Lipumba alitumwa na nani kukwamisha mchakato wa katiba mpya?

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,843
1,841
Kama ambavyo amekuwa akikili na kujinasibu mbele ya watanzania ndugu Lipumba pasipo shaka ndio muasisi wa UKAWA, na kupitia hotuba yake maarufu ya "INTARAHAMWE" katika bunge la katiba alitangaza rasmi wapinzani kujitoa katika mchakato wa katiba mpya.

Lakini hata baada ya katiba pendekezwa kupitishwa na bunge hilo tena kwa gharama kuubwa bado serikali ya CCM inayojinasibu kuokoa fedha na kubana matumizi imegoma kuumalizia mchakato huo kwa visingizio eti hauko katika ahadi zao za uchaguzi. Wabunge wa CCM wameshangaa na kupigwa butwaa lakini wachache wanajua.

wakati lipumba akihamasisha kuanzishwa kwa UKAWA na kuhamasisha wapinzani kujitoa katika mchakato wa katiba mpya, Kila mpinzani alimwamini kuwa ni JEMBE la upinzani lenye malengo chanya kwa TAIFA, ambayo hata ivyo hayakuwahi kuainishwa. Hakuna aliyewahi kujiuliza wala kushuku motive ya mchumi LIPUMBA

Ambacho Lipumba na waliomtuma hawakutegemea, wala kukiwazia ni kwamba baada ya kuundwa umoja huo itaibuka hoja ya kuendelea na UKAWA kama umoja wa vyama pinzani katika Uchaguzi mkuu.

Hili hawakulitegemea hata kidogo, na kawaida yao ukianzisha KITU na kikazaa mtoto asiyetegemewa ni kazi yako wewe uliyeanzisha/asisi KUKIVUNJA KITU HICHO na mtoto wake tena kwa gharama yoyote (DEAL WITH YOUR OWN BABY). Katika hili tena LIPUMBA kafanikiwa vizuri tu.

Kwa kuwa wote (namaanisha wananchi wa kawaida, wapinzani na wapenda katiba mpya) TUMESHATAMBUA ya kwamba LIPUMBA si mpinzani wa kweli, wala si mwakilishi wa kweli wa sera za wapinzani, swali gumu ni JE NANI ALIMTUMA LIPUMBA KUWASHAWISHI WAPINZANI ILI KUKWAMISHA KATIBA MPYA? JE LIPUMBA ALIKUWA AGENT WA taasis gani, Nchi gani au ni kundi la watu gani?
 
Nitarudi. ... nafuatilia hivi vikao vya siri vya ccm,sijui zanzibar imewakaba koo
 
kama ndio huyu Jamaa ni proffeser kweli kama kaweza kuwaingiza kina zero kingi kazi ipo
 
Back
Top Bottom