Lipumba amhusisha JK na Richmond | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba amhusisha JK na Richmond

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 13, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wana-JF hii ni stori kuuu ya ukurasa wa mbele wa gazeti la Mtanzania Daima leo. Hivi imekaa vipi stori hii, hasa kwa Profesa kuyasema haya wakati huu, na hasa kwa kupitia gazeti hili?

  (“Operesheni Sangara” katika ibara ya pili ni makosa ya mhariri ambalo bila shaka halitamfurahisha Mbowe hata kidogo.

  **********************

  Lipumba amhusisha JK na Richmond

  * Asema ndiye aliyetoa kibali kwa kampuni hiyo
  * Adai kujiuzulu kwa Lowassa ni kutolewa kafara
  * Asema serikali yajitafutia umaarufu kesi za EPA
  * Aishangaa CCM kukwepa mahakama ya Kadhi


  Tanzania Daima, Julai 13, 2009


  Jinamizi la ufisadi wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond, limefufuliwa upya, baada ya Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, kumtaja hadharani rais jakaya Kikwete, akimhusisha na ufisadi wa kampuni hiyo.

  Lipumba alitoa madai hayo mazito aliyoyaita ‘siri kubwa iliyofichwa’ juzi jioni mbele ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CUF wa uzinduzi wa Operesheni Sangara katika viwanja vya shule ya Mirongo, Kata ya Mirongo, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.

  Akifafanua alisema, taarifa alizonazo zinaeleza kuwa Kikwete ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho kutoa kibali ambacho hatimaye kiliiruhusu Richmond ambayo baadaye ilibainika kuwa ni kampuni ya kitapeli, kuleta mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura.

  Alisema kutokana na ukweli huo basi, mtu ambaye kimsingi alikuwa akipaswa kujiuzulu kutokana na sakata hilo la Richmond lililosababisha kuanguka kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na mawaziri wengine ni rais Kikwete mwenyewe.

  Akiendelea, Lipumba alisema ili kujinusuru na kuanguka au kuwajibika kutokana na kashfa hiyo ya kifisadi ya Richmond, Rais Kikwete aliona ni vyema akamtoa kafara rafiki yake.

  “Wananchi, leo nawatobolea siri juu ya Kampuni ya Richmond… mhusika mkuu wa ufisadi wa Richmond ni Rais Jakaya Kikwete. Ukiangalia vizuri ripoti iliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe, utaona inamhusisha Rais Kikwete na ufisadi huo.

  “Kwa ukweli huo, Lowassa yeye katolewa kafara tu na rafiki yake Kikwete, lakini rais huyu ndiye aliyepaswa na mpaka sasa ndiye anayepaswa kuwajibika kwa taifa. Hatuwezi kufika kwa mtindo huu,” alisema Profesa Lipumba huku akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wa hadhara………
   
 2. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,818
  Likes Received: 2,529
  Trophy Points: 280
  Do hii kali ya mwaka!! lakini uchaguzi 2010 unakaribia kwa hiyo tutapata mengi zaidi ya hayo nahayo ya Kagoda tutayapata tu na wamiliki halali tutawapata yetu masikio.
   
 3. C

  Calipso JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Duh! nafkiri huyu mwandishi anataka kufukuzwa!!! lkn hapo 'sangara' ilikuwaje maana alikuwa anatakiwa aandike ZINDUKA au ndo 'mfupa hauna ulimi'
   
 4. J

  Jafar JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Lipumba - we know this already, give us another script to play. Dont recite the obvious.
   
 5. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mtanzania daima linamilikiwa na nani?Nadhani muhandishi amekuwa biased kiasi kama mimi nilivyo biased katika hoja hii. Mi bado hisia zangu zinaniambia zaidi ya asilimia 80% aliye engineer mpango huu kama hakuwa lowasa basi ni watu waliopoata baraka za lowasa. JK aliingizwa mkenge tu.
   
 6. nkawa

  nkawa Senior Member

  #6
  Jul 13, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks...hana jipya huyo kazi kudandia yawezake......
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mhhh! Pana kitu hapo Zak. Kwanza Profesa ataliitaje sakata la Richmond kuwa ni la kifisadi wakati hivi karibuni alikuwa anaipigia debe mitambo chakavu ya kampuni hiyo (iliyorithiwa na Dowans) inunuliwe na serikali?

  Wakati ule Profesa alionekana ametumwa na RA, na haya matamshi yake ya sasa pia yana harufu ya mkono wa RA. Inaonekana uswahiba baina ya JK na RA/EL unaota mbawa polepole!
   
  Last edited by a moderator: Jul 13, 2009
 8. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,521
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  I conqur with U. Huyu Profesa kaishiwa na kabadilika kuwa kuwadi wa kuwasemea watu. Kuna kipindi aliwahi kumsifia Prof. Mwandosya kuwa ndiye aliyestahili kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania kwa kuwa ni makini. Na sasa anakuja na Operesheni Safisha Mafisadi. TUMESHTUKA SEMA LINGINE PROF WA CUF.
   
 9. U

  Utatu JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2009
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60

  Watu wengine bwana....Ninyi mnaojua mnafanyia nini hiyo kujua kwenu? Hawa wanasiasa kazi yao mojawapo ni kupiga kelele za mwizi...mpaka hatua zichukuliwe
   
  Last edited: Jul 13, 2009
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Mhhh! Pana kitu hapo Zak. Kwanza Profesa ataliitaje sakata la Richmond kuwa ni la kifisadi wakati hivi karibuni alikuwa anaipigia debe mitambo chakavu ya kampuni hiyo (iliyorithiwa na Dowans) inunuliwe na serikali?

  Wakati ule Profesa alionekana ametumwa na RA, na haya matamshi yake ya sasa pia yana harufu ya mkono wa RA. Inaonekana uswahiba baina ya JK na RA/EL unaota mbawa polepole!"

  ________________________

  Hard Hitter:

  Kidogo umegusa kitu hapo Mkuu. Uswahiba unaanza kuota mbawa. Hivi karibuni Mwanahalisi liliandika kuwa JK alimkacha RA kule Jo’burg wakatiJK alipokwenda kwenye sherehe za kuapishwa Zuma. Baada ya siku chache gazeti hili hili la Tanzania Daima lilikuwa na stori ya kuijanja janja ya iliyomnukuu RA akijaribu kupinga stori ya Mwanahalisi kwamba alikachwa, ingawa RA alikiri kuwapo kule Bondeni wakati mmoja na JK. Alisema hakukachwa kwani huwa wanakutana na JK hapa hapa Bongo.

  Lakini kuna habari kuwa suala la Kagoda ndilo linamtesa JK (na RA pia) na inasemekana wafadhili wanambana JK kwa hilo – alitakiwa awafikishe wahusika mahakamani kabla ya kuanza Bajeti ili waweze kufungua pochi zao. Hajafanya hivyo, siku zinakwenda na ahadi za wafadhili zinabakia kuwa ahadi tu.

  Hali kadhalika matamshi ya Hosea mwezi Mei kwamba kuna kesi “kabambe za kutetemesha nchi” zingefikishwa mahakamani Mapema Juni kabla ya Beajeti lililenga Kagoda pia.

  Aidha stori ya leo ya Mwananchi – ya “Kagoda inamuumiza kichwa DPP” bila shaka ni mlolongo wa haya ninayosema -- kwamba Kagoda sasa inachemka na hivyo RA naye anajipanga kukabili lolote litakalotokea – hata kuamua kuwatumia wanasiasa dhaifu wa upinzani kama akina Profesa.

  Isitoshe nani asiyejua kuwa Mhariri Kibanda wa Tanzania Daima ni swahiba wa RA na humtumia mara kwa mara kupitisha stori zake za kijanjajanja?


   
 11. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  If you already know it what have you done so far to stop it?. Take any action to show that you know it, if you can't prevent it, criticise it loudly and publicly not under cover like this, and that's what Lipumba has done.

  Ya wenzake yapi?. Ufisadi hauna mwenyewe unaumiza watanzania wote bila kujali vyama vyao. Bora yeye limemuuma kaliongea bayana kama Lipumba kuliko wewe unayetoa shutumua huku ukiwa umejificha kichakani usijulikane.


  There is no politics in the issue of grand corruption (ufisadi) as long as it hurts us all as Tanzanians, regardless you are a low profile CCM member who waits for election gifts and takrima only in two months of every 5 years while the rest the time struggling to survive or begging for your own rights. It doesn't matter whether you are a nonpartisan or an opposition member, Ufisadi unatuumiza kama taifa sisi wote kasoro wao (mafisadi).
   
  Last edited: Jul 13, 2009
 12. U

  Utatu JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2009
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Thank you.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Is it? Doesnt some of grant corruption crussaders doing so politically?
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapa Mengi alipowataja mafisadi ,walizuka wanaJF na kumpongeza na kufikia kudai hakuna aliewahi kusema au kuwataja aliowataka na mijineno kibao.

  Sasa Lipumba ametaja kichwa cha Mafisadi kuwa ni Mheshimiwa Raisi Kikwete ndie mhusika mkuu ambae ndie alietakiwa awajibike badala ya aliekuwa waziri Mkuu ,sasa kama wengine mliwahi kusema au kumtaja kuwa Raisi wa nchi ndie mhusika mkuu basi mlimtaja mkiwa vichochoroni tena mnaongea na kusikilizana wenyewe kwa wenyewe.

  Mkuu Lipumba naona ameubeba mzigo mzito ambao wengi wenu mlikuwa unawapa tabu kuubeba mkipita mkianguka nao ,kudai kuwa taarifa alizo zinaonyesha Mkuu wa kaya ni mmoja kati ya wahusika, basi ujue kuwa sasa wana ngangari wameanza mambo yao ya kulipuwa mizinga mbele ya wananchi.

  CUF mwisho ,niliwahi kuwambia Chadema wasiwe na pupa kulipuwa mabomu huko au ndani ya bunge hakutasaidia kitu zaidi ya kupigwa danadana na mabomu yatawamalizikia na ndipo walipo sasa.

  Hapa mnaonekana kuwa kwa mitazamo yenu Lipumba amechelewa .lakini ukweli huu ndio wakati mzuri wa kupiga mizinga maana muda wa kuunda kamati na kijirekebisha ikifuatiliwa na uchunguzi wa kina ili kujisahihisha kwa CCM hakuna tena nafasi.
  Tusubiri CCM wadai ushahidi ,na wale waliosema wamechoka kuona viongozi wa serikali na viongozi wa CCM wakitupiwa maneno mazito ya kuwaumbua wakome nafikiri itakuwa wamepata challenge kutoka kwa kiongozi wa juu wa CUF.

  Naweza kusema CUF sasa imevamia Ikulu kwenyewe na kuweka wazi kwa wananchi,na hapa ndio itaeleweka ule ugumu wa serikali iliyokuwepo kuwachukulia hatua wale waliojiuzulu.
  Hongera CUF.
   
 15. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Lipumba endelee kuleta wote wafichue kabla ya 2010 wananchi waamue huku wakijua what CCM stands for??? safi sana go go prof. tuko pamoja nawe.
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna wakati mtu unatoa mawazo kama msomi wa fani hiyo na pia Lipumba yupo sahihi kabisa kwa hili na , Sio kweli hata kidogo kuwa Kibanda ni wa RA
   
 17. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana matamshi ya Prof. Lipumba katika siku za karibuni na kugundua kwamba amegeuzwa kuwa mouthpiece ya RA na fisadi mwenzie EL. Mpango uliopo hapa ni kumsafisha EL ili atimize azma yake ya kuwa Rais. Profesa huyu hayuko peke yake. Fuatilieni kwa makini sana kelele za baadhi ya wapinzani, mtagundua kitu kikubwa. By the way, James Mbatia yuko wapi hivi sasa? Nasikia yupo nje ya nchi anasoma. Anasomeshwa na nani? Mlikuwa mnasikia kauli zake zenye utata kuhusu mafisadi kabla hajatoweka? Watz bado kazi tunayo!
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Umesema ndugu yangu. Profesa kukubali kutumiwa na wenye pesa ina maana amekuwa kushney kabisa. Hakugombea Biharamulo kwa kuogopa aibu, ingekuwa zaidi ya Busanda, na visingizio vipya akawa hana. Karibu atakuwa kama Lyatonga, kuwaponda wapinzani kwamba ndiyo wanakwamiza demokrasia.

  Ni mara chache sana kusikia Chadema inawaponda wapinzani -- tangu wakati ule Mbowe aliposema Muungano wa vyama vinne basi!

  Uswahiba wa Profesa kwa RA umepitia kwa Jussa na kuna siku Lwakatare atatoa siri kuhusu hili ambalo ndilo lilimtapisha akaondoka zake: CUF kuingiliwa na mafisadi.
   
 19. F

  FM JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jafar kujua ni kitu kingine na kuthubutu kusema tena hadharani ni kitu kingine, kama kuna unachojua weka hadharani basi kama Lipumba watu tufaidi. Bila kufanya hivyo hutusaidii mwache Lipumba amwage issues. Kwa haraka haraka naona kama unataka kumnyamazisha Lipumba kama sumari alivyotaka kumnyamazisha slaa kwa kumwambia atafute hoja nyingine.
   
 20. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280

  Hili sakata lilianzia mbali ...........tuendelee...........

  Hakuna ubishi kuwa aliyetembelea Houston na kuwa mgeni wa Mohamed Gire wakati wa mchakato wa Richmond alikuwa ni Jakaya Mrisho Kikwete. Huo ugeni wa nguvu uliwezekana baada ya maandalizi yaliyomhusisha balozi wetu Marekani wa wakati huo, Andrew Daraja. Kinachoshangaza ni kamati ya kuchunguza Richmond iliyoongozwa na Mh. Mwakyembe kushindwa kuianika hili !!!! Kaazi kwelix2.
   
Loading...