Lipo wapi tatizo kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Tafakari!

Great Bro

Member
Oct 3, 2019
9
5
It has been a tradition to relish the festival and celebrate the founders of our Union Mwalimu Nyerere and Abeid Karume to parades. However, it has been a sin, too dangerous for anyone to question or want to critique this Union.

My purpose here is not to question the history or legitimacy of the Union of Tanzania but its benefits as a result of the Union system by the Constitution of Tanzania, the existing powers such as the Courts, Parliament, and the House of Representatives to mention a few.

Wazanzibari wanaishi Tanganyika na kumiliki ardhi bila tatizo Ila wanaotokea bara wanapewa masharti kumiliki ardhi Zanzibar.

Wazanzibar wanafungua biashara Bara ila ukiwa mzawa wa bara ni ngumu kumiliki biashara Zanzibar labda uonge au uwe na Wazanzibari wenye nguvu serikalini. Kwenye harakati za kulisaka tonge nimekutana na huu mkasa na sijui mwisho wake ni upi ikiwa vijana tunaambiwa kujiajiri. Biashara halali na yenye manufaa mapana katika jamii ila unaambiwa hupati kibali kama siyo Mzanzibari!

Wazanzibari wana Baraza lao la Mitihani na hawataki kusikia unatumia mtaala wa NECTA kwa shule za msingi na maandalizi (chekechea). Kwani Wizara yao ya Elimu inafanya kazi gani ikiwa kiwango cha Elimu visiwani kipo chini sana? Unakuta mtu yupo kwenye kitengo kilekile zaidi ya miaka 20!

Wana bendera yao !

Wazanzibar wana vitambulisho kama Wazanzibar na siyo Watanzania!

Swali;
Je, kwa nini tuliweka baadhi ya vipengele Fulani (Articles of Union 'signed in 1964) kwenye masuala ya muungano na vingine visiwe? Vipengele hivyo vipo 11 tu.
Je, Muungano huu una maana gani ikiwa vipengele ilivyoko vinakinzana na lengo kuu ya kuunda Taifa lenye nguvu na umoja?

Je, Wananchi wa Tanzania, wananufaika vipi na Muungano huu na wanaathirika vipi kutokana na Muungano huu na mfumo wake?

Je, kuna haja ya kuupitia Muungano na ama kupengua vipengele fulani au kuunganisha kila kitu na kuwa na sura moja bila kutofautisha ya hili la Watanganyika au Watanzania Bara na lile ni la Wazanzibari?

NB: maswali mengine nimeyapata kwa wadau wengine ila ni muhimu tukiyagusia kama familia moja.

Asante.
 
Mind you there are currently 22 articles of Union as scheduled in The Constitutions of both sides.

Secondly, I always take this Union as forced marriage whose Spouses never loved one another let alone intended to marry but were forced by their Parents.
 
Katika Vitu Ambavyo Nyerere Bila Kuvifanyia Kazi Kwa Ufasaha.

Basi Ni Ili Janga la Muungano Fake Wa Tanganyika Na Zanzibar.

Tageti Yake Ilikuwa Ni Kuwafanya Watanganyika Wawe Wamoja Na Wala Hakuna Kitu Kingine Na Alifanikiwa"
 
Kama Zanzibar ni nchi kuna haja gani kulilia muungano?! Tizama EAC kila mtu kivyake, wafanye yao waache kulialia.
 
Katika Vitu Ambavyo Nyerere Bila Kuvifanyia Kazi Kwa Ufasaha.

Basi Ni Ili JangaMuungano Fake Wa Tanganyika Na Zanzibar.

Tageti Yake Ilikuwa Ni Kuwafanya Watanganyika Wawe Wamoja Na Wala Hakuna Kitu Kingine Na Alifanikiwa"
Great point! Sisi wanyonge ndio tunaumia aseh. Itafikia hatua Rais wa Jamhuri atakuwa anapokelewa Zanzibar kama balozi maana ikulu ipo moja. Na pengine akienda Zanzibar huwa anafikia hotelini.
 
It has been a tradition to relish the festival and celebrate the founders of our Union Mwalimu Nyerere and Abeid Karume to parades. However, it has been a sin, too dangerous for anyone to question or want to critique this Union...
Leo Tarehe 26 April, 2020 ni sikukuu ya Muungano, sikukuu hii ndio sikukuu muhimu kuliko hata uhuru kwasababu hii ni siku JMT ilipozaliwa. Lakini kutokana na janga hili la Corona, siku hii inaadhimishwa kimya kimya.

Naawatakia Muungano mwema huku nikisisitiza. Nautakia huu muungano wetu adhimu udumu milele na hivyo kukitokea yoyote anayetaka kuuchokoa muungano, namshauri chokochoko amchokoe pweza, muungano hutauweza kwasababu tutaulinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia muungano mwema.

P
 
Wewe Mayalla sauti yako ni kubwa kidogo, waambie hao jamaa zako wawatoe mashehe wazanzibar gerezani kama ni kweli wanataka ustawi wa kimuungano.
 
Back
Top Bottom