Lionel Messi aandika rekodi mpya ya dunia ya kufunga magoli mengi kwa mwaka

dah,i see haka katoto ni hatari,nasikia kamezaliwa shinyanga eti
Kuna kitu Messi kafanya muda mfupi uliopita ambacho si kawadia kabisa...karibia afunge goli katika mazingira ambayo hakuna mtu anaweza kutegemea jambo kama hilo...Alikiuwa katikati ya defenders akama 3 na bado kaweza kumiliki mpira na kupiga shuti golini...

Ni bahati mbaya kwamba mpira umegonga mwamba!!
 
Hawa vijana sina hakika kama wametoka kwenye hii dunia yetu!!
Nina uhakika hata kina Pele na Maradona wanawaonea wivu sana kina Messi.

Kiukweli kabisa wao wanalindwa na historia. Hawajaucheza mpira kwa stahili hii. Ni mwenda wazimu peke yake atakayeukosoa mpira unaopigwa na Barca.

Naweza sema hata Mungu ni shabiki wa Barca.
 
Kwani hii iliopo uliitengeneza wewe? Wengine watasajiliwa bana. Kwanza labda uniambie wazeeke, ulishawahi ona timu ina-bid mchezaji wa Barca?

Pale hawaondoki mpaka Barca wenyewe wawaondoe. Ronaldo ndio ushindani umemshinda sasa anataka kutoroka

Hii iliyopo sikuitengeneza mimi na wala hukuitengeneza WEWE alieitengeneza ni Frank Ridjkaard . Pili Man City walimnunua Yaya Toure toka Barcelona

Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
next year,atakuwa anacheza messi na kipa tu,yaani wao wawili tu dhidi ya timu pinzani
 
Kumbuka kuwa Messi kavunja rekodi mbili usiku wa leo. Ya kwanza goli 86 katika kalenda ya mwaka 2012 na ya pili mfungaji muhimu anaeongoza kwenye klabu yake wakati wote akimvuka baba'ke mzazi pedro rodriguez, cesar goli 190 kwa mechi 282yeye goli 192 kwa mechi 218
 
Nina uhakika hata kina Pele na Maradona wanawaonea wivu sana kina Messi.

Kiukweli kabisa wao wanalindwa na historia. Hawajaucheza mpira kwa stahili hii. Ni mwenda wazimu peke yake atakayeukosoa mpira unaopigwa na Barca.

Naweza sema hata Mungu ni shabiki wa Barca.

Wivu wa Pele mbona live mkuu. Alishasema mara nyingi kuwa Messi hana kiwango alichonacho Neymar wa Brazil. Lakini kwa jinsi Messi alivyo nguli, siku Santos ilipocheza na Barcelona kwenye fainali ya klabu bingwa ya dunia, Messi alilamba tuzo mbele ya Neymar, na alifunga goli huku Neymar akikimbiakimbia tu.

Usipompenda Messi basi una uhusiano na ugonjwa wa moyo.
 
Hii iliyopo sikuitengeneza mimi na wala hukuitengeneza WEWE alieitengeneza ni Frank Ridjkaard . Pili Man City walimnunua Yaya Toure toka Barcelona

Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk

Hapo ndio unakosea. Frank Rijkaard kuitengeneza sio nongwa. Kwani tangu ameondoka imekufa? Kina Patrick Kluivert aliokuwa nao bado wapo?

Barca walimuuza Yaya Toure kwa kuwa walipenda kufanya hivyo lakini hakuna mchezaji anayetamani kuhama Barca kwenda kwenye timu inayoishia round ya kwanza kwenye CL
 
Kaka sina shaka kabisa Kama unajua mambo ya mpira lakini ukweli lazing usemwe. Yule Mdachi ndo alieisuka team, hapa Guardiola alisema hvyo, sasa hvi hata wewe ukiwa manager wa Barca ustashinda tu

Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
Kaka sina shaka kabisa Kama unajua mambo ya mpira lakini ukweli lazing usemwe. Yule Mdachi ndo alieisuka team, hapa Guardiola alisema hvyo, sasa hvi hata wewe ukiwa manager wa Barca ustashinda tu

Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk

Usidhani wazungu wana akili kama za Mziray za kuwaponda wenzao au ulitegemea Guardiola ajikweze kwa kusema ''yule haniwezi mimi''? Mimi siwezi kuifundisha Barca labda wewe uliyewahi kuwa coach hapo awali na kufanikiwa kuchukua vikombe na kwa minaajili hiyo uongozi wa Barcelona unapoteza fedha kumlipa Vilanova wakati kumbe ile timu inaweza kufundishwa na mtu yeyote.

Unazungumza kama huyo Rijkaard kaondoka jana. Nikukumbushe kuwa wapo wachezaji wachache wamebakia toka kikosi alichokitumia Rijkaard. Tangu aondoke Henrik Larsson, Juliano Belletti, Deco, Etoo, Marquez, Ludovic Giuly, Toure, Ronaldinho na wengine wengi wameshaondoka na bado Barca inaendelea kushinda na itaendelea kushinda. Kama yapo masalia basi hayazidi 7, mimi nawajua Valdes, Puyol, Xavi na Iniesta. Sasa kukaa kaisuka kaisuka mbona isifumuke kama unadhani makocha waliopo hawafai?

Namkubali sana Ridjkaard, lakini haimaanishi kuwa makocha waliomfuatia hawana kazi.
 
Doh! Sikatai ulisemalo labda niweke hvi" Barcelona miaka yoote inakua na team nzuri" toka Luis Van Gaal, Sir Bobby Robson. Na Barcelona tamu ilikua ya kina Romario na Stoichkov na Van Basten. Haya siku njema acha nitafte ugali wa familia

Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
Doh! Sikatai ulisemalo labda niweke hvi" Barcelona miaka yoote inakua na team nzuri" toka Luis Van Gaal, Sir Bobby Robson. Na Barcelona tamu ilikua ya kina Romario na Stoichkov na Van Basten. Haya siku njema acha nitafte ugali wa familia

Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk

Barcelona tamu kwangu ni hii ya Messi na mguu wake wa hovyo. Unafungwa mpaka wewe mwenyewe unasikia raha
 
Samahanini wanajamvi kuna forums fulani ya nje wanadiscuss kama kuna uhusiano wa dini na kucheza football!

Kuna wanaoshikilia eti dini ina mchango wake ndio maana wachezaji footbal bora wote duniani waliopata kuweka record ni Wakatoliki! Wanaweka orodha ya Maradona, Pele, Ronaldo, Ronaldo Cristian, Messi, Inesta...nk.nk nyie mnalionaje hilo jambo? kuna ukweli wowote au unazi tu wa watu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom