Onambali
Member
- Mar 11, 2011
- 67
- 10
Wana JF,
Nawasalimu.
Baada ya kutangaza nia yangu ya kuomba ridhaa ya kuwa rais wa nchi yetu mwaka 2030, nimeulizwa maswali mengi sana mojawapo nilitakiwa nitaje chama changu cha siasa.
Kusema kweli kabisa, mimi bado sijawa mwanachama wa chama chochote cha siasa.
Mheshimiwa rais wa kwanza wa Tz, Dr JK Nyerere, aliwahi kusema kama ukichota maji kwa kikombe kutoka kwenye dimbwi halafu uyafanyia utafiti wa kichambuzi, maji yale yatakuwa sawa na yale yaliyobaki kwenye dimbwi . Kama kauli hii ni ya kweli, basi fananisha viongozi wetu wa siasa na maji ndani ya kikombe yaliyochotwa kutoka kwenye dimbwi (jamii). Ukifananisha hivyo utaona kwamba, tatizo kubwa nchini kwetu ni kukosekana kwa utu, utashi, uzalendo, ubunifu, maono, maadili, ukweli na haki ndani ya jamii nzima. Matokeo yake ni kwamba sampuri (kiongozi) anayetokana na jamii husika huwa na mawazo ya kisanii maana jamii imejitwika usanii katika ngazi zote za kiutawala kuanzia kwa baadhi ya wakuu wa kaya mbalimbali kuwa wasanii hata kwa wenzi wao, watoto wao, nk.
Nina mengi ya kutengenza nchini kwetu. Lazima tujenge jamii inayojitambua, inayojithamini, inayojiamulia, inayojiheshimu, isiyojisanii, inayolinda utaifa wao kuwa urithi wa vizazi vya leo na vile vijavyo, na inayofahamu uhuhimu wa kila raia wake.
Baada ya kusema haya, nafikiri sasa kujiunga au kuanzisha chama cha siasa ili nianze rasmi mbio za kudai uhuru wa kweli wa mtanzania kutoka kwa wakoloni wakuu yaani umaskini wa kufikiri, magonjwa ya kufikiri na ujinga ulioganda vichwani kwa watu bila kujali nyadhifa , shahada walizo nazo hata kama ziwe za heshima au za kusoma, nk.
Naomba ushauri wenu great thinkers, lipi jema, kuanzisha chama cha siasa kipya au kujiunga na chama cha siasa ambacho tayari kimesajiliwa tayari? Kama ukinishauri nijiunge na chama cha siasa naomba pia uniambie kipi na kwanini.
Asanteni sana wana JF.
Onambali, rais mtarajiwa 2030.