Linux Ubuntu 7.10 (Gutsy) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Linux Ubuntu 7.10 (Gutsy)

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MwanaHaki, Jan 30, 2008.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Jan 30, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Waheshimiwa Wajumbe,

  Nimehamia majuzi kwenye Linux, ninatumia distribution ya Ubuntu, version 7.10 (Gutsy), ambayo inashabihiana na distribution ya Debian.

  Nina mahitaji makuu kama ifuatavyo:

  1) Awali, Windows XP drivers za CDMA Mobile PCMCIA card zilikuwa zinaniwezesha kutumia huduma ya Zantel ku-access Internet nikiwa nyumbani na popote pale ambapo kuna CDMA access, yaani signal. Kwa sasa, sina drivers wala client software ya huduma hii. Device name ni TXD666CDMA. Kama kuna ambaye anajua jinsi hii device inavyoweza kufanya kazi kwenye Linux Ubuntu 7.10 environment, tafadhali anijulishe.

  2) Kuna software inaitwa Skencil, ambayo awali ilikuwa inafanya kazi chini ya Python 2.4. Ubuntu 7.10 ambayo ndiyo latest release imetoa version mpya ya Python, yaani, 2.5.1 ambayo ndiyo latest release. However, Skencil imekuwa fixed ku-run under Python 2.5.1, lakini kwenye process ya kufanya build ili iwe installed, kuna several errors, ambazo zinahusiana na Permission. Kama kuna mjuzi hapa tafadhali tuwasiliane.

  Kwa leo ni hayo tu. Tafadhali naomba tuwasiliane moja kwa moja kupitia email address aziz.mongi@qi.co.tz. Itarahisisha mambo mengi. Au, pia napatikana kwenye MSN Messenger under aziz_mongi@hotmail.com au Yahoo Messenger under aziz_mongi@yahoo.com.

  Asanteni.

  ./mwanahaki
   
 2. C

  Chuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  MwanaHaki naona umejitambulisha hapo chini....OK wapigie simu wa Zantel uwaulize kama wanayo version ya linux...kama hawana fikiria njia ingine...

  Kipya kina matatizo yake...moja ya wapo ni kuwa old zinaweza zisifanye kazi, na hio ndio hofu ya watu wengi wanaogopa kutumia VISTA. baadhi ya program nyingi hazifanyikazi..

  Either uweke double OS...pia jaribu kuingia ktk ubuntu forums..unaweza saidiwa...
   
 3. green29

  green29 JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Intellijentsia Unit inafanya kazi naona.

  I am perplexed.Mwanahaki aka Aziz Mongi tafadhali jibu tuhuma dhidi yako kama zilivyowekwa katika link hiyo.Ukiacha kujibu waungwana watakuwa na bashasha litakalowaruhusu kuchukulia tuhuma zisizojibiwa kuwa huenda zina ukweli.
   
 5. mtuwawatu

  mtuwawatu Senior Member

  #5
  Jan 31, 2008
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
 6. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #6
  Feb 1, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kuhusu shutuma,

  Kwanza kabisa napenda kuwaeleza kwamba mimi ni mtu wa kawaida kabisa. Ninafanya kazi kwa kujiajiri, sijaajiriwa, na ninaridhika na ninachopata. Ni mtu wa kawaida, wala sihesabiki kwenye kundi la matajiri.

  Unapokuwa unamshutumu mtu, unapokuwa una ugomvi na mtu, ni jambo la busara kumtafuta mgomvi wako na kuyamaliza naye. Ni jambo la kawaida kwa watu kushutumiana, kugombana, kutofautiana.

  Lakini si busara 'kuanika' ugomvi wako na mtu mwingine kwenye 'public forum' ambazo zinapatikana kwenye Internet. Unapofanya hivyo unataka nini kitokee? Unataka ueleweke kwamba wewe ni mtu ambaye hawezi kupata suluhu na mgomvi wako, bila kuanika ugomvi wako na yeye kwenye Internet? Basi, nenda kaandike kwenye magazeti, ili ulimwengu mzima ujue kwamba wewe una ugomvi na mtu fulani.

  Kama kuna mtu ana 'matatizo' na mimi, anifuate, tupate suluhu. Kuanza kujibizana kwenye tovuti za Internet si desturi zetu za Kitanzania. Sisi ni watu wastaarabu, tunaojua utu na uungwana.

  Ada ya mja kunena. Muungwana ni vitendo. Mwenye ugomvi nami na aje. Nitamalizana naye, kwa kuzungumza.

  Kwa hiyo, sitajibu shutuma zozote zilizotolewa dhidi yangu, na, kwa kuwa zimetolewa kwenye 'online forum' sitazisoma. Nadhani nimeeleweka.

  ./Mwanahaki

  P.S. Sina sababu ya kujificha wala kumwogopa BINADAM yeyote. Anayepaswa kuogopwa ni Mungu peke yake. (Innalillahi wa Innalillahi Raaj'un!)
   
 7. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..sawa.

  ..kwahiyo,ushapata suluhu ya tatizo lako?

  ..nadhani itabidi ufanye dual boot kama unanuwia kutumia hiyo card au usb modem, inshaallah mpaka pale ndugu zetu wa ubuntu watakapo ona umuhimu wa kufanya vitu hivi vifanye kazi out of the box.

  ..btw,kama pc yako ina wireless,this thing works out of the box.
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  i know this guy in person
  and he is capable kwa tuhuma dhidi yake ni miongoni mwa watanzania wachache ambao wanaichafua sifa ya nchi kwa tricks za kinaijeria.

  mshikaji ana deals kibao na kila kitu ukimuuliza anaweza kufanya ila tatizo utagundua ktk sentensi zake kuna walakini. kwa mfano ukisoma ktk majibu yake hapo juu utagundua kuna ana walakini. haiwezekani mtu aje umalizane naye huku umebadilisha contacts zako na you are no where to be found.

  paragraph hapo juu ameanza vizuri lakini angalia alivyoharibu mwishoni, hivyo nazidi kukandamiza kibara kwamba jamaa ana walakini. Ninamfahamu jamaa huyu. he can do any fishy to earn his life....

  Ninaomba aingizwe ktk chumba cha mahojiano angalau tujihakikishie kuwa amejirekebisha (samaki aliye kauka hukunjika?). achunguzwe huyu...
   
 9. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..umefanikiwa?

  ..there's a solution,that's why nime-delete ile post yangu [research and trials zimesaidia]

  ..talkback,will'ya?
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kaaaz kweli,
  mambo ya february haya
   
 11. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..kaazi kweli,kama deal ni kusanifu watu na si kuwasaidia!
   
Loading...