Lipumba amhusisha JK na Richmond

Hili sakata lilianzia mbali ...........tuendelee...........

Hakuna ubishi kuwa aliyetembelea Houston na kuwa mgeni wa Mohamed Gire wakati wa mchakato wa Richmond alikuwa ni Jakaya Mrisho Kikwete. Huo ugeni wa nguvu uliwezekana baada ya maandalizi yaliyomhusisha balozi wetu Marekani wa wakati huo, Andrew Daraja. Kinachoshangaza ni kamati ya kuchunguza Richmond iliyoongozwa na Mh. Mwakyembe kushindwa kuianika hili !!!! Kaazi kwelix2.

Hoja kuhusu Profesa siyo kwamba JK hahusiki na Richmond -- anahusika sana, anafanya ujanja ujanja tu eti kujiweka mbali na akina EL na RA. Hoja kuhusu Profesa ni kulieleza hilo kwa wananchi wakati huu -- wakati watu wanaanza kulisahau sakata la Richmond.

Kuna hisia kama vile amepata msukumo kuyatamka haya wakati huu.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Mag3,

Soma vizuri ile article; Kikwete hakuwahi kutembelea Houston wakati ule ... Daraja ndiye aliyekwenda Houston! Just kuweka mambo kwenye perspective; na sina maana kwamba Kikwete anahusika au hausiki.
 
Lipumba anayo sema ni kweli, lakini naye siku hizi inabidi tumuangalie kwa makini, kwani amezua katabia ka kuwapigia pande mafisadi, sasa na hii ya kumtaja JK wakati huu inabidi kuiangalia kwa makini, usikute ni katika harakati zile zile za kuwapa shavu kina RA et al.

hasa ukizingati mambo ya Kagoda na Richmond ni moshi unao fuka! afu angalia muunganiko na maelezo ya DPP kwamba walitumwa hawezi washitaki!
 
Mkwere anakazi kubwa, iweje Mengi alipowataja Mafisadi Prof Lipumba aqlimponda sana Mengi, lakini RA alipomponda Mengi Prof akakaa kimya kama Sofia Simba na Mkuchika, lakini leo tunashangaa anamwingilia mkuba wa nchi na kutuambia kwamba ndio masterminder wa mchakato mzima wa Richmond, huyu bwana inaonekana kaisha kabisa kisiasa na elimu yake haimsaidii kabisa, anashinikizwa na Sharif Amad kufanya mambo ya upuuzi kabisa, natumaini tutapata mengi kutoka kwa Lwakatare na pia Prof Safari
 
Hoja kuhusu Profesa siyo kwamba JK hahusiki na Richmond -- anahusika sana, anafanya ujanja ujanja tu eti kujiweka mbali na akina EL na RA. Hoja kuhusu Profesa ni kulieleza hilo kwa wananchi wakati huu -- wakati watu wanaanza kulisahau sakata la Richmond.

Kuna hisia kama vile amepata msukumo kuyatamka haya wakati huu.
....Very interesting.....Ufisadi ukisemwa/Ukitajwa na Viongozi wa Chadema basi OK, wakitaja wengine..wamesukumwa...?..is it?

Hofsted kaweka vema anaeumia ni kila Mtanzania.....!!! Chadema washaona Vita dhidi ya Ufisadi ni ya kwao...!!! ...
"Kwa Mtanzania wa kawaida anaathirika zaid na Richmond kuliko EPA..."..Richmond inatutafuna kila siku inavyokwenda Mbele....!!! Wakati Pesa ya EPA ilikuwa imekaa tu...!!! Msije mkaelewa vibaya kuwa nawafagilia EPA guys....UFISADI ni UFISADI....hauna sura...na Kila Mmoja yapasa aupige Vita UFISADI...!!!

Kwa watu wenye Kuelewa Prof.Lipumba anazungumzia tatizo ni CCM yote na si kuchagua nani hayupo na nani yupo...!!!..Wewe unavyofikiri akimgusa Mkuu wa Nyumba Nyeupe basi EL au RA hawamo?....au mwataka ku-twist habari km mwandishi wa Tz Daima?
 
Mkwere anakazi kubwa, iweje Mengi alipowataja Mafisadi Prof Lipumba aqlimponda sana Mengi, lakini RA alipomponda Mengi Prof akakaa kimya kama Sofia Simba na Mkuchika, lakini leo tunashangaa anamwingilia mkuba wa nchi na kutuambia kwamba ndio masterminder wa mchakato mzima wa Richmond, huyu bwana inaonekana kaisha kabisa kisiasa na elimu yake haimsaidii kabisa, anashinikizwa na Sharif Amad kufanya mambo ya upuuzi kabisa, natumaini tutapata mengi kutoka kwa Lwakatare na pia Prof Safari
Mkuu, Lipumba hakukaa kimya, alisema Mengi amekosea kumtaja RA akiwa hana ushahidi, akaongezea kama ana madai yoyote angeyafikisha kwenye vyombo vinavyohusika..akitetea Dowans alisema swala hapa ni Dowans sio RA..
Sasa, sielewi anachofanya yeye kuna tofauti gani na Mengi.
 
