Lipumba amepoteza hadhi ya kuwa Mwenyekiti CUF

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Lula wa Ndali Mwananzela Toleo la 296

29 May 2013

WAKATI mwingine unafikiria vitu vimefika pabaya; halafu vinaharibika kabisa! Ni sawa sawa na uone gari lako linapasuka tairi na unajitahidi kwa ufundi wote kuliegesha pembeni na unajua hili ni baya lakini unashukuru Mungu kuwa angalau ni tairi tu utabadilisha.

Unapoegesha gari na kuanza kutoa tairi la akiba na jeki kabla hujatulia rejeta ya gari inaanza kuchemka na moto unalipuka kwenye injini na kabla hujafanya lolote moto unalipuka na kuanza kuteketeza gari lako.

Ukiwa umekaa chini unasikitika maana hata kujaribu kuzima huna nafasi simu yako inaita na unaambiwa mtoto wako kagongwa na gari amekimbizwa hospitali! Kwenye Kiingereza wanasema when you think things are bad, they get worse!

Suala la udini Tanzania tumelizungumza na kufika mahali kujua kuwa tuko pabaya. Tumeshuhudia kauli za ajabu na za kichochezi, hadi tumefika tunagombea nani achinje na nani asichinje huku wengine wakitaka Mahakama ya Kadhi iingizwe kwenye Katiba na wengine wakipinga. Wakati hatujatulia tunaona video za kina Ilunga na wengine wakichochea mauaji ya viongozi na waumini wa Kikristu.

Tukiwa bado tunatafakari hayo na tukiwa hatujatulia katika suala la kuchinja na masuala mengine yenye harufu zote udini, Profesa Ibrahim Lipumba mmoja wasomi mashuhuri wa Tanzania akaja na lake jipya.

Akizungumza kwenye Msikiti wa Idrissa Kariakoo jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumba amesikika akisema kuwa chama chake kilifanya kampeni ya kidini ili kumsaidia Rais Jakaya Kikwete – Muislamu mwenzao ili asije akaangushwa. Bila kumung'unya maneno Prof. Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (Wakiislamu?) amesema kuwa pamoja na kuwa uchaguzi wa 2010 kutokuwa huru na wa haki yeye na wenzie ilibidi watumie mbinu za ziada ili kuokoa "jahazi".

Pamoja na kauli hiyo Prof. Lipumba ameonekana akiwagawa Watanzania kwa misingi ya kidini upande mmoja wakiwepo Waislamu ambao licha ya kumsaidia Kikwete kuupata urais hawakupata matunda yoyote hadi hivi sasa na upande wa pili ni "wenzetu" ambao ni wazi akimaanisha ni Wakristu. Prof. Lipumba akizungumzia hili amesema kuwa "Kwa hiyo kama Waislamu tunataka kupata haki zetu, kama tunataka kuishi kama raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu, lazima tujipange kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015; na sisi tuanze kujipanga kwa sababu wenzetu wameanza kujipanga, vinginevyo tutaendelea kubaki masikini na raia wa daraja la nne katika nchi yetu wenyewe"

Prof. Lipumba amesema mengi sana kwenye hadhara ile kiasi kwamba maswali makini yanahitaji kuulizwa ama kuhusu usomi wake na hekima ambayo watu walitarajia kuwa nayo au amesema vile kwa sababu anajua sasa hivi njia ya kutokea ni hii ya udini. Kwa mtu ambaye ametumikia serikali (kama mshauri wa Rais) na kama mmoja wa wasomi kauli zake ambazo nyingi zinaonesha dalili ya ujinga (siyo tusi) ni wazi ile imani ambayo watu walikuwa nayo kuwa Prof. Lipumba ni msomi inabidi kuangaliwa upya.

Ni usomi gani unaoweza kumfanya mtu kuwa mbaguzi wa wazi ambaye anaiangalia jamii anayotaka kuiongoza kwa misingi ya "sisi dhidi ya wao"? Hivi alipogombea urais mara nne alikuwa anataka kuwa Rais wa Waislamu ili awape Waislamu maendeleo? Wakristu na wale wasio na imani hizi mbili wangeishi vipi katika Tanzania chini ya Lipumba ambaye Sheikh Basaleh akimtambulisha alimtambulisha kama "Rais mtarajiwa"? Kweli Wakristu wanaweza kuwa salama chini ya mtu kama Lipumba?

Lakini pia inabidi twende mbali zaidi na kuhoji kama Lipumba anaweza "kuweka imani yake mbele" kama alivyopongezwa na Sheikh Basaleh mara baada ya Uchaguzi Mkuu (kwa kauli yake mwenyewe) je, anaweza kukiongoza chama cha siasa ambacho ni cha kitaifa ambamo ndani yake wamo Wakristu? Je, inawezekana ndani ya CUF Mwenyekiti Lipumba na Katibu Mkuu Maalim Seif (wote Waislamu) Wakristu wanaweza kuwa na haki yoyote sawa au wanaonekana kama watu ambao wanachukuliwa kama ishara tu ya kitaifa lakini chama kwa kweli ni cha Waislamu chenye kupigania harakati za Waislamu?

