Lini Wa Tanzania Wataachana Na Dhana Ya Kuadhibu Vibaka Wadogo?

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
Kila kukicha utasikia wananchi wenyehasira wamempiga/wapiga au hata kuwachoma Moto vibaka waliokuwa katika jaribio la kuiba/ au walioiba vitu kama simu, kuku n.k. vitu ambavyo hata katika sheria za Nchi yetu kifungo chake hakizidi miaka 2.Lakini hawa wanaoiba mali ambazo kifungo chake kinaweza kuwa cha maisha au hata kunyongwa hadi kufa wanaendelea kula pipi mtaani

Kinachoshangaza ni kwa hawa vibaka (Mapapa wakubwa) na huenda wasiwe tena mapapa bali Nyangumi kama kina EL, Karamagi, Rostam Aziz, Mkapa, Mramba n.k ambao uhalifu wao unagharimu maisha ya watanzania zaidi ya milioni moja kwa kwaka. Kwani kuna kina mama waja wazito na watoto wachanga wanaokufa kwenye vituo vya afya kwa kukosa huduma bora za afya. Ajali za barabarani kwa ubovu wa miundombinu

Kama kweli watanzania wanaweza kuwashughulikia vibaka wadogo wanaowasababishia kero ndogondogo katika maisha yao na kushindwa kuwashughulikia hwa vibaka wakubwa wanaohatarisha maisha ya jamii nzima ya Tanzania ni swali niliulizalo bila kupata jibu sahii. Hivi sisi watanzania tumeroga na nani?
Sitaki kuamini kuwa hatujui haki zetu za msingi ila tu tumekuwa waoga kwa hawa vibaka wakubwa na kusema eehwala Mungu atatulipia.

Ukifuatilia hali halisi ya siasa za nyumbani kama ingekuwa Nchi za wenzetu katika kikao cha maandili ya CCM kilichofanyika jana waandamanaji kutoka kila kona ya Tanzania wangeweka kambi Dodoma kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa kushinikiza kujiudhuru kwa Lowasa, Karamagi, Msabah, Rostam ,Hosea Mwanyika na wengineo. Lakini kwa watanzania kila mtu amekaa akisubiria uamuzi wa chama katika masuala yasiyo ya kichama.
Maana suala la ufisadi hatuwezi kulichukulia kama la chama bali ni suala linalaomgusa kila mtanzani mwenye itikadi tofauti.
Kinachotia uchungu zaidi ni watendaji wakuu katika masuala ya rushwa na Sheria Hosea na mwanyika nao wanahusishwa na sakata hili sasa nani atamfunga paka kengele?
Naomba kutoa hoja wana JF maana keyboard inalowa kwa machozi
 
Kibaka anayekwapua shilingi mia hupewa kipigo cha mbwa barabarani. Libaka linalokwapua mabilioni ya fedha za wananchi linapishwa na kila mtu linapopita barabarani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom