Lini zitaanza kutolewa ajira Milioni 8 zilizoahidiwa na ilani ya CCM 2020?

DUMU

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
431
577
Ndugu zangu msione katika thread zangu natabasamu na kucheka lakini behind the pillow ni muhanga wa ajira. Iliani ya CCM ilisema miaka mitano iliyomalizika imetoa ajira 5m lakini hizi ajira nimekuwa nikipishana nazo yaani sijui zilikuwa zinapita njia ipi na mimi nilikuwa na pita njia ipi.

Sasa mwaka wa kwanza wa kiuongozi wa awamu ya sita imeanza; hivi hizi ajira 8m zimeanza kutoka ama bado na kama bado zitatoka lini. Nikae njia gani ili nizikamate kisawasawa japo moja tu hata itakuwa ya muda mfupi ilimradi niondoe japo nuksi ya kutoajiriwa katika maisha yangu.

Nahisi kukata tamaa ya kimaisha japo naonekana nipo ngangari ila nimesurrender huu mziki wa kukosa ajira uwe unausikia tu kwa jamaa zako.

Nimeoa mke na ninamtoto mmoja ila aaah wacha we huu mziki wa kukosa kipato cha uhakika kinanitesa.

Inafikia hatua nahisi kukosa ajira ni ulemavu wa kiakili ila sijaacha kupambana siunajua uwe na mke halafu maisha yaende hovyo mbona mapenzi nayo yanakuwa zigo lisilo simulika.

Ndugu zangu nipeni maujanja mlitumia njia gani kupata ajira ya kudumu.

Chonde chonde wandugu hizi ajira 8m zikianza kutoka mnisaidie kuzipata.
 
Nimekuelewa. Ajira ni janga la taifa. Hata hao walioajiriwa wanalilia mshahara. LAKINI endelea kupambana na maisha Mungu anaweza kukufungulia njia ukajiajiri na kujipatia kipato cha kukusogezea siku. Maadam ulizikosa zile 5m si ajabu kukosa hata hizo 8m kama zitakuwepo. Usibweteke ukazisubiriiiii weeeeee utakuta mwana si wako!
Usikate tamaa... fikiria na pambanana!
 
Nimekuelewa. Ajira ni janga la taifa. Hata hao walioajiriwa wanalilia mshahara. LAKINI endelea kupambana na maisha Mungu anaweza kukufungulia njia ukajiajiri na kujipatia kipato cha kukusogezea siku. Maadam ulizikosa zile 5m si ajabu kukosa hata hizo 8m kama zitakuwepo. Usibweteke ukazisubiriiiii weeeeee utakuta mwana si wako!
Usikate tamaa... fikiria na pambanana!
Sawa mkuu
 
Ajira hizo haimaanishi kuwa zitatolewa na serekali Bali
Serekali utaweka mazingira kwa ajili ya sector binafsi kuweza kutengeneza ajira hizo kwa watanzania

Kumbuka kuwa Tanzania na dunia kwa ujumla muajiri mkuu na anaetoa ajira ni sector binafsi na sio serekali
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom