Lipigie kura Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuweza kushinda kipengele cha ‘Best Government Page of the Year 2020’

TANESCO

Official Account
Jul 12, 2014
4,584
2,104
Lipigie kura Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuweza kushinda kipengele cha *Best Government page of the year* kwa mwaka 2020.

Cha kufanya;

1. Fungua hiyo link utakutana na neno Vote chini kabisa ya ukurasa

2. Utakutana na Vipengele vitatu yani *Award Category*, *Sub Category * na *Selection*

3. Kwa upande wa Award Category chagua *DIGITAL GOVERNANCE* na chagua *BEST GOVERNMENT PAGE OF THE YEAR* kwenye kipengele cha Sub Category

4. Kwenye kipengele cha Selection chagua TANESCO

Hatua ya mwisho wameandika VOTE NOW! Bonyeza hapo na utakua umefanikiwa kupiga kura yako. Asanteni sana na tunaomba ushirikiano wako!


 
Kulinganisha na upupu ulipo nchini kweli nyie mnajitahidi, yaani in a city of blind people, a one eyed person will be the King. Hivi kuna category ya worse company niwapigie NIDA (by the way hivi NIDA ni shirika au ni nini ?)
Nida ni mamlaka
 
Mshukuruni Mungu sana hamna wapinzani wa kutoa huduma ya nishati ya umeme.
Mafisadi wametakatisha sana na kula kodi zetu sana kupitia hili shirika.
Huduma zenu mbovu kuanzia kuunganisha umeme, huduma kwa wateja na hata dharura.
Na ubovu wa katiba yetu hakuna mahali pa kuwawajibisha.
Huduma mnayotoa ingekuwa na competition kama bank au mitandao ya simu mngekuwa out of business miongo kadhaa iliyopita.

Acheni kebehi, Mkipiga kura waajiriwa wote mnaweza kushinda pia. Sio lazima tupige kura sisi maana ntapiga kura kwa mazuri yapi !? Kwa huduma zipi !? Hata mkishinda itakuwa ni ushindi batili tuu maana hamna vigezo kabisa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom