Lipi hasa Jukumu la Makamu wa Rais?

Hii post sioni umuhimu wake. Kimsingi raisi wa zanzibar ndiye alitakiwa kuwa makamu wa raisi kama enzi za marehemu karume.

Ingekuwa enzi za mzee wa Standard and Speed.. Angekwambia LOH HILO SWALI JIPYA KABISA , MH. WAZIRI UNAWEZA KULIJIBU AU UKALIACHA!
 
Katiba mpya ilipaswa kuangalia mfumo mpya wa uongoz nchi hii maana mlundikano wa vyeo/wizara kibao lakini utendaji 0
 
Majukumu na nguvu ya makamu wa rais yanatajwa kwenye Ibara ya 47 (1) (a) (b) na(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, ikiwa ni (tafsiri ya kiingereza isiyo rasmi);
(a)kumsaidia raisi katika kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kila siku za muungano,
(b)kutekeleza majukumu yote na kazi aagizwazo na raisi,
(c)kutekeleza majukumu yote na kazi za ofisi ya raisi pindi raisi awapo nje ya ofisi au nje ya nchi.

Lakini imegeuzwa kuwa ni kiongozi mwenye jukumu la kufungua miradi na kupiga kampeni za chini kwa chini za chama chake.

Kifupi makamu wa raisi ameshindwa kuonesha uwajibikaji wake katika nafasi yake...yupo yupo tu!
 
Kwa staili hii,tumefunga ndoa na umaskini,more expenditure than income,loss!
 
Back
Top Bottom