Lipi ni hitaji kuu la Watanzania kwa Rais wanatemtaka 2020? Je ni Tundu Lissu au Magufuli?

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
✳LIPI NI HITAJI KUU LA WATANZANIA KWA RAIS WANAYEMTAKA 2020? JE NI TUNDU LISSU AU MAGUFULI❓

🔵Na: Shujaa Charles Richard Mwaisemba( ©️®️M )


Kwanza nilazima tukubaliane na tuheshimiane kuwa kila mtu anamitizamo yake, matamanio yake na itikadi zake juu ya yule anayetamani awe Rais wake .Yale unayoweza kuyaona wewe ni mabaya kwako kwa wengine ni mazuri, hivyo jifunze kuheshimu maoni ya wengine hata kama yapo tofauti na wewe kwani Katiba ina mpa uhuru kila mtu kuwa na chama anachokipenda, kuchagua mtu anayempenda bila kupangiwa.

Utofauti wa maoni yetu katika vile tunavyovipenda havihusiani kabisa na maswala ya dini/imani kwamba Usipomchagua lisu au usipomchagua magufuli basi inakufanya ukose mbingu au uwe mbali na Mungu.Ni lazima tufahamu MUNGU HANA CHAGUO LA RAIS WAKE, Kazi ya kuchagua Rais tunayemtaka ipo katika maamuzi yetu sisi ndio tunamtaka mtu wa namna gani ? ,wala Mungu hatatuhukumu kuwa wakosaji tukitofautiana machaguo!!

Pili, Kumekuwepo na makundi mengi ambayo yameanza kujotokeza na mengine yataendelea kijitokeza katika kipindi hichi ambacho kila kundi litatoa sababu zake za msingi kwanini Wanaunga mkono Juhudi za TUNDU LISSU na wengine kwanini wanaunga mkono Juhudi za JOHN POMBE MAGUFULI

Kutakuwapo na makundi mengi ambayo wao watamuunga mkono Magufuli kwasababu waliona amewajengea barabara na Flyover na miundombinu katika vijiji au miji yao, Kutakuwepo na makundi ya wafanyabiashara, wakulima, wafanyakazi nao wataonekana wanaunga mkono Serikali ya magufuli kwa sababu zao mbalimbali za msingi kwasababu wamefanyiwa hivi au vile.Lakini pia kutakuwepo na makundi ambayo yatamuunga mkono Tundu Lissu kwasababu ndio ameonekana ni mtetezi wao wa kuyasemea zile changamoto walizokabiliana nazo kwenye serikali ya magufuli, Wengine watamuunga mkono Tundu Lissu kwasababu wanafahamu alipigwa risasi 16 akiwa kama Mpinzani aliyekuwa anaonekana anaipinga serikali ya magufuli na kutetea wananchi kwa msaada mbalimbali ili wasionewe na kufungwa

Lakini pia kutakuwepo na hata Makundi ya dini au viongozi wa dini ambao nao wataunga mkono juhudi za Magufuli kwasababu tu ameonekana kulinda maslai ya dini na kuonyesha ucha Mungu wake na kuheshimu mambo ya KiMungu.Yaani kila kundi linavutia upande wake kulingana tu maslai ya kundi hilo linanufaikaje na kuwepo kwa Magufuli au Lissu....Makundi yote hayo yanayounga mkono upande wowote yapo sahihi kabisa kwasababu ni kweli maslai yao wanayoyahitaji yameguswa....Lakini JE HAYO MASLAI NDIO HITAJI KUU LA WATANZANIA WOTE?, Jibu ni Hapana kwa herufi kubwa HATUCHAGUI RAIS KWA KUANGALIA MASLAI YETU BINAFSI AU YA KUNDI BINAFSI BALI TUNAANGALIA MASLAI MAPANA YA WANANCHI WOTE

