Lipumba aanze yeye kujiuzulu- Jaji Makame | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba aanze yeye kujiuzulu- Jaji Makame

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Babuji, Mar 11, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Mar 11, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi Nchini Jaji Mstaafu Lewis Makame amesema iwapo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba anamtaka yeye ajiuzulu wadhifa wake ni vema akaanza yeye kufanya hivyo.

  Kauli hiyo ya Jaji Makame inakuja kutokana na Mwenyekiti huyo wa CUF kumtaka ajiuzulu kwa madai kuwa hana jipya la kusaidia vyama vya siasa na wananchi wanaotaka mageuzi tofauti na kulinda maslahi ya Chama Tawala cha CCM.

  Jaji Makame alisema hajaona sababu ya yeye kujiuzulu kwani anaamini kuwa yeye ni mwadilifu na anatekeleza kazi zake kwa mujibu wa katiba na sheria zilizipo.

  Mwenyekiti huyo wa Tume ya Uchaguzi alisema suala la mtu kukosea lipo kwa binadamu yoyote lakini kwa upande wake haamini kwamba amefanya makosa ya kumlazimu ajiuzulu wazifa wake.

  Alisema Lipumba anapaswa kuonyesha mfano yeye kutokana na ukweli kwamba ameshiriki katika chaguzi mbalimbali zaidi ya mara tatu bila kushinda hivyo hana jipya lolote kwa chama chake.

  Mwenyekiti huyo alisema Profesa Lipumba amekuwa akitumia hoja hiyo ya kumtaka kujiuzulu kwa kuwahadaa wanachama wa chama hicho ambao wameshindwa kubaini udhaifu wa kiongozi wao.


  Source:
  Nifahamishe.com
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Lewis Makame anaonesha kuwa amekubali makosa, lakini hiyo haitoshi. Hakuna asiyejua kuwa yeye ameifaya tume ya uchanguzi kama idara ya CCM, aitufanye wajinga kwa kuwa tunafahamu ni yapi amefanya kuhakikisha CCM inashinda na kuwafanya opposition ikiwa ni pamoja na Lipumba wawena hard time. Japokuwa siwezi kumlaumu moja kwa moja kwa kushindwa kwa vyama vya upinzani, yeye ana mindset ya chama kimoja vyama vingie kwake ni kama udhia.
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huwezi amini haya maneno yanatoka kwa mtu ambaye alikuwa Jaji, ambaye anatakiwa kuweka kando upenzi na kuisimamia haki. Analipa fadhila moja kwa moja kwa waliomchagua (CCM). Manake Mwenyekiti wa tume unapolaumiwa unatakiwa kujibu tuhuma hizo na kusema kuwa zipo ama ni uzushi, na kama zipo kweli unazitatua vipi. Sio kujibu kama mwanasiasa.

  Nashindwa kujua hivi angelaumiwa na Kiongozi wa CCM angesema kuwa kashindwa kuongoza chama chake. Hapa kabisa anaonesha jinsi tume isivyo huru. Lakini hata Jaji Liundi alipoondolewa kuwa msajili wa vyama si alijaribu kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki kupitia CCM, sitashangaa na huyu atafuata mkumbo huohuo.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huwa nasema kila siku kuwa hatuna Katiba wala Tume ya Uchaguzi wala vyombo vya dola maana hawa wote ni wafuasi wa SUltani CCM ,si mdhamini wa Vyama vya Siasa wala hawa walioko kwenye tume wote ni mamluki au ni wafadhili waliofadhiliwa na Chama tawala kuwekwa kwenye sehemu nyeti na za udhibiti.

  Wapinzani haina haja ya kupigashana kelele na walowezi hawa ,lazima madai ya kweli kuhusu Mabadiliko ya Katiba na Tume Huru ya uchaguzi yapigiwe makelele ya nguvu ,ili kukomesha hizi jeuri za mamluki wa Chama Tawala waliojificha katika vyombo hivi vinavyosimamia haki ya Mtanzania.

  Vyama vya upinzani ni lazima viamshe hisia za wananchi kuhusu madai haya na sio kuzungumza na vyombo vya habari au wanapohojiwa ,madai yapelekwe kwa wananchi hakuna njia ambayo itaweza kusikilizwa na Sultani CCM zaidi ya wananchi wote kuungana ili kudai madai haya kwa nguvu na umoja.Hizi kauli za akina Makame ni jeuri tu wakiona wao wapo juu ya sheria na hakuna wa kuwagusa.
   
 5. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Pamoja na kuwa ametoa unproffessional comments lakini alichosema ni sahihi kwani sioni sababu ya viongozi wanaoshindwa uchaguzi kuendelea kungangania madaraka kwani kushindwa maana yake ni kuwa wewe sio competitive figure katika political philosophy kama ilivyo kwenye biashara ukishindwa kuwa competitive unawapisha wenye uwezo waweze kuendesha chama.

  Mfumo wa anayeshindwa kuachia ngazi unatumika kwenye nchi nyingi zilizoendelea kwanini hatuwezi kuiga mifumo ya aina hii na kuwapa nafasi watu wengine waweze kujaribu competitiveness yao.

  Au ndio mambo ya usurutani wa kukaa madarakani kwa miaka nenda rudi, sasa huyo mmpe urais huone anakuwa kama kibaki kenya
   
 6. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Umenena ukweli lakini subiri Mwiba atakavyokushambulia.
   
 7. C

  Chuma JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Utashindaje wakati mazingira ya kushinda hayapo?...Huyu Jaji Bwege ktk Mabwege au wamekuwa wakiandaa mazingira ya CCM kushinda siku zote...

  Tume haipo Huru...lkn wanayoyafanya pia Hayapo huru...maana kama wamechaguliwa na CCM, na kama wangeamua kutelekeza Haki asingelaumiwa....

  Ukiliangalia zoezi zima la Uandikishaji hadi ushaguzi halijakaa sawa... Upinzani unatengenezewa mazingira kuonekana dhaifu kwa vigezo vya chaguzi ambazo hazina transparency...
   
Loading...