Lini viongozi wetu watakuwa na majibu ya kiofisi? Na sio maoni yao binafsi

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
867
219
DPP amkana Hoseah

ASEMA HAJAPATA JALADA LA CHENGE,
AAMBIWA AKAANGALIE MASJAJA


SIKU moja baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, kusema kwamba ofisi yake imekamilisha uchunguzi wa madai ya kumiliki Dola za Marekani 1.2 milioni katika Kisiwa cha Jersey, Uingereza yanayomkabili Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge na kwamba imekabidhi faili lake kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kumfungulia mashtaka, kiongozi wake, Eliezer Feleshi amejitokeza na kusema kwamba hawahi kuliona jalada hilo.

"Niko safarini subiri hadi wiki ijayo
…
kwanza ashtakiwe kwa kosa gani? Acheni siasa nyie," alisema DPP alipotakiwa kuthibitisha kama jalada
hilo limefika mezani kwake na lini Mwanasheria huyo Mkuu wa zamani wa Serikali atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili... "Aseme ni tarehe gani alileta jalada hilo kwangu?"

Kutokana na majibu hayo ya DPP,
Mwananchi lilimtafuta Dk Hoseah kupata ukweli juu ya kauli yake hiyo aliyoitoa juzi huko Arusha na kusisitiza kuwa jalada hilo limepelekwa katika Ofisi ya DPP na kumtaka mkuu huyo wa Mashitaka nchini asiharakishe kusema hajaliona, kwani siyo lazima kila kitu akabidhiwe mikononi... "Kwani kila kitu kinachopelekwa kwake lazima akione? Ameangalia registry (masjala)?. Suala hili nimeshaliongea nanyi vya kutosha hivyo muulizeni zaidi DPP."

Juzi, Dk Hoseah alisema taasisi yake imekamilisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Chenge na kwamba jalada lake limepelekwa kwa DPP kwa hatua zaidi. Alisema Chenge atashtakiwa chini ya Kifungu cha 27 cha Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007. Kwa mujibu wa kifungu hicho, mtu akiwa na mali ambazo hazilingani na kipato chake alichokipata akiwa madarakani au baada ya kuondoka ni kosa kisheria.

Chenge anadaiwa kukutwa na kiasi hicho cha fedha mwaka 2008 baada ya uchunguzi wa kashfa ya ununuzi wa rada uliofanywa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO). Tuhuma hizo ndizo zilizomfanya alazimike kujiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu mwaka huo.

Malumbano kati ya Dk Hoseah na Feleshi siyo ya kwanza. Mwaka jana waliwahi kulumbana baada ya mkuu huyo wa Takukuru kusema kuna majalada takriban 50 ya kesi za rushwa ambayo yamekaliwa na DPP.

Pia Dk Hoseah aliwahi kumshutumu DPP mbele ya wabunge wakati wa semina elekezi mapema mwaka huu akidai kwamba amekuwa kikwazo cha kesi kubwa za ufisadi kupelekwa mahakamani kwa kukwamisha majalada.

MAONI:
Kwa mtendaji kama DPP ambaye ana negative attitude ya kitu ambacho haya kiona/kifanyia kazi anaweza ku;itendea haki TAIFA?
wakina nani waache siasa? watanzania au wanaTAKA KUJUA UNDANI WA RADA?
ingekuwa nchi inayoeleweka hii kauli ingemng'a au kuondoa uhalali wa yeye kushiriki katika suhali ili maana baada ya kutoa kauli hiyo maana huo ndio msimamo wake wa ndani ya kwamba ana amini chenge hakufanya kosa
nchi hii inakwamishwa na chuki miongoni mwa watendaji wa serikali na kujuana
 
Back
Top Bottom