Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 752
Jana kulikuwa mambo haya:
1.Nape kutaka kuongea na wanahabari.
2.Nape kuzuiwa kuongea na wanahabari.
3.Nape kutishiwa na bastola.
4.Maulidi kitenge kupambana na anaesadaiwa ni askari hata kumshinda.
5.hamorapa kukimbia bastola
6.Nape kufanikiwa kuongea alichodhamiria.
7.Nape kuzuiwa tena na RPC akiwa anatoka.
8.Nape kuonesha kuchukizwa na kutishiwa bastola.
Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyotokea kwenye tukio la jana.lakini cha ajabu nilishangaa kuona watu kwao kubwa ni hamorapa kukimbia..
Nakushangaa uliempa kipaumbele hamorapa kukimbia, ukaacha hata la Kitenge kumsukuma (mnyambafu) ambaye bila Kitenge angeleta fujo zaidi...
Mimi huwa naamini mara nyingi askari wa TZ huwa ni chanzo na kiini cha fujo na vurugu nyingi nchini;badala ya kuleta amani wao huleta ghasia, na hii ni kwa sababu ya kukosa maarifa na kutoangalia mazingira harisi...
Embu fikiria jana askari asingemsumbua Nape, je vurugu zile zingeazishwa na Nape?...
Wanajifanya kuogopa kitu kisichonekana; si wangesubiri waone kwanza ataongea nini...shame on you guys!!!.....
wewe unaongea na mtu kwa simu yupo dar,...wewe upo Arusha then anakuambia piga, wakati huo mazngira hayo wewe unaona kabisa hayaruhusu kupiga.
Askari wetu pamoja na kuagizwa changanyeni na akili zenu pia...
Mfano mzuri ilikuwa ni jana...Maulidi kitenge alichangia sana kuliepusha hili...wewe upo unahangaika na aliekimbia....