....Very interesting.....Ufisadi ukisemwa/Ukitajwa na Viongozi wa Chadema basi OK, wakitaja wengine..wamesukumwa...?..is it?

Hofsted kaweka vema anaeumia ni kila Mtanzania.....!!! Chadema washaona Vita dhidi ya Ufisadi ni ya kwao...!!! ...
"Kwa Mtanzania wa kawaida anaathirika zaid na Richmond kuliko EPA..."..Richmond inatutafuna kila siku inavyokwenda Mbele....!!! Wakati Pesa ya EPA ilikuwa imekaa tu...!!! Msije mkaelewa vibaya kuwa nawafagilia EPA guys....UFISADI ni UFISADI....hauna sura...na Kila Mmoja yapasa aupige Vita UFISADI...!!!

Kwa watu wenye Kuelewa Prof.Lipumba anazungumzia tatizo ni CCM yote na si kuchagua nani hayupo na nani yupo...!!!..Wewe unavyofikiri akimgusa Mkuu wa Nyumba Nyeupe basi EL au RA hawamo?....au mwataka ku-twist habari km mwandishi wa Tz Daima?
Ni Kwao na ndio wao ndio wameanzisha na kuwamashisha watu kuona na kutambua wewe hujui, Wao walikuwa wapi muda wote?? Mbona yalikuwa yanafanyika wao walikuwa kimnya sana sana why man walikuwa kimnya sana
 
"Mhhh! Pana kitu hapo Zak. Kwanza Profesa ataliitaje sakata la Richmond kuwa ni la kifisadi wakati hivi karibuni alikuwa anaipigia debe mitambo chakavu ya kampuni hiyo (iliyorithiwa na Dowans) inunuliwe na serikali?

Wakati ule Profesa alionekana ametumwa na RA, na haya matamshi yake ya sasa pia yana harufu ya mkono wa RA. Inaonekana uswahiba baina ya JK na RA/EL unaota mbawa polepole!"
________________________

Hard Hitter:

Kidogo umegusa kitu hapo Mkuu. Uswahiba unaanza kuota mbawa. Hivi karibuni Mwanahalisi liliandika kuwa JK alimkacha RA kule Jo’burg wakatiJK alipokwenda kwenye sherehe za kuapishwa Zuma. Baada ya siku chache gazeti hili hili la Tanzania Daima lilikuwa na stori ya kuijanja janja ya iliyomnukuu RA akijaribu kupinga stori ya Mwanahalisi kwamba alikachwa, ingawa RA alikiri kuwapo kule Bondeni wakati mmoja na JK. Alisema hakukachwa kwani huwa wanakutana na JK hapa hapa Bongo.

Lakini kuna habari kuwa suala la Kagoda ndilo linamtesa JK (na RA pia) na inasemekana wafadhili wanambana JK kwa hilo – alitakiwa awafikishe wahusika mahakamani kabla ya kuanza Bajeti ili waweze kufungua pochi zao. Hajafanya hivyo, siku zinakwenda na ahadi za wafadhili zinabakia kuwa ahadi tu.

Hali kadhalika matamshi ya Hosea mwezi Mei kwamba kuna kesi “kabambe za kutetemesha nchi” zingefikishwa mahakamani Mapema Juni kabla ya Beajeti lililenga Kagoda pia.

Aidha stori ya leo ya Mwananchi – ya “Kagoda inamuumiza kichwa DPP” bila shaka ni mlolongo wa haya ninayosema -- kwamba Kagoda sasa inachemka na hivyo RA naye anajipanga kukabili lolote litakalotokea – hata kuamua kuwatumia wanasiasa dhaifu wa upinzani kama akina Profesa.

Isitoshe nani asiyejua kuwa Mhariri Kibanda wa Tanzania Daima ni swahiba wa RA na humtumia mara kwa mara kupitisha stori zake za kijanjajanja?

Alaaa kumbeeee! Ndio maana nikisoma articles za Kibanda naziona zina walakini! Kweli vipande vya pesa vilisababisha YUDA kumsaliti Kristo!
 
Mkuu Mag3,
Soma vizuri ile article; Kikwete hakuwahi kutembelea Houston wakati ule ... Daraja ndiye aliyekwenda Houston! Just kuweka mambo kwenye perspective; na sina maana kwamba Kikwete anahusika au hausiki.

