Lionel Messi jela miezi 21 kwa kukwepa kodi

Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kutokana na kukwepa kulipa kodi, vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti.

Baba yake, Jorge Messi, pia amehukumiwa kifungo kwa kukwepa kulipa kodi inayokadiriwa kufikia Euro 4.1 milioni kwa kipindi cha kuanzia 2007 hadi 2009.

Pia, wawili hao watakumbanana na faini ya mamilioni ya Euro kwa kutumia njia za ulipaji wa kodi wa Belize na Uruguay, ambako kuna kiwango cha chini, zilizokuwa na lengo la kujipatia kipato cha haki za picha zake (Messi).

Hata hivyo, Messi mwenye tuzo tano za mchezaji bora wa dunia wa Fifa na baba yake wanaweza kukwepa maisha ya jela.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania, kipengele cha kwenda jela chini ya miaka miwili kinaweza kutumikiwa kwa makubaliano maalumu.
Mshambuliaji huyo wa Barca na baba yake walikutwa na hatia ya makosa matatu katika kodi wakati wa hukumu ya jana katika Mahakama ya Barcelona.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, Lionel Messi alisema kwamba 'hajui chochote' juu ya usimamizi wa fedha zake, akidai kuwa kazi yake ni 'kucheza

Chanzo:Mwananchi online
Hivi wewe umesahau kuwa UKAWA ndio watetezi wa wezi na wakwepa kodi? Kila leo hii wakikamatwa mnaanza kulia kuwa haki za binadamu zimekiukwa tena mna mtuma mama yenu Kibijo simba atoe tamko!
 
Soma hapo kwenye however utaona hilo gazeti la bongo ni la udaku pia pitia the same topic kwenye soccernet.com. Hiyo nime copy and paste from BBC Sport hapa hatutetei mtu kukwepa kodi ila Habari ya huyu jamaa siyo sahihi jamaa hafungwi
 
magufuli go,go...!.kumbe huko nje watu hawana masihara katika suala la ukwepaji kodi hakuna kuangalia ustaa wa mtu.'Taifa corrupt halikusanyi kodi..'.hapa wadau wa soka tunajifunza kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom