Lini uchaguzi wa diwani kata ya mianzini, kigamboni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lini uchaguzi wa diwani kata ya mianzini, kigamboni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima wa Kuku, Oct 6, 2012.

 1. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Wiki kadhaa sasa wananchi wa jimbo la Kigamboni wamekuwa wakilalamikia utendaji wa mbunge wao kwenye forum hii na mimi nilisema kuna kata moja ya mianzini ambayo inakuwa kama haina Mbunge, M/Kiti wa serikali za mitaa wala mtendaji wake kwa jinsi ambavyo mambo yanaenda mzobemzobe. Nilitahadharisha kuwa mtaanza kuwaona uchaguzi wa kujaza nafasi ya Diwani michakato yake itakapoanza. Juzi na jana walipeleka grader kwenda kuchimbua barabara. Cha kushangaza ni kuwa sehemu walizochimba ndiyo kama mkondo wa maji na hatuna hakika kama wananchi wa eneo hilo watakuwa na barabara mvua kidogo tu itakaponyesha. Ikumbukwe kuwa Kilwa Road inajengwa kwa upya na kuna kifusi cha kutosha kwa ajili ya ameneo yote korofi lakini nasikia mtendaji analalama kuwa hawana fedha za kununua kifusi hicho/kusafirisha kifusi hicho. Tutaendelea kuwajuza juu ya ushindi au kushindwa kwa viongozi wa Kata ya Mianzini kurekebisha barabara zake wakisaidiana na Mbunge.
  Au uchaguzi wa Diwani umeshakaribia nini?
   
Loading...