Mkuu umedandia treni kwa mbele - sawa, article inaongelea ugeni wa Balozi Daraja mwaka 2003 wakati huo Jakaya Mrisho Kikwete ni Waziri husika katika serikali ya Ali Hasan Mwinyi lakini ugeni ninaouongelea ni wa Raisi baadaye wakati wa mchakato wa Richmond 2006/2007. Kumbuka kuwa kampuni ya Richmond iliwahi kupewa tenda ya bomba la mafuta Kikwete akiwa Waziri ikashindwa lakini ikaja kupewa tena tenda ya umeme Kikwete akiwa Raisi nayo ikashindwa vile vile - mara zote hizo common factor ni JMK. Mohamed Gire na Kikwete walianzia mbali.....tuendelee.........

Hata hivyo Richmond Development Company hadi leo wanajitangaza hivi:-

After an international competitive bidding process, in July 2006, Richmond was awarded a contract to provide 100MW of power on a BOO for a period of 2 years with extensions.
Richmond designed, secured financing and built the first phase of the plant in 52 days and delivered power on time in accordance with the awarded contract.
After successfully connecting to the grid and with written approval and acceptance from Tanesco, Richmond sold its interest to Dowans.
Almost a year later, a politically motivated parliamentary investigation of the contracting process was conducted, led by a rival faction of the ruling party, resulting in the resignation of the Prime Minisister in February 2008.
Political press in Tanzania and a group of bloggers repeatedly attacked Richmond.
An independent non-political investigation of the contracting process by the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) cleared Richmond of all wrong-doing.

Richmond in November 2008 filed an ICC arbitration against Tanesco for contractual violations, defamation and interference.
We are aware of the misinformation in the politically charged Tanzania press and blogs that support rival factions and parties. However the facts are that Richmond designed, secured financing and built power plant on time and under budget. That plant has been in operation at Tanesco's headquarters in Ubungo and is still fully functional. Tanesco actually sought permission from the government to purchase the plant from Dowans to provide power for the next 25 years.
Na serikali yetu kimya.... kaazi kweli kweli !
 
Rukeni juu mkidondoka ,Mheshimiwa Lipumba amelipasua jipu ,Jipu ambalo wengi walikuwa wanaogopa hata kuliangalia.
Kwa kiswahili kingine tunaweza kusema amemfunga paka kengele ,sasa kama ilikuwa siri na watu wakiogopa ,siri ndio hio imeshawekwa uwanjani ,kuwa hasara inayotokana na Richmond imesababishwa na Kikwete mbali ya saini inawezekana kabisa mkakati aliuanzisha kitambo, ili kuweka mrija. Hivi bado richmond inalipwa ?

Ukichunguza ile ripoti ya Mwakiyembe utakumbuka ile sehemu alilalamika kuwa kuna mambo mengine hawakuyaanika kutokana kuwa ni siri nzito au inaigusa serikali pahala pabaya ,sasa unaweza kupata picha ya palipo kuwa pataiumbua serikali. Na ndipo utakapoona ni jinsi gani Lowasa alitoswa ,na kuondolewa katika Uwaziri Mkuu,na ndio maana utaona Lowassa alikaa kimya na wala hakulalamika sana au kukusanya vyombo vya habari ,inawezekana kabisa ile ya kujiuzulu Lowasa ni mipango ya pamoja na Kikwete ili kufunika mambo ,remember they are from the sane mtandao & well friends.
 
Mkuu umedandia treni kwa mbele - sawa, article inaongelea ugeni wa Balozi Daraja mwaka 2003 wakati huo Jakaya Mrisho Kikwete ni Waziri husika katika serikali ya Ali Hasan Mwinyi lakini ugeni ninaouongelea ni wa Raisi baadaye wakati wa mchakato wa Richmond 2006/2007. Kumbuka kuwa kampuni ya Richmond iliwahi kupewa tenda ya bomba la mafuta Kikwete akiwa Waziri ikashindwa lakini ikaja kupewa tena tenda ya umeme Kikwete akiwa Raisi nayo ikashindwa vile vile - mara zote hizo common factor ni JMK. Mohamed Gire na Kikwete walianzia mbali.....tuendelee.........

Hata hivyo Richmond Development Company hadi leo wanajitangaza hivi:-

Na serikali yetu kimya.... kaazi kweli kweli !

Mkuu,

Ninaweza kukueleza kwa uhakika kabisa kwamba JK hajawahi kwenda Houston, Texas baada ya kuwa Rais; yaani toka 2005.
 
