Lipumba akataa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa mojawapo wa kamati za Bunge

Wanasiasa wetu ni majanga tupu.

Huyu ndiyo anaona leo hayo mapungufu baada ya kubwagwa jana na Anna Abdallah katika kinyang'anyilo cha uenyekiti wa Kamati namba 10.

Katika picha hii chini alikuwa anafanya nini?. Ina maana kama angechaguliwa kuwa mwenyekiti na kugundua kuwa kuna viongozi wachache kwa upande wa Zanzibar, angejihudhuru?.

Ninadhani ameamua kutumia hoja kuhusu uchache wa wajumbe wa Zanzibar kukataa cheo kwa sababu ingekuwa ni aibu sana kwake kama Mwenyekiti wa CUF Taifa kubwagwa katika kura zilizofanyika jana halafu tena apewe uongozi wa kihisani na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.

Nikisema anatafuta political cheap popularity nitakuwa nimekosea?. Nikisema ana agenda zake nitakuwa ninakosea?. Nikisema hana msimamo anaousimamia kwa faida ya Taifa nitakuwa ninakosea?.

Halafu huyu ndiyo Chairman wa The Alliance for People's Constitution (UKAWA). My foot!

Sura zaidi ya moja za viongozi mbali mbali walioko kwenye usukani wa kisiasa ndiyo zinadidimiza safari ya kimaendeleo nchini.

821.jpg

Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti katika kamati No. 10 ya Bunge Maalum la Katiba Prof. Ibrahim Lipumba akimpongeza Mhe. Anna Abdalah baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo.(Picha na Owen Mwandumbya – Sekretariat ya Bunge Maalum).

Yangu macho na masikio.
 
Hamna katiba hapo bali ni genge la WAHUNI la CCM wamekutana Dodoma kutunga waraka kuhakikisha CCM haitoki madarakani!
Bunge makini linalofanya kazi kwa maslahi ya watu haliwezi mchagua Sendeka wala Chenge kuongoza kamati
 
Kukubali au kukataa kwangu mm ni sawa tu kutokana na sababu zilizopo., lakini hapa sasa tahadhari ni ccm kuupata huo mwanya na kuanza kuutimia na kutumaliza kabisa kabisa
 
Mm nampongeza sana lipumba na pia nimemshangaa Yule Baloz Mahalu kukubali uteuzi huu sasa Kama angefungwa Mchango wake tungeufuata segerea ?
 
It,s painful 4 wat ccm ar doing now! Shame on zem. Wadau ze process has already consumed 90b/= taxpayers money so far, yet no optimism of getting ze conzt in tym.ccm ziolots in ze ar palarazing ze process. No wonder wadau if sita n his alies continue zis ze process will end up in breakin. Oposition n ze 201 members shall walk out n leav ccm alone,a move zat shal lead zem too 2 parcel n pave ze seats 4 ze bunge budget sessions. Stand firm 2 curse n zea partsansm
Nilisema hapa kuwa mchakato huu hautafika destination,baada ya Hotuba ya Ba'Mkwe
 
Nakushukuru sana profesa wa kweli ninaamini na hawa wafuatao wataiga mfano wako


dr. Lyatonga mrema
cheyo
dovutwa
makaidi
na vikaragosi wengine wote

Kwenye hiyo list hamna hata mwenye ubavu wa kukataa cheo chochote cha kupewa. Kuna wengine hapo waligombea urais kura walizopata hata diwani wetu alimzidi.
 
Sijui kwanini Lipumba amekubali kuwa mjumbe wa Bunge la Katiba, maana jina lake ni miongoni mwa zile 201. Sina uhakika kama katika uteuzi wa majina yale na hata uwiano wa Bunge lenyewe Lipumba alikuwa anakubaliana nayo kwa asilimia Mia moja! Hata hivyo nampongeza kwa kuchukua hatua muhimu hata kama amechelewa.
 
kwa kweli hata mimi amenifurahisha sana kama alivyonifurahisha kangi lugola kwa mchango wake.

Kwa kweli amenifurahisha sana huyu profesa. Huyu Sitta kama alikuwa anatarajia kugombea uraisi aandike kaumia kutokana na ubabe wake. Nadhani huyu jamaa anazeeka vibaya au maji aliyoyarudia chura kayakuta ya moto au ni ya bahari yenye chumvi na hivyo yamemshinda.
 
Hamna katiba hapo bali ni genge la WAHUNI la CCM wamekutana Dodoma kutunga waraka kuhakikisha CCM haitoki madarakani!
Bunge makini linalofanya kazi kwa maslahi ya watu haliwezi mchagua Sendeka wala Chenge kuongoza kamati

Halafu kumbe huyo Sendeka ni no school? Ndiyo maana anasaidiwa kujenga hoja na Chenge. Sasa ataongozaje kamati? Mh! Haya.
 
Lipumba bado anakumbuka jinsi walivyoingizwa chaka na Ccm kule Zanzibar hawezi kuludia kosa!
 
Unapomkosoa Lipumba ni sawa na kumkosoa mwalimu wako aliyekutoa ujinga shuleni,KWA HILI HEKOO LIPUMBA.wajinga mutajijuuuu.
 

Attachments

  • 1395774786458.jpg
    1395774786458.jpg
    27 KB · Views: 94
Wajumbe wa bunge la katiba wenye itikadi ya CCM ni wapatao 400.

Bunge zima la katiba lina wajumbe 639. Kiasi cha kufanya zaidi ya 70% kuwa wenye itikadi ya CCM.

Katika hali hiyo, tunatarajia kamati za bunge hili ziongozwe na mjumbe kutoka chama pinzani?!

Jamani, Watanzania ndio wamewachagua wabunge wa CCM kwa wingi wao. Katiba ni ya Watanzania. Hivyo sioni tatizo kwa CCM kuongoza kamati zote.

Kama CHADEMA au CUF wanataka madaraka, wajitahidi kwenye uchaguzi mkuu 2015 kushinda viti vingi bungeni. Otherwise, watabaki kusubili sana.
 
View attachment 147128

Duh! unafiki mbaya sana Lipumba leo anajifanya kukataa uteuzi huku mambo mengi tu kakubaliana na CCM kama hili la kumpongeza JK Baada ya uchaguzi wa 2010

View attachment 147129

Hawa ni wale wafuasi wa CUF waliokamatwa na kuteswa kule Mtwara kilichosikitisha ni huyu huyu Lipumba baada ya tukio hili alikwenda Ikulu kupeleka malalamiko yake na yeye na viongozi wenzake walijinadi kuwa watafungua kesi juu ya walichofanyiwa hawa ndugu lakini hadi leo Kimya si Lipumba wala Mtatilo waliotia neno tena baada ya kutoka Ikulu.

Wahenga walisema,"Kufanya kosa, si kosa, kosa, kurudia kosa!" Kwa tendo ulilolifanya Lipumba, siku ya leo, wazalendo, tumeyasahau yote ya nyuma! BIG UP Lipumba! Umeandika historia, wazalendo watakukumbuka vizazi na vizazi!!!!!!!!! CCM wanasaga meno, hawaamini kwamba huyu ndiye Lipumba wanayemjua! Usirudi nyuma!!!!!!
 
kuita binadamu mwenzako kikaragosi ni kosa na ni ushamba usiokuwa na mantiki. unadhan wewe ni bora kuliko hao unaowaita kikaragosi. kila mtu ana msimamo kulingana na anavyoolewa mambo, huwezi kulazimisha kila mtu akufuate wewe unavyotaka, shimdana kwa hoja na wala si matusi ni ushamba na ulimbukeni wa mambo
 
Back
Top Bottom