Lini wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii watanufaika na uwekezaji wa mifuko hiyo?

mdhalendo

JF-Expert Member
Dec 14, 2011
282
273
Mifuko ya Hifadhi za Jamii kama NSSF inafanya uwekezaji mkubwa sana kwa kutumia michango ya wanachama. Miradi hiyo ya matrillioni ya Shillingi inajumuisha uwekezaji kwenye mabenki, kilimo na majengo makubwa ya kibiashara (Real estate), madaraja ya kulipia pamoja na uuzaji wa nyumba.

Je, wenye Mamlaka hawaoni kama ni busara sasa kwa wanachama wa mifuko hii kunufaika na michango yao kwa kupata GAWIO la angalau 10% ya faida inayotokana na miradi hii?

Kama mifuko inanufaika na ukwasi wa michango yetu, ni vibaya na sisi wanachama tukanufaika na faida ya uwekezaji huo? Karibu tutafakari pamoja.
 
Faida tunaipata tukistaafu. Mifuko hii inakupatia mshahara wa kila mwezi Hadi ufe huku hufanyi kazi.
 
Faida tunaipata tukistaafu. Mifuko hii inakupatia mshahara wa kila mwezi Hadi ufe huku hufanyi kazi.
Unalipwa mshahara au wanakurudishia ulichowapa bila riba na wao wanakurudishia kidogokidogo ?
 
wapo wanaonufaika sio moja kwa moja (indirectly)

Mfano
1. Wachangiaji ambao watoto wao wako kwenye vyuo vilivyojengwa kwa rasilimali za mifuko hiyo
2. Wachngiaji ambao wanatumia miundombinu mfano barabara zimeboreshwa kwa rasilimali za mifuko hiyo
3. Baadhi wamepangishiwa katika majengo kiofisi/malazi ambayo yamejengwa kwa rasilimali za mifuko hiyo

sasa issue ipo endapo ulitaka ufaidike moja kwa moja (direct) gawio la uwekezaji, ngoja wataalamu watakuja kukujibu
 
Sikuwahi kujua kuwa shareholder mkubwa wa bank ya Azania ni mfuko wa hifadhi ya jamii

Je hii ni kweli?

Kwanini wanatoza riba kubwa sana kupita kawaida?

Mbona ilipaswa kuwa kinyume?
 
Back
Top Bottom