Lipi lilikuwa lengo lao kutushinikiza tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Hivi ni lipi lilikuwa lengo la wazungu kutushinikiza waafrika tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi?

Ikumbukwe hapo kabla walitutawala kwa mabavu na kutufanya watumwa hadi tulipojikomboa kwa mbinde wakatushinikiza tuwe na mfumo wa vyama vingi.
 
Kina nani Mkuu? Mie nimeuliza tu mbona?

Umetoa mawazo, hujauliza swali peke yake.

Umesema wazungu walikushinikizeni vyama vingi .

Basi vifuteni tu. Tujue moja. Mlivifuta 1965, halitakuwa geni.

Malcolm X: Ninaheshimu sana mtu anaenambia anachofikiri kuliko anaekuja na vazi la kondoo ilhali ni shetani mtupu.
 
Mkuu, historia inaeleza hivyo sio Mimi. Mimi maoni yangu ni kwamba vyama vingi ni muhimu kwa watu wanaovikubali kwa thati ya mioyo yao ila experience take afrika imekuwa na changamoto kuliko faida jambo ambalo MTU anaweza kusema ni kama tulivikubali tu ili tuonekane tumekubali ila in real sense hatuko serious.
 
Sina hakika kama tulishinikizwa bali najua kuna vuguvugu lilipita kama lile la miaka ya 50-60 nchi nyingi za africa zilipopata uhuru. Basi ikaja upepo huu wa vyama vingi na sisi hatukuwa nyuma. Inasemekana Nyerere ilibidi akubali japo waliopinga mfumo huo walikuwa ni 80%. Na Nyerere ilibidi apitishe hao wachache kwakuwa alijua kabisa watanzani wengi walikuwa hawajitambui na walitawaliwa na unafiki, hivyo akafanya maamuzi sahihi badala ya kufuata maoni ya wengi.

Sidhani kama ni kweli mfumo wa vyama vingi hauna faida, bali tabia ya viongozi wa kiafrica kuwa na uchu wa madaraka imekuwa ni tatizo kubwa. Kwa bahati mbaya tabia hiyo hata hapa kwetu nayo inazidi kupata kasi. Unakuta mtu hakubaliki analazimisha yeye aendelee kukaa madarakani, ukimuuliza inakuwaje majibu yake eti hawaamini wengine eti watauuza chama/nchi!! Sasa hivi imefikia hata unyama unafanyika kamachomacho ili watu wakae madarakani kinyume cha sheria na kanuni zilizopo.
 
watanzania wengi hawakupenda multpartism...ni busara za Nyerere tu
Sidhani kama ilikuwa busara aisee,naamini kulikuwa na shinikizo fulani.Nyerere angekuwa na busara hiyo asingegombana na swahiba wake Kambona,Bibititi,Kaselabantu et al..
 
Sina hakika kama tulishinikizwa bali najua kuna vuguvugu lilipita kama lile la miaka ya 50-60 nchi nyingi za africa zilipopata uhuru. Basi ikaja upepo huu wa vyama vingi na sisi hatukuwa nyuma. Inasemekana Nyerere ilibidi akubali japo waliopinga mfumo huo walikuwa ni 80%..
Mkuu hill vuguvugu lilikuwa ni vuguvugu gani has a?

Na hakuna mtu aliesema havina faida. Nilichosema ni kwamba experience ya uwepo wake Afrika imeonekana kuleta changamoto zaidi ya faida. Hii maana yake sio kwamba havina faida.
 
Huenda ninakosa neno zuri zaidi ya kuita vuguvugu, kwa mfano kile kilichotokea miaka michache nyuma ya nchi za Africa kaskazini kuondoa viongozi wao kwa njia ya maandamano makubwa. Hiyo ndio hali iliyoleta mfumo wa vyama vingi kwa nchi za africa.

Unaposema unachangamoto zaidi ya faida huenda sijakupati vizuri, badala ya kucheza na lugha sema kinyume cha faida ni hasara na usiite changamoto ili kupooza uhalisia. Tatizo kubwa na sisi waafrika wengi tunaongozwa na uchu wa madaraka. Ukiona mtu anaingia madarakani na akawa hataki kutoka hilo sio tatizo la kushinikizwa kuingia kwenye huo mfumo bali ni walioko kwenye mfumo kukiuka kanuni za mchezo.

Kingine kinachofanya huu mfumo kuleta matatizo barani Africa ni kitendo cha nguvu kubwa kupewa rais kuliko taasisi. Marais wengi wa africa wako juu ya katiba/sheria, hawashitakiwi wala kuchukuliwa hatua zinazowafanya kufuata utawala wa sheria. Hivyo kujikuta wengi kujilimbikizia mali, kutawala huku wakatesa wapinzani wao, hivyo ikifika siku ya kutoka madarkani hawataki maana wanaona wapinzani wao watalipiza walichowafanyia na hata kuwapora mali walizojilimbikizia. Njia nzuri kwa nchi za kiafrika ni kujenga taasisi imara, na hili litawezekana iwapo kitawekwa kifungu cha kumshitaki rais awapo madarakani au awe amestaafu. Kinyume na hapo mfumo wa vyama vingi ndani ya africa ndio utabaki kuwa hiyo uliyoita changamoto kuliko faida.
 
hivi mmezaliwa lini nyinyi watu ?
unajua hata vyama vingi vimekuwepo kabla ya uhuru ?

je wajua kukosolewa na kupingwa kumekuwepo hata wakati wa chama kimoja ?
 