Sasa binafsi sina tatizo kabisa na Lipumba kama Muislamu kuzungumzia mambo ya Uislamu – kwangu haijalishi sana; lakini shida inakuja kuwa kiongozi wa umma anaposimama na kuzungumza lugha ya kuligawa taifa jinsi alivyofanya Lipumba kweli anaweza kuaminika? Inawezekana ni kweli Watanzania walitambua huu mwelekeo wa Lipumba ndio maana walimkataa mara nne na tena mara ya nne walimkataa vibaya zaidi?

Lakini swali ambalo linabakia ni jinsi gani Lipumba anaweza kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama cha siasa wakati Mwenyekiti wake anapigania maslahi ya kidini kwa kupitia chama chake akithibitisha kuwa CUF ilifanya hivyo mwaka 2010? Sheria ya vyama vya siasa inakataza kabisa vyama kuundwa kwa maslahi ya kupigania dini au maslahi ya kidini. Kwamba CUF kimefanya hivi na Lipumba amethibitisha swali kubwa linabakia – Je, Msajili wa Vyama vya Siasa ana ujasiri wa kufanya lolote?

Kama Lwakatare kwa maneno ya video ameweza kushtakiwa na kunyimwa dhamana kwa sababu ameoneka na akipanga njama – wengine walisema ugaidi – je, Lipumba ambaye ameonekana akithibitisha kuwa chama chake ni chama cha kupigania haki za Waislamu na hili liko wazi kwenye video na yeye mwenyewe hajakanusha je, John Tendwa ana uwezo wa kusema lolote au ataumauma maneno ya kutaka "kuletewa malalamiko rasmi"?

Ninapoacha maswali haya na mengine nabakia kujiuliza tunafikiri tumefika pabaya je, inaweza kuwa mbaya zaidi ya hivi? Muda utajibu.

Hata akiondolewa CUF bado atasimama kugombea Urais kama mgombea binafsi (rejea rasimu ya katiba mpya), Sheikh Ponda naye anaingia Bungeni kama Mbunge wa Ubungo (mgombea binafsi), Sheikh (jina limenitoka) naye ataingia Bungeni, hata Ustadh fulani naye ataingia Bungeni...hii ni mtake msitake!

Tumenyanyaswa sana acheni nasi tujikongoje ,Nchi yetu wote hii tutabanana humuhumu!
 
Lipumba mimi sijui anakwenda wapi lakini ndiyo mwisho wake unakuja.
 
Hata akiondolewa CUF bado atasimama kugombea Urais kama mgombea binafsi (rejea rasimu ya katiba mpya), Sheikh Ponda naye anaingia Bungeni kama Mbunge wa Ubungo (mgombea binafsi), Sheikh (jina limenitoka) naye ataingia Bungeni, hata Ustadh fulani naye ataingia Bungeni...hii ni mtake msitake!

Tumenyanyaswa sana acheni nasi tujikongoje ,Nchi yetu wote hii tutabanana humuhumu!
Sasa nani atamchagua huu siyo mda wa slaa,lipumba wala lowasa ni mda wa vijana wengine tu.
 
Hata akiondolewa CUF bado atasimama kugombea Urais kama mgombea binafsi (rejea rasimu ya katiba mpya), Sheikh Ponda naye anaingia Bungeni kama Mbunge wa Ubungo (mgombea binafsi), Sheikh (jina limenitoka) naye ataingia Bungeni, hata Ustadh fulani naye ataingia Bungeni...hii ni mtake msitake!

Tumenyanyaswa sana acheni nasi tujikongoje ,Nchi yetu wote hii tutabanana humuhumu!

Kwani MBUNGE BINAFSI wameruhusi?
 
Sideeq,

..mbona tumeshapata kuwa na wabunge ambao ni mashekhe??
 
Last edited by a moderator:
Hata akiondolewa CUF bado atasimama kugombea Urais kama mgombea binafsi (rejea rasimu ya katiba mpya), Sheikh Ponda naye anaingia Bungeni kama Mbunge wa Ubungo (mgombea binafsi), Sheikh (jina limenitoka) naye ataingia Bungeni, hata Ustadh fulani naye ataingia Bungeni...hii ni mtake msitake!

Tumenyanyaswa sana acheni nasi tujikongoje ,Nchi yetu wote hii tutabanana humuhumu!

Sikiliza sijali kama SHEIKH ataingia BUNGENI - kuna Viongozi wa DINI nyingine BUNGENI so it is not my issue as long as anfuata SHERIA ya JAMHURI kuwa SHERIA ya KATIBA kwanza DINI BAADAYE -- sita Jali ...

