Lipumba alivyo mtathimini Kikwete

jobe ayoub

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
203
99
148185_252626404866630_1021907490_n.jpg

‎

Mwenyekiti wa chama cha wannachi (CUF)Pro Ibrahimu Lipumba alisema rais kikwete ana weza kuweka rekodi ya rais wa mwisho... katika kusimamia shughuli za serikali toka tulipopata uhuru , alisema katika marais wote waliomtangulia, rais Kikwete ameshindwa vibaya katika kusimamia masuhala ya taifa.

Je kauli ya lipumba ni ya kwel?

Toa sababu kwa kutaja sehem alizoshindwa kuzisimamia vizuri.
 
Inawezekana ni maneno ya kisiasa tu. Inaweza ikawa kweli iwapo upinzani utaimarisha nguvu zao mapema kuanzia ngazi za chini. Lakini ni kazi ngumu kufikia hilo.
 
Baya kuliko yote.

Ameshindwa kuwaunganisha watanzania kuendelea kuwa wamoja, sasa wamegawanyika kwa misingi ya dini zao kwa uwazi na

wanachukiana bila sababu
kuliko kiongozi yeyote aliemtangulia madarakani. Huko nyuma hali haikuwa mbaya kiasa hiki
 
Lipumba msanii tu angeanza kumtathmini Maalim Seif kwanza kwenye ule mseto

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Ameweza kutengeneza rekodi yake kwa uteuzi usiokuwa makini

- Ameunda serikali yenye kubadilisha mawaziri kama suti kuliko watangulizi wake

-Ameweka rekodi ya mfumko wa bei kuliko ilivotokea hapo kabla

-Ameweka recod ya kushuka kwa kiwango cha elimu bora (quality education) kuliko hapo kabla sasa hivi tuna elimu ya quantity not quality.

-Ameweka rekodi ya kutoa huduma mbaya kabisa za afya, ukitaka kujuwa katibiwe huko serikalini utajuwa.

-Nikiongozi aliyefanya utalii duniani zaidi kuliko watangulizi wake japokuwa uchumi wa inchi hauongezeki kwa tija za safari zake.
 
148185_252626404866630_1021907490_n.jpg

‎

mwenyekiti wa chama cha wannachi (cuf)pro ibrahimu lipumba alisema rais kikwete ana weza kuweka rekodi ya rais wa mwisho... Katika kusimamia shughuli za serikali toka tulipopata uhuru , alisema katika marais wote waliomtangulia, rais kikwete ameshindwa vibaya katika kusimamia masuhala ya taifa.

Je kauli ya lipumba ni ya kwel?

Toa sababu kwa kutaja sehem alizoshindwa kuzisimamia vizuri.



kwa kuwapa matumaini ya maisha yetu wanasiasa wetu uchwara ni wazi kwamba hata tufanye nini matatizo hayatakwisha

ndio maana wengne wanaamua tuh kujirusha

kama maisha ni mafupi sisi tunayarefusha

maisha yamekua mafupi na wanasiasa wanataka kuyafupisha zaidi
 
Kwenye uchumi kwa ujumla maana vitu vinapanda bei kila kukija.
Kodi ya nyumba,
mchele,
nyama,
ada ya shule kama unanunua shule vile
 
ni kweli kabisa, kaunda tume kibao na bado ameshindwa kutoa maamuzi, alipewa orodha ya wauza unga mpaka leo hajashughulika nao, analalamika mafisadi wanauanchi na chama chake lakini hajui kuwa yeye ndo amiri jeshi mkuu na pia kiongozi wa chama, for sure ameshindwa kabisa. Amekua mfanya biashara wa kujenga mahoteli
 
Lipumba msanii tu angeanza kumtathmini Maalim Seif kwanza kwenye ule mseto

Chama
Gongo la mboto DSM

Mseto umewekwa na WAZANZIBARI wenyewe pale walipofanya "Referendum" na 67% walitaka uwepo Mseto. Sasa hapa Maalim anamakosa gani??
"Nashangaa kuna watu wanaumia sana juu ya serikali ya umoja wa kitaifa iliyopo kule Zanzibar wakati tumeiyeka WENYEWE Wazanzibari"
Amani Karume, Kizota.
 
Maneno ya Lipumba ni ukweli mtupu. Angalia elimu inavyoporomoka. Hujaskia wanafunzi wanaomaliza shule ya msingi bila kujua kusoma na kuandika. Angalia uvunjifu wa amani ulivyotamalaki kipindi hiki- migogoro ya kidini, watumishi wa umma na serikali, angalia nidhamu ya watendaji serikalini, angalia uteuzi wa majaji na maofisa wengine wa serikali ulivyo wa ovyo, angalia wawekezaji wanavyopora ardhi ya Tanzania. Angalia watu wanavyokwepa kodi na kuangaliwa tu. Angalia fujo na kutoheshimiana baina viongozi wa ccm, Angalia wahalifu wanavyochekewa mf. wauza ARV feki, Angalia ubabe na ukatili unaofanywa mf kwa dr ulimboka, ufungaji na utishaji wa kutoa mawazo na maoni mf. gazeti la mwanahalisi. Tazama dhulma kwa walimu. Tazama matumizi mabaya ya vyombo vya ulinzi na usalama- kuua mwandishi wa habari na wananchi wasio na hatia kama yule wa morogoro. Angalia matanuzi ya viongozi katikakati ya bajeti finyu ya nchi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom