Lini watanzania watajua kura yao ni lulu

drphone

JF-Expert Member
Sep 29, 2009
3,542
281
wakuu heshima mbele
kuna jambo linanitatiza nalo ni jinsi watu wengi wasivyojua thamani ya kura yao kiasi kwamba anaweza kuiuza kwa pilau, tshert,kanga, kofia buku, 5000, na 10,000.
chakushangaza ni kwamba wagombea wanajua kwamba kura ni lulu na ndio yenye uwezo wa kuwaingiza kwenye mdaraka na ukubwa wakisha pata tu anajisahau akiamini baada ya 5 yrs mchezo ni ule ule pesa.

jamani tufanye nn\ nn kifanyike watu wajue umuhimu wa kura zao waache kuziuza kirahisi na kuburuzwa kwa miaka 5
 
Kibaya zaidi hata wasomi wetu waliopo vyuoni wamekaa kimya tu, wamepoteza haki yao ya msingi ya kupiga kura bila sababu ya msingi na wao wamekaa kimya,.

namaanisha kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi walijiandikisha kupiga kura wakiwa vyuoni,..na inamaanisha kua vituo vyao vya kupigia kura ni vyuoni mwao.. serikali ikaja na tamko kua vyuo vyote vifunguliwe novemba hii ina maana baada uchaguzi mkuu... sasa swali hawa raia watapataje fursa ya kupiga kura ?
 
yani cjui ni lini wadanganyika wataamka kutoka usingizi mzito walo lala unaowapa wanasiasa nguvu yakufanya wanayotaka bila kupingwa yani utasikia ahadi kedekede kweli akuna wasomi nchi hii
 
nashangaa watu wanao jazana na kushangilia kwenye mikutano ya kampeni ni kweli awaoni yanayotendeka baada ya kuwapa kura waheshimiwa
 
Wa Tz wamebadilika kifikra zaidi ktk uchaguzi wa mwaka huu na biashara ya kuuza na kununua kura kwa t-shirts,kanga na kofia mwaka huu hakuna na tutaraji makubwa kwenye viti vya ubunge na udiwani zaidi ya yote kura za muungwana zitashuka sana.
 
mkuu nakubaliana nawe lakini watu kama wamelogwa na ccm
 
tusiwadharau watanzania, mimi naamini kabisa mwaka huu mabadiliko yanawezekana, tusiwaaminishe ccm kwamba watanzania
bado wamelala, si kweli kabisa, wasije wakiba kura na sisi tukaamini kweli wameshinda maana tumelala, si kweli, aliyetoa hoja
hii achunguzwe isije kuwa anataka kujustfy wizi wa kura, kinachowasaidia ccm ni wizi wa kura na si kwamba tumelala.....
 
Back
Top Bottom