Hivi ni lipi lilikuwa lengo la wazungu kutushinikiza waafrika tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi?

Ikumbukwe hapo kabla walitutawala kwa mabavu na kutufanya watumwa hadi tulipojikomboa kwa mbinde wakatushinikiza tuwe na mfumo wa vyama vingi.
NYERERE HAKUJUA HAYA KAMA YATATOKEA
 
Hata Nyerere alikubali kwa shingo upande-ndo maana ametuachia katiba yenye dosari kibao inayopendelea yule ambae anashika dola na kubana vyama vingine. Kwa mshangao mkuu yeye mwenyewe alisema likatiba hili nikitaka kuwa dikiteta naweza. Sasa tunayaona.
 
Hapana, hapana, nafikiri lengo kuu la wapigania Uhuru wengi hasa wasomi ilikuwa kushika hatamu na siyo kuongoza Africa ifikie maendeleo ya kweli ndo maana kilichofuata baada ya Uhuru ni kutumia nafasi za uongozi kujilimbikizia mali na ndiyo chanzo cha "azimio la arusha" sasa wengi hawakupenda azimio chini kwa chini wakawa wanahujumu juhudi za Mwalimu lkn majukwaani utawasikia "zidumu fikra za mwalimu" baada ya mwalimu kuona hilo alishawishi mfumo wa vyama vyingi lengo nikuruhusu fikra mbala dhidi ya fikra za kushika hatamu
 
Ulichosema ni sahihi, lakini ni kipande tu cha jibu linalotakiwa!

Makosa yako kwetu, lakini pia ni kweli kulikuwa na shinikizo kutoka kwa hao wazungu.

Kwamfano ni sahihi kabisa kusema viongozi wetu Africa “walijilimbikizia mali” mara baada ya kupata uhuru.

Lakini pia ni kweli kwamba wakoloni hawakutaka tupate viongozi watakaoweza kutuletea maendeleo. Kwahiyo walitengeneza mazingira mengi tu ambayo yatatoa changamoto ama kuwa shida zaidi kuongoza.

Mfano wanaona ni rahisi kumjazia kiongozi wa kiafrika mabilioni ya dola kwenye akaunti zake, na vifaa vya kijeshi vya kujilinda, kuliko kulipa pesa stahiki kwenye rasilimali zetu, pesa ambazo zitaweza kusaidia Taifa zima na siyo kiongozi huyo, familia yake, na group lake.

Mambo ya demokrasia ya vyama vingi, wanatusukumia pia kwasababu hiyohiyo, kwamba akitokea kiongozi mwenye kutetea maslahi ya wananchi, yani ambaye atadai dau kubwa kutoka kwenye rasilimali zetu, basi hawatampenda nk. So hapo wataweza kuhonga mmojawapo anayepinga, wakampa maslahi, na yeye akaorganize against serikali.

Mwalimu aliona hayo yote, lakini nadhani hatua alizochukuwa, nyingi hazikuwa sahihi. Kipindi kile mambo yalikuwa magumu zaidi. Kwamfano, Nyerere ndiye raisi ambaye amekoswakoswa kupinduliwa mara nyingi zaidi kuliko marais wote. Hilo lilimpa uoga na kujaribu ku consolidate as much power as possible!

Na kwasababu ni kipindi hicho ambacho uhuru ulikuwa unapatikana kwa mbinde sana, wengine kwa kumwaga damu nyingi, ndiyo maana ilibidi chini ya serikali ya mwalimu, aufute upinzani, kwasababu aliona ni kama wakoloni wanaweza kuwatumia ili kurudi, ama kuwafanya vibaraka wao.

Situation kama hizo bado zinaendelea, ila with a different style! Kwamfano hata mataifa ya waarabu ie Iraki, na hata Libya, kosa lao kubwa ni kuuliza pesa nyingi zitakazowasaidia wananchi na Taifa kwa ujumla kutoka kwenye rasilimali zao. Ndo maana wananchi wa hayo mataifa walikuwa vizuri kimaisha.

Ukitaka kupatana na hayo mataifa wewe kama kiongozi, basi jali maslahi yako binafsi kuliko ya wananchi. Ukitaka kuwa adui, do the opposite.
 
watanzania wengi hawakupenda multpartism...ni busara za Nyerere tu
Siyo kweli kwamba hawakupenda! Kwanza walikuwa brainwashed!

Wananchi kuona mpinzani ni mtu anayeshirikiana na mabepari na wakoloni!

Hakuna mwananchi katika hali ya kawaida, aliyeona ni busara kuipinga serikali ambayo ni ya miafrika mwenzao na siyo ya mzungu/mkoloni.
 
Bado mtu anaweza akajiuliza, kwa mazingira ya Tanzania, hivi mfumo Wa vyama vingi una faida kuliko mfumo Wa chama kimoja?
 
Back
Top Bottom