Ni Kwao na ndio wao ndio wameanzisha na kuwamashisha watu kuona na kutambua wewe hujui, Wao walikuwa wapi muda wote?? Mbona yalikuwa yanafanyika wao walikuwa kimnya sana sana why man walikuwa kimnya sana
Josh Michael..
Duh! wangu chadema ndo wameanzisha kuficha ufisadi?,duh! umesahau kama mtu wa kwanza alikuwa ni Lipumba alivoongea na waandishi wa habari kuhusu ufisadi? umesahau aliitasha mkutano wa hadhara jangwani akazungumzia? halafu ndo wakaja kina slaa na zitto.. au coz ni Lipumba,ikiwa slaa ndo sawa.. duh! kweli tutafika?
 
"Mhhh! Pana kitu hapo Zak. Kwanza Profesa ataliitaje sakata la Richmond kuwa ni la kifisadi wakati hivi karibuni alikuwa anaipigia debe mitambo chakavu ya kampuni hiyo (iliyorithiwa na Dowans) inunuliwe na serikali?

Wakati ule Profesa alionekana ametumwa na RA, na haya matamshi yake ya sasa pia yana harufu ya mkono wa RA. Inaonekana uswahiba baina ya JK na RA/EL unaota mbawa polepole!"

________________________

Hard Hitter:

Kidogo umegusa kitu hapo Mkuu. Uswahiba unaanza kuota mbawa. Hivi karibuni Mwanahalisi liliandika kuwa JK alimkacha RA kule Jo’burg wakatiJK alipokwenda kwenye sherehe za kuapishwa Zuma. Baada ya siku chache gazeti hili hili la Tanzania Daima lilikuwa na stori ya kuijanja janja ya iliyomnukuu RA akijaribu kupinga stori ya Mwanahalisi kwamba alikachwa, ingawa RA alikiri kuwapo kule Bondeni wakati mmoja na JK. Alisema hakukachwa kwani huwa wanakutana na JK hapa hapa Bongo.

Lakini kuna habari kuwa suala la Kagoda ndilo linamtesa JK (na RA pia) na inasemekana wafadhili wanambana JK kwa hilo – alitakiwa awafikishe wahusika mahakamani kabla ya kuanza Bajeti ili waweze kufungua pochi zao. Hajafanya hivyo, siku zinakwenda na ahadi za wafadhili zinabakia kuwa ahadi tu.

Hali kadhalika matamshi ya Hosea mwezi Mei kwamba kuna kesi “kabambe za kutetemesha nchi” zingefikishwa mahakamani Mapema Juni kabla ya Beajeti lililenga Kagoda pia.

Aidha stori ya leo ya Mwananchi – ya “Kagoda inamuumiza kichwa DPP” bila shaka ni mlolongo wa haya ninayosema -- kwamba Kagoda sasa inachemka na hivyo RA naye anajipanga kukabili lolote litakalotokea – hata kuamua kuwatumia wanasiasa dhaifu wa upinzani kama akina Profesa.

Isitoshe nani asiyejua kuwa Mhariri Kibanda wa Tanzania Daima ni swahiba wa RA na humtumia mara kwa mara kupitisha stori zake za kijanjajanja?
alaa! kumbe KIBANDA na RA ni maswahiba,umenifungua macho mzee.. na hili Tz Daima ni la nani? hebu nisaidie hapo.. maana naona tayari kuna harufu ya fisadi hapo...
 
Josh Michael..
Duh! wangu chadema ndo wameanzisha kuficha ufisadi?,duh! umesahau kama mtu wa kwanza alikuwa ni Lipumba alivoongea na waandishi wa habari kuhusu ufisadi? umesahau aliitasha mkutano wa hadhara jangwani akazungumzia? halafu ndo wakaja kina slaa na zitto.. au coz ni Lipumba,ikiwa slaa ndo sawa.. duh! kweli tutafika?

Hata tukikubali kwamba -- haya, sawa, Profesa ndiye alianzisha vita dhidi ya ufisadi, kitu ambacho bado sikiamini -- lakini ni viongozi wa Chadema ndiyo wanaendelea kuwasha moto ndani ya chupi za viongozi wa chama tawala kuhusu masuala ua ufisadi, bungeni na nje.

Kwa nini Profesa hakuwa na ujasiri kusimama jukwaani na kutoa majina ya vinara wa ufisadi kuanzia JK mwenyewe -- kama alivyofanya Slaa kule Mwembe Yanga?

Viongozi wa Chadema wanafanya hivi kwa data -- na siyo kutamka tu "Napinga ufisadi" -- na mfano tu ni jana Bungeni pale Dr Slaa alivymuashia moto waziri wa maji kuhusu ufisadi katika mradi wa maji wa Shinyanga.

Sijasikia kiongozi wa CUF akitoa data kama hizo Bungeni -- soma Mwananchi ya leo na magazeti mengine.

Sasa hivi Profesa anawatetea mafisadi, kama vile alivyotetea ununuzi wa mitambo chakavu na ya kifisadi ya Dowans!!!!!
 
Back
Top Bottom