Lipumba aishukia Tume ya Jaji Warioba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba aishukia Tume ya Jaji Warioba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 15, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"] [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 15 July 2012 10:26 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]
  Profesa Lipumba mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF
  Joseph Zablon


  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeishukia Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba kikidai kuwa tume hiyo ni mtego wa kisiasa unaoweza kuitumbukiza taifa katika matatizo ya kiasiasa.

  Tume hiyo inaongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph warioba ikiwa na wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF, jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba alidai kuwa ni ‘ndoto ya alinacha’ tume hiyo kumaliza kazi zake kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

  Alisema ni muhimu ikaundwa kwanza tume huru ya uchaguzi badala ya kusubiri inayotegemea mabadiliko ya katiba aliyosema kwa hali ilivyo yatafanyika baada ya mwaka 2015 kwa kuwa tume ya katiba itakuwa haijamaliza kazi yake.

  “Tumewekwa katika mtego wa kisiasa utatutumbukiza katika matatizo bila sababu za msingi,” alisema Lipumba.

  Aliongeza kuwa miezi 18 iliyopewa tume hiyo ni michache na kwamba hali hiyo imechangiwa na Rais Jakaya Kikwete kushindwa kutekeleza ipasavyo majukumu yake ya kisiasa.

  “Miezi 16 kabla hajaunda tume tulimtaka afanye mabadiliko ya katiba, lakini hakuchukua hatua zozote hadi hivi karibuni alipounda tume hiyo ambayo itafanyakazi hadi Aprili 14 mwaka 2015,” alisema Lipumba.

  Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa baada ya hapo kitakachofuata ni kujadili mapendekezo hayo katika bunge la katiba kabla ya kura ya maoni kupigwa na wananchi na baadae muswada huo kuwasilishwa kwa Rais ili aidhinishe na katika mapendekezo hayo ndipo kunakotarajiwa kyuibuliwa ka suala la tume huru ya uchaguzi.

  Alisema kuwa tume hiyo ina walakini mkubwa na kwamba hakuna atakayekubali kuibngia katika uchaguzi mkuu chini ya Tume ya Uchaguzi (NEC), ya sasa akitoa mfano wa tofauti za takwimu za watu wanaojitokeza kupiga kura aliosema idadi yao inashuka kila chaguzi.


  Alisema Lipumba kikao hicho pia kitajadili suala la madaktari ambao aliwataka kwa sasa warejeee kazini kutokana na ukweli kuwa suala lao limegubikwa na hombwe na uongozi kwani sera ya afya ya mwaka 2007 ilianisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na madai ya madaktari ya sasa.

  “Sera alishiriki kikamilifu kuiandaa Waziri wa Afya wakati huo, Profesa David Mwakyusa lakini alipoikamilisha akaondolewa katika nafasi yake hiyo licha ya kuwa alikuwa mbunge jimboni kwake na kuteuliwa watu wengine wapya ambao hawajashughulika na sera hiyo.

  Lipumba alisema madaktari wana hoja na serikali haiwezi kujondoa katika kashfa ya kupigwa, kujeruhiwa na kutupwa porini kwa kiongozi wa mgomo huo, Dk Steven Ulimboka na kuilichotokea ni fedhea ya serikali.

  Pia Lipumba alisema kikao hicho kitapitia pia njia za kuichukua ili kukabili mfumuko wa bei ambao umechangiwa na serikali ya CCM ambayo imeshindwa kusimamia uchumi kwa kutoa kipaumbele katika bajeti yake katika matumizi ya kawaida kuliko kilimo na maendeleo hali ambayo inachangia mfumuko wa bei.

  “Tanzania iliridhia mkataba wa kutaka kila serikali katika Jumuia ya Uchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaotaka bajeti za nchi wanachama kutenga asilimia 10 katika kilimo lakini cha ajabu toka wakati huo hadi sasa ikiwa ni miaka 20 serikali haijaweza kutenga hata walau asilimia 7 kwa ajili hiyo” alisema.

  Profesa Lipumba alisema mbaya zaidi mwaka huu fedha zilizotengwa kwa ajili ya kilimo ni wastani wa asilimia 3 ya bajeti nzima na kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa mfumuko wa bei lazima utakuwa wa juu zaidi ya uliopo sasa wa asilimia 18 kiwango ambacho ni zaidi ya kile cha mwaka jana 2011 cha asilimia 8.

  Lipumba alisema kikao hicho cha baraza kuu ambacho kitaibuka na dira ya uchumi na uongozi 2015, kinataka serikali itoe tamko ili kuondoa mkanganyiko ambao unaelekea kuzua mgogoro baina ya wasilamu na wakristu hasa baada ya Televhsieni ya Taifa (TBC) kutoa takwimu za watu zisizo sahihi.

  “Watoe tamko kumaliza mtafaruku uliopo kama kweli wanataka sensa ifanyike kwa amani na utulivu” alisema Lipumba.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nakubalina nawe mr prof haya maneno yako yatakuwa shahidi tume yakatiba isipokuwa makini kutatokea matatizo nivema tume ya warioba ikaishauri pia serikali juu ya ushauri wa profesa mtaalam wa uchumi
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Well said Prof. Lipumba..
   
Loading...