Lipo kwetu na ndani ya uwezo wetu....

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Eti aliyeitia nchi katika mkenge huu wa deni la B94 kwa Dowans ni watanzania wenzetu, wapo wale ambao walisaidia kuisajili kampuni hewa Dowans na wengine kuvaa gwanda la uzalendo ili kuisaidia hapa nchini kama akina Rost, eti kumbe na yule Jaji aliyedhaniwa atakuwa mzalendo kugoma kusajili wa Tuzo ya ICC Tanzania lakini akaenda kinyume na matarajio ya wengi ni Mtanzania mwenzetu,  na wanaoshabikia kuwa deni lazima lilipwe akiwemo Mhe, Jaji Werema ;(mwanasheria Mkuu wa serikali ambae ofisi yakealiyepaswa kuishauri Tanesco kwa usahihi kuhusu ununuzi wa mitambo ya dharura na badae kuhusu kesi yake na Dowans lakini ikaishia kuiacha Tanesco ikiingia mkenge,) ni wenzetu,. nI mwenzetu, huyu Werema ambae kwa mujibu wa Sheria inayoanzisha Ofisi yake na katiba ya JM wa Tanzania, 1977 ana mamlaka ya kuchukua kesi yoyote ile yenye maslahi ya umma kama hii ya Tanesco lakini akaiacha kwa kampuni binafsi yenye ubinafsi ya Uwakili ili kukwepa lawama. Ni wenzetu hawa ambao waliliahidi Bunge kushughulikia mapendekezo 23 ya Kamati ya Mwakyembe lakini baadae wakaja na hoja ya kuliondoa suala la Richmond Bungeni na kuwasafisha wale wote waliohusika kwa madai kuwa Serikali ingepata hasara kubwa ikiwa wangewachukuliwa hatua za nidhamu.

http://www.google.co.tz/url?sa=t&so...WW1ahC&usg=AFQjCNE86pQLJANkA7E8lC9jQSQitN2S-A
http://www.google.co.tz/url?sa=t&so...Wwzc0z&usg=AFQjCNFXrJwHrbg30WO7YrCGXPaiOYa1_A

Na wale wanasheria walioenda kuitete Tanesco ICC pasipo hata kuthibutu kuweka pingamizi kuhusu uhalili wa Dowans kurithi mkataba wa Kampuni  hewa ya Richmond ambayo kwa wakati huo ilikuwa ikifanya kazi nchi na Mkurugenzi mmoja tu (Bw, Mohamed Gire) kinyume na Sheria ya Makampuni inayotaka kampuni yoyote binafsi (Private Company) ili iwe halali ni lazima wakurugenzi wake wasipungue wawili (two director) ni wenzetu.  Hata pale tulipodhani kesi ya Jinai ya Jamhuri dhidi ya Mohamed Gire ingetoa mwanga na matumamini kwa wauala hili, tulikuja kusitaajabu ni Mtanzania mwenzetu hakimu wa Kisutu akimwachia kuwa hana hatia..ns ni wenzetu ambao walishindwa kuidhibitishia Mahakama juu ya hatia ya tapeli huyo.

Eti hata tusipolipa na Dowans  wakiamua kufungua dai la kuidhalau mahakama watafungua hapa hapa nchhi  kwetu na kwa kutumia sheri zetu  na ikiwa itaamuliwa kuuzwa mali za Tanesco labda kwa   mnada, manada huo si shaka utafanywa na watanzania wenzetu, na mali hizo ;zitanunuliwa na watanzania wenzetu au watu ambao tutawapa kibali wenyewe kuingia nchini kununua mali hzo iwapo si watanzania.Ikiwa Meneja wa Tanesco atakana kulipa deni na apelekwe Mahakamani kama mfungwa wa madai (civil prisoner) atapelekwa kwenye magereza yetu na ni askari wetu ndio watakaomlinda asitoke. 

TUNAAMBIWA TUSIPO LIPA ETI TUTAIDHARAU MAHAKAMA YETU, HIVYO TULIPE TU ILI TUJENGE HESHIMA YA NCHI YETU KWENYE SURA YA DUNIA ILI TUONEKANE PIA TUNA HESHIMU UTAWALA WA SHERIA ILIHALI WATANZANIA WENZETU WANAZIDI KUUMIA KWA UMASKINI NA KUKOSA HUDUMA. KWA ZILE ZILIZOHUSU WATU WETU KAMA ILE YA VALAMBHIA, NK HIZO TULIONA TUNADAIWA NYINGI LAKINI HAZIKUFIKA HATA BILIONI KAMA HIZI ZA DOWANS, TUKAKIMBIA KUBADILI MPAKA SHERIA KWA LENGO LA KUONDOA UWEZEKANO WA MALI ZA BOT KUKAMATWA..LAKINI HILI HATUWEZI KUKWEPA KWA KUBADILI SHERIA YA TANESCO KUPITIA WABUNGE WETU ILI MALI ZAKE ZISIKAMATWE KWA KUWA;HILI NI LA WENZETU WAKUBWa (...)

>The Companies Act Cap. 212 R.E 2002
section 29.If at any time the number of members of a company is reduced, in the case of a private company, below two, or, in the case of any other company, below seven, and it carries on business for more than six months while the number is so reduced, every person who is a member of the company during the time that it so carries on business after those six months and is cognisant of the fact that it is carrying on business with fewer than two members, or seven members, as the case may be, shall be severally liable for the payment of the whole debts of the company contracted during that time
, and may be severally sued therefor.</strong></div>

http://www.google.co.tz/urlsa=t&sou...Xv04FD&usg=AFQjCNEE4y4fTjFgeqJwKl1s2zPvRM-ABw
 
Ingekuw amri yangu hawa mafisadi wakifungwa kila mwisho wa mwezi wanapelekwa uwanja wa wataifa wanalala katikati ya uwanja kila mtanzania anapita anakunya kwenye nyuso zao
 
Ingekuw amri yangu hawa mafisadi wakifungwa kila mwisho wa mwezi wanapelekwa uwanja wa wataifa wanalala katikati ya uwanja kila mtanzania anapita anakunya kwenye nyuso zao

Tunawafahamu lakini tumeamua kuwalinda kwakuwa ni wenzetu.
 
Back
Top Bottom