Hivyo ni Muhimu kujua Hatumuhitaji Tundu Lissu eti kwakuwa tunamuonea huruma kwa kuwa alipigwa risasi 16 hata kunusurika kufa, Hilo sio Hitaji la wananchi wote wa Tanzania, Wala hatumchagui Tundu Lissu kwasababu eti ndio mgombea pekee wa upinzani mwenye mvuto na uwezo wa kujenga hoja au kwakuwa aliwai kuwatetea wanachi wengi nchini zaidi ya 400 waliowai kufungwa kwa kesi za kusingiziwa na washinda kesi hizo

Vile vile Hatumchagui Magufuli kwasababu amejenga Flyover, mabarabara, amenunua ndege n.k hayo yote amefanya kama wajibu wake kama Rais kwani hata marais wa awamu zilizopita nao walifanya kwa namna hiyo hiyo.Wala hatumchagui eti kwasababu tu alipokuwa Rais katika majukumu yake aligusa maslai ya kundi letu mojawapo.Pamoja na Ucha Mungu wake alioonesha hasa katika mambo ya kidini/ imani ya kuweza kumtanguliza Mungu hasa katika janga kama la corona ambalo liligusa sana maslai ya Kundi la watu wa dini kwa Mungu, bado hilo sio hitaji kuu la watanzania wa makundi yote wanalolitaka kwanza!!Hivyo pamoja na mengi ambayo tungeweza kuyataja ambayo tunadhani magufuli ameyafanikisha katika awamu yake bado hayo sio Hitaji kuu tunalolitaka watanzania.....



Sasa, HITAJI KUU kwa watanzania wote lipi?Pamoja ya kuwa tuna mahitaji tofauti tofauti katika makundi fulani fulani tuliyo nayo kama kwa wavuvi,wafanyabiashara Viongozi wa dini, wafanyakazi, wanafunzi au taasisi mbalimbali n.k lakini hata tungepata Rais mzuri kiasi gani bado tutajikuta Hatufiki pale tunapopataka.Sasa Hitaji kuu kwa watanzania wote ni MABADILIKO YA MFUMO WA UTAWALA ULIOPO SASA. Nchi yetu ya Tanzania kwa miaka mingi tupo chini ya mfumo mbovu katika maeneno mengi ambao umetokana na kuwa na KATIBA YA ZAMANI ambayo ilikuwa ni ya kipindi ya chama kimoja ambayo inatumika mpaka sasa ambayo INAMPA MAMLAKA KUBWA RAIS KUPITA MIHIMILI YOTE YAANI BUNGE NA MAHAKAMA.Mfumo wa katiba tuliyo nayo sasa haukidhi mahitaji ya wakati wa sasa na kuna mambo mengi yanashindwa kukaa sawa na kushughulikiwa kwasababu ya Mfumo mbovu uliopo ulianzia katika katiba

Ikiwa tutaweka Nguvu katika kubadilisha tu watu katika Chaguzi zetu kila baada ya miaka 5 kabla ya KUBADILISHA MFUMO MZIMA WA NCHI NA WA KIKATIBA, Bado tunakuwa na hatari kubwa sana ya kuiharibu nchi kwa maana Kila Rais atakuja na Dira yake anayojisikia kufanya kwani Katiba haimbani Kufanya yale wanayotaka wala katiba ya sasa haiwezi kumuwajibisha pale anapovunja katiba, hivyo itapelekea ikiwa atakuja Rais kichaa anaweza kuiharibu nchi zaidi kwasababu ya uhuru mkubwa aliyopewa Rais

Hivyo ndio maana Hitaji kuu tunalolitaka kwa sasa ni MABADILIKO YA MFUMO MZIMA ambao utatupatia watanzania kupata KATIBA MPYA ambayo kwa hiyo itakuwa na uwezo wa kumuongoza Rais yeyote hata kama awe mbaya kiasi gani bado Mwongozo huo wa kikatiba ulitokana na maoni ya watanzania wenyewe, utaweza kumfanya hata Rais kuiongoza nchi si kama apendavyo yeye.Lakini hatari iliyo Serikali zote za CCM za awamu zote ndio wamekuwa kipaumbele KUPINGA WANANCHI KUPATA HIYO KATIBA MPYA.Na hii ndio sababu Wananchi wengi wanaojielewa wanaipinga CCM si kwasababu ya magufuli ni mbaya au mzuri ila wanaipinga CCM kwasababu wanataka MABADILIKO YA KIMFUMO KWA KUPATA KATIBA MPYA..


Hivyo mabadiliko hayawezi kupatikana CCM kwani ndio wapinzani wakubwa ,ndio maana watu wapo tayari kuyatafuta Mabadiliko hata kwa UPINZANI.Hii ndio sababu ya watu kuonekana kama ni wapinzani si kwasababu ya TUNDU LISSU bali kwasababu WANATAKA MABADILIKO YA KIMFUMO na mabadiliko kwa sasa yanapatikana UPINZANI na mtu pekee anayeungana na wananchi kuwa tayari kutupatia MABADILIKO HAYO YA KIMFUMO NI TUNDU LISSU

Tukumbuke hatutafuti Rais ambaye ni mtakatifu sana wa kutupeleka Mbinguni, Nu kweli tunatafuta Rais mcha Mungu ambaye bado atamuheshimu na kumtanguliza Mungu lakini bado mwenye uwezo wa KUTULETEA MABADILIKO YA KIMFUMO TUNAYOYATAKA..Na ilivyo ni kwamba Ikiwa tutapambana kumpata Rais atakayeweza kutupatia KATIBA YETU MPYA TUNAYOITAKA bado ikiwa ndio tutachagua Rais awe mcha Mungu basi yote hayo tunayoyataka yatapatikana katika hiyo katiba mpya tutakayoitaka ambayo itamtaka kila Rais ajaye kabla ya kugombea lazima akidhi hivyo vigezo vya ucha Mungu ila kwa sasa TUNAHITAJI RAIS ATAKAYEWEZA KULETA MABADILIKO YA KIMFUMO NA KUPATA KATIBA MPYA. Na Rais huyo bila shaka ni Tundu Lissu...

Tukichagua Rais kwasababu za kidini tu au kiimani tu na kusahau URais ni zaidi ya kuomgoza mambo kidini, bali anapaswa awe uwezo kuwa Kucontrol mambo ya kiuchumi,Kisiasa,kibiashara, kielimu n.k.Yapo maeneo mengi tu ya kumpima Rais tunayemtaka mbali na mambo ya kidini pamoja na umuhimu wake.....Ni maoni yangu...

🔵Na: Shujaa Charles Richard Mwaisemba (©️®️ M)
stmwaisembac@gmail.com
0712054498/0759420202
 
Na ilivyo ni kwamba Ikiwa tutapambana kumpata Rais atakayeweza kutupatia KATIBA YETU MPYA TUNAYOITAKA bado ikiwa ndio tutachagua Rais awe mcha Mungu basi yote hayo tunayoyataka yatapatikana katika hiyo katiba mpya tutakayoitaka ambayo itamtaka kila Rais ajaye kabla ya kugombea lazima akidhi hivyo vigezo vya ucha Mungu ila kwa sasa TUNAHITAJI RAIS ATAKAYEWEZA KULETA MABADILIKO YA KIMFUMO NA KUPATA KATIBA MPYA. Na Rais huyo bila shaka ni Tundu Lissu...
CCM wakisoma hapa miili yao inasisimka mithili ya mpiga tarumbeta aliyepewa embe chachu!
 
Kwa namna Katiba inavyombeba rais sidhani hata lissu akiingia atapenda kuibadilisha ni sisi wananchi tu ndio tunaweza kulazimisha Katiba mpya.
 
Back
Top Bottom