Kwanini unaongelea kama anatisha? na kuwa watu hawamtaki? ndio makosa yako Unasikiliza HABARI za CHUKI unafikiri ndio kweli -- HATA kidogo labda ndio njia ya kupata wasikilizaji MSIKITINI
 
hii swala ni mtambuka, linahitaji umakini na busara katika kulijadili.. huenda kama taifa tukawa tunaelekea tusikopajua
 
Suala la msingi hapa ,ni kwamba nchi yetu imeingia kwenye Udini mpaka watu wameuana.Sasa tuko kwenye wakati wa kuwatafuta wachochezi,Huyu ni mmoja wapo ambaye anaonekana kulifahamu vizuri suala hili.Kwa hiyo akamatwe na kuhojiwa.
 
Hata akiondolewa CUF bado atasimama kugombea Urais kama mgombea binafsi (rejea rasimu ya katiba mpya), Sheikh Ponda naye anaingia Bungeni kama Mbunge wa Ubungo (mgombea binafsi), Sheikh (jina limenitoka) naye ataingia Bungeni, hata Ustadh fulani naye ataingia Bungeni...hii ni mtake msitake!

Tumenyanyaswa sana acheni nasi tujikongoje ,Nchi yetu wote hii tutabanana humuhumu!

sheikh kuwa mbunge au rais hakuna tatizo! Kuna sheria na kanuni za kufuata. Hofu yangu kwa sheikh Ponda kakutwa na hatia na kuhukumiwa hivyo hana sifa
 
Hata akiondolewa CUF bado atasimama (Lipumba)kugombea Urais kama mgombea binafsi (rejea rasimu ya katiba mpya), Sheikh Ponda naye anaingia Bungeni kama Mbunge wa Ubungo (mgombea binafsi), Sheikh (jina limenitoka) naye ataingia Bungeni, hata Ustadh fulani naye ataingia Bungeni...hii ni mtake msitake!

Tumenyanyaswa sana acheni nasi tujikongoje ,Nchi yetu wote hii tutabanana humuhumu!

Mkuu nafikiri uko katika usingizi mnono wenye ndoto zisizo na mashiko
Huyo jamaa Mdini, Lipumba, hana ubavu wa kupata asilimia zaidi ya 50% ya kura zote nchini.
Kwa kauli alizotoa za kidini pengine ana kura nyingi za msikiti wako!!!!!
 
Hata akiondolewa CUF bado atasimama kugombea Urais kama mgombea binafsi (rejea rasimu ya katiba mpya), Sheikh Ponda naye anaingia Bungeni kama Mbunge wa Ubungo (mgombea binafsi), Sheikh (jina limenitoka) naye ataingia Bungeni, hata Ustadh fulani naye ataingia Bungeni...hii ni mtake msitake!

Tumenyanyaswa sana acheni nasi tujikongoje ,Nchi yetu wote hii tutabanana humuhumu!

Idiot!!! Nani kawanyanyasa? Mnajinyanyasa wenyewe na fikra zenu mgando.
Kwanini msiamke mkaingia kwenye ushindani badala ya kukaa na kupiga kaswida za kunyanyaswa? Kwa takribani miaka saba au zaidi sasa uongozi wa juu wa nchi umekuwa chini ya ya watu wenye imani yenu, je mmetumia vipi fursa hiyo?

Mmekaa kujadili imani za wezenu kwenye mihadhara, badala ya kufikiria ni jinsi gani tutawekeza kwenye elimu na afya. Wezenu hawana muda wa kuchezea kama nyinyi na kukaa kwenye vigenge vya kahawa na kula mirungu. Wanafikiria fursa mpya kila siku.

Mnatakiwa kutumia common sense japokuwa common sense sio common now days.
 
Hata akiondolewa CUF bado atasimama kugombea Urais kama mgombea binafsi (rejea rasimu ya katiba mpya), Sheikh Ponda naye anaingia Bungeni kama Mbunge wa Ubungo (mgombea binafsi), Sheikh (jina limenitoka) naye ataingia Bungeni, hata Ustadh fulani naye ataingia Bungeni...hii ni mtake msitake!

Tumenyanyaswa sana acheni nasi tujikongoje ,Nchi yetu wote hii tutabanana humuhumu!

Tehe tehe tehe!

Nacheka kwa kujiondolea maumivu, watu wa Ubungo tumetukanwa, ngoja niuze nyumba yangu nihamie Rufiji.

Jamani nauza nyumba. Ipo Ubungo Riverside, ina vyumba vitatu vya kulala, sitting room, dining na master bedroom ina AC. Fensi ni ya mchongoma ila kuna parking ya gari 4 na bado inabaki sehemu kubwa tu ya kucheza watoto.

Bei yeyote, ili mradi tu nihame Ubungo kabla ya 2015
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom