi wa wanaharakati walioishitaki Dowans isilipwe na kushindwa kesi, Dk Sengondo Mvungi, alisema kitendo cha Mahakama Kuu kukubali kusajili tuzo iliyotolewa na ICC ni kukubali kulipa deni, jambo ambalo mtandao huo ulipinga.Alisema malipo hayo ni ufisadi wa waziwazi na yakitekelezwa, maana yake Serikali imehalalisha dhuluma dhidi ya wananchi wake.

“Kitendo cha Mahakama Kuu kukubali kusajili tuzo hiyo kimetuangusha sana, kwa sababu walijua wazi kuwa mwisho wa kesi hiyo ni kuilipa Dowans. Huu ni ufisadi na ni sawa na kuhalalisha rushwa ndani ya Serikali. Tunawaomba wananchi wapinge kwa nguvu zote malipo hayo,” alisema Dk Mvungi.

Kwa mujibu wa Dk Mvungi, mkataba tata ulioingiwa kati ya Richmond na Tanesco, bado unaendelea kulitafuna taifa kwani ndio uliorithiwa na Dowans na sasa kampuni ya Symbion.“Symbion ni mrithi wa Richmond na Dowans, hivyo mwisho wake ni mahakamani tena. Wananchi wanapaswa kuwa makini na wakemee dhuluma hiyo,”aliongeza.

Novemba 15, 2010, ICC iliiamuru Tanesco iilipe Dowans fidia ya Sh 94 bilioni kwa kuvunja mkataba baina yake na kampuni hiyo kinyume cha sheria. Kufuatia uamuzi huo wa ICC, Januari 25, 2011 Dowans iliwasilisha maombi mahakamani hapo ikiomba tuzo yake hiyo isajiliwe ili utaratibu wa ulipwaji wake uwe na nguvu ya kisheria .

Katika kesi hiyo, Tanesco kupitia kwa mawakili wake, Rex Attorneys kwa kushirikiana na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Februari 9, 2011, waliwasilisha mahakamani hapo pingamizi la usajili wa tuzo hiyo.Tanesco waliwasilisha hoja 11 za kupinga tuzo hiyo ya ICC wakieleza kuwa mahakama hiyo ya kimataifa ilijipotoka kisheria katika kutoa tuzo hiyo kwa Dowans na hivyo kuiomba Mahakama hiyo iitupilie mbali tuzo hiyo. Hata hivyo, hoja zao zilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu kusajili tuzo ya Dowans.

Habari hii imeandaliwa Elias Msuya, Patricia Kimelemeta, Ellen Manyangu na Elizabeth Edward
chanzo: Gazeti la Mwananchi

whttp://mwananchi.sekenke.com/aambie Ukweli tunataka viongozi kama nyie Msiogopa kitu katika nchi yetu masikini.........
 

Derimto

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
1,307
303
Dowans lazima walipwe ili Igunga paeleweke maana chama kitagawanyika hakuna njia mbadala na kumfukuza ngeleja ni mtu mdogo sana amewekwa tu pale kama kibao cha kupitisha madili ya wakubwa (wanamtandao)
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,153
30,872
Dowans lazima walipwe ili Igunga paeleweke maana chama kitagawanyika hakuna njia mbadala na kumfukuza ngeleja ni mtu mdogo sana amewekwa tu pale kama kibao cha kupitisha madili ya wakubwa (wanamtandao)
Kama ni mimi Rais wa Nchi hii ya Tanzania ningemuambia Waziri Ngeleja ajiuzulu mara moja ni aibu kubwa kwa nchi yetu hii kumlipa Dowans mapesa yote hayo?????????? Hizo pesa sizingesaidia matatizo ya umeme iweje Mahakama iamuru serikali ya Mheshimiwa J.kikwete imlipe Dowans Hizo pesa Ahhhhhhhh tunakokwenda huko pabaya sana je tutafika kweli........?
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,153
30,872
haya Tena muanglie tena huyo Wazriri ngeleja anavyosema hapa chini

Serikali yapata mwarobani tatizo la umeme


Thursday, 29 September 2011 21:01
haya ngeleja.jpg
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu ujenzi wa miundombinu ya gesi asili ya kuzalishia umeme.Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakimu Mwasi. Picha na Zacharia Osanga​


Fidelis Butahe
SERIKALI imedhamiria kumaliza tatizo la umeme nchini na tayari imepata mkopo wa Dola 1 bilioni za Marekani kwa ajili ya kujenga bomba kubwa la kusafirishia gesi asili kutoka Mnazi Bay mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam.

Gesi hiyo itatumika kuzalisha megawati 3,900 za umeme. Bomba hilo litasaidia kusafisha na kusafirisha gesi kwa ajili ya mitambo ya gesi ya kufua umeme inayomilikiwa kwa ushirikiano wa serikali, taasisi za umma na sekta binafsi, lengo likiwa ni kuliwezesha taifa kuondokana na utegemezi katika umeme unaotokana na maji. Imesema mradi huo ukikamilika, pia utashusha gharama za umeme kwa asilimia 30.Hivi sasa uniti moja ya umeme inauzwa kwa bei ya Sh160 na mahitaji ya juu ya nishati hiyo nchi nzima hayazidi megawati 1,000. Kwa mujibu wa mkataba, utekelezaji wa mradi huo unapaswa kuanza wiki ya pili ya mwezi ujao na kukamilika kabla ya Machi mwaka 2013. Hata hivyo kutokana na ukubwa wa tatizo la umeme, serikali imeomba na kukubaliwa kuwa ukamilike Desemba mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema mkataba huo ni wa kujenga na kupanua bomba la gesi kutoka Mnazi Bay kupitia Songosongo Kisiwani (Kilwa) hadi Dar es Salaam.

Alisema uamuzi wa kutolewa kwa mkopo huo kupitia Benki za China, umetokana na Serikali za Tanzania na China kutiliana saini mikataba ya uhandisi, manunuzi na ujenzi, uliofanyika Septemba 26 mwaka huu. Alisema mkataba wa mkopo huo wa masharti nafuu na ambao serikali itachangia asilimia 10,utalipwa kwa kipindi cha miaka 20 kwa riba ya asilimia mbili.

Waziri Ngeleja alisema” mkataba huo una vipengele viwili, cha kwanza ni ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mnazi Bay na Songosongo hadi Dar es Salaam lenye urefu wa kilomita 532 na cha pili ni ujenzi wa mitambo miwili ya kusafisha gesi huko SongoSongo kisiwani na Mnazi Bay,” alisema Ngeleja. Alisema Shirika la Petroli Tanzania (TPDC) na CPTDC ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Petroli la China (CNPC), zimekubaliana katika vipengele vyote viwili.

Kwa mujibu wa Ngeleja, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alifanya ziara China ambako Benki ya Exim ya nchi hiyo, ilikubali kutoa mkopo huo”.

Alifafanua kuwa mpaka sasa TPDC imeshakabidhiwa Sh6.5 bilioni na serikali kwa ajili ya kulipa fidia wananchi watakaoathirika na mradi huo na kufanya utafiti wa maeneo ya kupitisha mabomba hayo. Utekelezaji wa mradi Alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo utakuwa katika awamu mbili.

Utaanza na ujenzi wa bomba la gesi utakaohusisha bomba la inchi 24, lenye urefu wa kilomita 25 kutoka Songo Songo Kisiwani hadi Somanga Fungu. “Pia utaambatana na ujenzi wa bomba lenye kipenyo cha inchi 36 lenye urefu wa kilomita 207 kutoka Somanga Fungu hadi Dar es Salaam,”
Alisema kuwa awamu ya pili itahusisha ujenzi wa bomba lenye kipenyo cha inchi 36 lenye urefu wa kilomita 285, kutoka Mnazi Bay hadi Somanga Fungu. Alisema bomba la sasa la kusafirisha gesi ni la inchi 16 na kwamba lilianza kutumia mwaka 2004. Alisema kitendo cha kuwa na bomba la inchi 36 kitawezesha upatikanaji wa gesi kiasi cha futi za ujazo 784 milioni kwa siku ikilinganishwa na futi za ujazo 105 milioni zinazozalishwa sasa.

“Hizi zitatumika kwa uzalishaji wa umeme ambao utafikia megawati 3,900, hivi sasa mahitaji mapya ya umeme utokanao na gesi asili pekee ifikapo 2015 yanakadiriwa kuwa megawati 1583,” alisema Ngeleja. Alisema bomba linalotumika sasa ambalo linamilikiwa na Songas limezidiwa na kwamba serikali imelazimika kuongeza bomba jingine kutokana na mahitaji ya gesi asili kwa ajili ya uzalishaji umeme. Alisema kuwa miundombinu ya mradi huo itakuwa chini ya TPDC kwa asilimia miamoja.

“Faida ya mradi huu ni upatikanaji wa umeme kwa gharama nafuu kwa kuwa ni gharama kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta ya dizeli, pia gesi hii itakayoletwa Dar es Salaam itafikishwa Bagamoyo kwa ajili ya kuhudumia viwanda chini ya mpango wa EPZ,” alisema Ngeleja.

chanzo: http://mwananchi.sekenke.com/

P
amoja na Serikali kula hasara bado Mheshimiwa Waziri Ngeleja ameomba mkopo mkopo wa Dola 1 bilioni za Marekani kwa Wafadhili ili azalishe umeme kasheshe kweli Serikali Yetu......
 

