Lipumba amlilia Mkurugenzi TBC -- Ni CUF Bara Tuu? Visiwani Hawana Malalamiko

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutengua uamuzi wa kumuondoa aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC Tido Mhando na kurudishwa kazini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara uliofanyika Temeke Dar es Salaam, Lipumba alisema hata kama mkataba wake uliisha lakini kulikuwa na jambo la busara la kumrudisha Tido kazini kwa mkataba mpya.
Alisema kama TBC ni ya serikali na si ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hakukuwa na sababu ya kuitwa chombo cha serikali kingeitwa chombo cha CCM, ili katika uchaguzi kifanye kazi za chama hicho tu.
Alisema serikali inakosea kwa kusema kuwa Tido alikuwa anapendelea wapinzani, ila kama ni chombo cha serikali hakuna jambo muhimu kama chombo hicho kikawa kinafanya kazi za wananchi wote bila kujali chama, wala rangi ya mtu. “Tido alifanya kazi kwa niaba ya wananchi na chombo cha serikali ni lazima kiwe kinafanya kazi kwa niaba ya watu wake. Hata hivyo mkurugenzi huyo amejenga heshima kwa taaluma ya habari kwa kuwa alifanya kazi bila ya upendeleo wa chama chochote,” alisema Profesa Lipumba.
 
Aliipendelea CUF ikapunguza kura za waislam kwa CCM. Pole Lipumba. Atangulie tu hakuwa na faida kwa CDM
 
Back
Top Bottom