Lionel Messi ashinda tuzo ya FIFA Ballon d’Or 2015

Babchabi

JF-Expert Member
Nov 10, 2012
1,745
777
messi-trophy_3546918b.jpg

Wakuu wote na wapenda soka kwa ujumla kwa mara nyengine tena leo tutashuhudia ni nani ataestahiki kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia tuzo ambayo inajulikana kwa jina la ballon d'or tuzo hii hufanyika kila mwaka na hutolewa na chama cha mpira duniani kinacho julikana kwa jina la FIFA katika mwezi wa january .

Hii mada sitaki niirefushe sana japo kuna mengi ya kuyaongea ila wakuu wengine waje hapa kutupatia mawili matatu wachezaji ambao wamesalia katika top 3 kuwania tuzo hii ni kama wafutao .


1. CRISTIAN RONALDO
2. NEYMAR DA SILVA SANTOS JUNIOR
3. LIONEL ANDRES MESSI
Tuwe pamoja ifikapo saa 8:30pm (saa mbili na nusu usiku africa mashariki) kuona ni nani atakae twaa tuzo hii
=======

Messi ashinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya soka ya Barcelona nchini Hispania, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ikiwa mara yake ya tano kushinda tuzo hiyo.

Messi ameshinda kwa kupata asilimia 41.33 ya kura zote na kumuacha kwa mbali mpinzani wake karibu, Christiano Ronaldo aliepata asilimia 27.76 na mchezaji mwenzake wa klabu ya Barcelona, Neymar.

Mwaka 2015 Messi amefunga magoli 52 kwa mechi 61 alizocheza na kusaidia magoli(assists) 27, akishinda magoli kwenye michuano yote sita ambayo timu yake imeshiriki na kushinda mitano.

Washindi 15 wa tuzo hio kwa miaka 15 ya mwisho ni Luis Figo(2000), Michael Owen(2001), Ronaldo(2002), Pavel Nedved(2003), Andriy Shevchenko(2004), Ronaldinho(2005), Fabio Cannavaro(2006), Kaka(2007), Cristiano Ronaldo(2008), Lionel Messi(2009), Lionel Messi(2010), Lionel Messi(2011), Lionel Messi(2012), Cristiano Ronaldo(2013), Cristiano Ronaldo(2014) na Lionel Messi(2015)
 
ha ha ha naweza ku bet hata kwa nyumba yangu,au nitameza panga au Mundu Messi asipochukua mwaka huu!!Ronaldo ni mshiriki tu tena footbal analysts wengi wa ulaya wana criticise hata uwepo wake kwenye hii Tuzo mwaka huu nafasi yake ilitakiwa awepo Suarez au Artulo Vidal
 
Messiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii hutaki kunywa sumu
 
Back
Top Bottom