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
3,839
628
hata siku moja ngeleja hawezi fukuzwa!
angalia ngeleja alikotolewa na rostam ili wamback up Jk
kwa hiyo ni ngumu sana hawa watatu ni ni kama piston kwenye gari!
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,153
30,872
Mahakama yaridhia Dowans kusajiliwa

Sasa zigo la Sh. bilioni 94 halikwepeki
Dowans(10).jpg

Mitambo ya kampuni za kufua umeme wa dharura ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Limited


Hatimaye Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imesajili tuzo ya kampuni za kufua umeme wa dharura ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Limited, ambapo sasa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) linatakiwa kuilipa kampuni hiyo fidia ya Sh. bilioni 94 kwa kuvunja mkataba wake, kinyume cha sheria.

Malipo ya fidia hiyo yaliamriwa kutekelezwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), baada ya Tanesco kutiwa hatiani kwa kosa hilo.

Uamuzi huo ulifikiwa na Mahakama Kuu, baada ya kutupilia mbali mapingamizi ya Tanesco, yaliyotaka tuzo hiyo isisajiliwe na mahakama. Tuzo hiyo imesajiliwa kutokana na Mahakama Kuu, kutokuwa na mamlaka ya kutengua hukumu iliyotolewa na ICC kupitia makubaliano ya pande zote mbili yaliyofanywa kati ya serikali na Dowans.

Uamuzi huo ulisomwa jana na Jaji wa Mahakama Kuu, Emilian Mushi, baada ya kupitia mapingamizi na majibu ya pande zote mbili kuhusu kutokusajiliwa kwa tuzo hiyo.

Kufuatia uamuzi huo wa ICC, wanaharakati mbalimbali na Tanesco, walifungua mapingamizi mahakamani hapo kuzuia tuzo hiyo kusajiliwa.
Mapingamizi hayo yalisikilizwa na Jaji Mushi.

Septemba 6, mwaka huu, mahakama hiyo ilitupilia mbali mapingamizi ya awali yaliyowasilishwa na Kituo cha Sheria na Hakimu za Binadamu (LHRC) na mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Timoth Kahoho.

Pia Jaji Mushi alikubaliana na hoja za pingamizi za Dowans na Tanesco kuwa maslahi ya umma yanalindwa na kutetewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Baada ya uamuzi huo kutolewa jana, Wakili wa Tanesco, Dk. Eve Sinare, alisema atalishauri shirika hilo kukata rufaa kwa faida ya kesi nyingine zinazoendelea kwa manufaa ya serikali.

“Mimi nitalishauri shirika kukata rufaa kwa manufaa ya kesi nyingine huko mbele serikali iweze kufanya vizuri,” alisema Dk. Sinare.
Amri kwa Tanesco ya kuilipa Dowans fidia hiyo, ilitolewa na ICC Novemba 15, mwaka jana.
Desemba 27, serikali kupitia AG, Jaji Frederick Werema, ilitamka kuridhia kulipa fidia hiyo.

Jaji Werema alinukuliwa akisema kwamba, baada ya kuisoma hukumu hiyo, ameridhika kuwa iko sawa na kwamba, serikali haina nia ya kukata rufaa.

Baada ya Jaji Werema kusema hayo, Januari 6, mwaka huu, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alitoa tamko la serikali kuhusu malipo ya fidia hiyo kwa Dowans na kusema imekubaliana na ushauri wa AG.
Hata hivyo, Januari 11, mwaka huu, mashirika 17 ya wanaharakati yakiongozwa na LHRC, yaliwasilisha Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara, taarifa ya kusudio la kupinga usajili wa tuzo hiyo.

Januari 17, ICC iliwasilisha tuzo hiyo Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam badala ya Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara.
Januari 19, LHRC iliwasilisha barua nyingine Mahakama Kuu ikielezea nia ya kupinga usajili wa tuzo hiyo mahakamani hapo. Januari 25, Dowans kupitia kwa Wakili wake, Kennedy Fungamtama, iliwasilisha mahakamani hapo maombi ya usajili wa tuzo yake hiyo ili utaratibu wa ulipwaji wa fidia uwe na nguvu ya kisheria.

Hatua hiyo ilifuatiwa na Dowans kuwasilisha mahakamani maombi hayo ya usajili na Januari 31, LHRC kwa pamoja na Chama cha Wanasheria wa Mazingira (LEAT) na Kampuni ya Sikika waliwasilisha rasmi mahakamani hapo pingamizi dhidi ya usajili wa tuzo hiyo.
Mbali na wanaharakati hao waliowakilishwa na Wakili Dk. Sengondo Mvungi, Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Kahoho naye aliwasilisha pingamizi la usajili wa tuzo hiyo.

Pamoja na sababu nyingine, wote walidai kuwa wamechukua hatua hiyo ili kulinda maslahi ya umma.
Tanesco nayo kwa upande wake, kupitia kwa mawakili wake, Rex Attorneys kwa kushirikiana na Ofisi ya AG, Februari 9, waliwasilisha mahakamani hapo pingamizi la usajili wa tuzo hiyo.
CHANZO: NIPASHE

 
0 Reactions
Reply
Top Bottom