Lini tutasikia tamko la JWTZ kuhusu mgogoro wa Malawi na Tanzania?

Status
Not open for further replies.
kwa nini Shimbo asijitokeze sasa na kutuliza wananchi kwamba mipaka yetu ipo salama?acha uwoga wa vita.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Nimeelezea kwa nini hapo ju, hujaja na swali jipya lenye leseni ya kupewa jibu jipya.

Kuhusu uoga, naambiwa ni dalili ya werevu. Soma wahenga na watu waliopigana vita wanavyosema. Mtu anayeijua vita hawezi kutaka vita kirahisi rahisi wakati njia nyingine za kidiplomasia hazijamalizwa kwanza.

"Kwa mwoga huenda kicheko, kwa shujaa huenda kilio" -Methali ya Kiswahili.

"If we take the generally accepted definition of bravery as a quality which knows no fear, I have never seen a brave man. All men are frightened. The more intelligent they are, the more they are frightened."
General George S. Patton
 
Uchaguzi ni suala internal, sababu ya shimbo kutokeza wakati ule ilikuwa hasa ninini wakati yeye ni mtu wa kulinda mipaka?
Sasa hv jambo linalowahusu lipo, wao wanasemewa na wanasiasa wakiacha Lowassa akipata nafasi nyingine ya kuuza sura kwenye media zetu.
Ni mambo ya ajabu sn haya!
 
Nimemsikia Lowasa tbc anasema amehakikishiwa na jeshi kwamba wapo makini na wamejiandaa vya kutosha kulinda mipaka yetu.
Lowasa kahakikishiwa na jeshi kama nani?kuwa mwkt wa kamati ya ulinzi na usalama ya Bunge sidhani kama kunampa mamlaka ya kuwasiliana na jeshi moja kwa moja. Au 'friend' keshachoka hivyo kamkaimisha Uamiri jeshi? Maana hawajakutana mtaani.
 
Hivi kelele zote hizi za wamalawi hazina mkono wa mtu nyuma yao? yaani hao jamaa wanaotafuta mafuta haiwezekani kuwa ndio wanaowapa kichwa wamalawi?
 
wanajeshi hawatoi tamko. Jeshi linapewa amri na wanatekeleza. Mfano wakiamriwa wakawaue wanachadema lazima watekeleze amri. Wakiamriwa kuingiza powertillers nchini inatekelezwa

Labda mtoa amri hana taarifa kwamba nchi imevamiwa, wamalawi wamejitwalia sehemu yetu ya ziwa nyasa.
 
anachojaribu kutuelimisha jingalao ni kuwa tusipende kuiacha siasa itawale kwenye masuala ya msingi.ona tunavyoaibika sasa.
 
Bila shaka JWTZ wanapaswa kujitokeza hadharani kuwahakikishia usalama wa mipka ya nchi hasa huko ziwa nyasa.
Kwa hali hii ambapo hata waziri wa ulinzi hajatembelea eneo lenye chokochoko na hajatoa tamko lolote kuwahakikishia ulinzi ni lazima wananchi wawe na wasiwasi wa mipaka ya nchi na usalama wa nchi.

Hizi busara za vikao vya mbege chini ya migomba.
 
Uchaguzi ni suala internal, sababu ya shimbo kutokeza wakati ule ilikuwa hasa ninini wakati yeye ni mtu wa kulinda mipaka?
Sasa hv jambo linalowahusu lipo, wao wanasemewa na wanasiasa wakiacha Lowassa akipata nafasi nyingine ya kuuza sura kwenye media zetu.
Ni mambo ya ajabu sn haya!


Hata tukisema kwamba Shimbo alikosea kusema vile - for the sake of argument- hilo halina maana kwamba jeshi kutoa tamko sasa hivi wakati mazungumzo ya kidiplomasia yanaendelea litakuwa ni jambo zuri kwa sababu zilizotajwa hapo juu.

Watu wanashabikia vita sana kiasi kwamba kitendo cha jeshi kutoa tamko kitaanzisha vita ya maneno, Wamalawi nao watataka jeshi lao litoe tamko, mwisho mtu atateleza ulimi aseme kisichotakiwa nchi moja itatukanwa na hali itafikia "point of no return" vita inapigwa kirahisi tu.

Hatujafikia stage ya wanajeshi kuingilia hili suala, kama nilivyosema mwanzo, wanajeshi ni watu wa kufanya mambo zaidi kuliko kusema.

Mkitaka kuanza kuwafanya wanajeshi waanze kusema sema wengine hawajui hata kusema watatoa maneno ya ku escalate mgogoro buree kwa munkari hali iwe mbaya zaidi.
 
kwa hivyo SHIMBO alichemka kutoa tamko wakati wa uchaguzi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Ndiyo, Shimbo alichemka. Na yule naibu mkurugenzi wa usalama wa taifa naye alichemka kufanya press conference kusuta madai ya Chadema. Usalama wa taifa daima wako nyuma ya pazia. Si kazi yao kuja mbele ya waandishi wa habari, kupigwa picha na kukanusha chochote kile. Lakini hapo ndipo alipotufikisha Kikwete na utawala wake wa kiswahiba.
 
Lowasa kahakikishiwa na jeshi kama nani?kuwa mwkt wa kamati ya ulinzi na usalama ya Bunge sidhani kama kunampa mamlaka ya kuwasiliana na jeshi moja kwa moja. Au 'friend' keshachoka hivyo kamkaimisha Uamiri jeshi? Maana hawajakutana mtaani.

mkuu hata mimi nimeshangaa,nafikiri hili swala kuna baadhi ya wanasiasa wemeona ni sehemu sahihi ya kupandia chati kwa wananchi.!
 
Hivi kelele zote hizi za wamalawi hazina mkono wa mtu nyuma yao? yaani hao jamaa wanaotafuta mafuta haiwezekani kuwa ndio wanaowapa kichwa wamalawi?

Nilikuwa nasoma kwenye mtandao mmoja wa wamalawi, baadhi wanajinasibu kwamba wako tayari kwa vita dhidi ya Tanzania kwakuwa wana support ya US na UK.
Na ukizingatia makampuni yanayofanya utafiti ziwani humo ni ya kiingereza na waziri Clinton wa US ametembelea malawi, huenda kuna ukweli mkubwa katika majigambo ya wanyasa.
 
mods nashukuru kwa kulegeza ukali wa title ya thread,lakini ni vyema ukatuacha tuwabane watawala kwani wamezoea kamchezo cha kutuhadaa.nataka nimsikie Shimbo.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Wanajeshi hawawezi kuanza kutoa matamko tamko tu wakati jitihada za kidiplomasia zinaendelea. Hilo litakuwa jeshi la kitoto.

Subiri diplomasia ichukue mkondo wake kwanza. Wanajeshi wakianza kusema sasa wanaweza hata kuharibu mazungumzo.

Halafu watu wanaoshabikia vita ndio hao hao hata wakiona mjusi tu wanakimbia.
Diplomasia gani kaka!!? serikali iseme tu ukweli kuwa kwa sasa magari mengi ya jeshi ni mabovu na hawaja service muda mrefu, wanatumia kivuli cha diplomasia kukarabati miundombinu ya kivita yakiwemo magari, tyre ,na vifaru.
 
anachojaribu kutuelimisha jingalao ni kuwa tusipende kuiacha siasa itawale kwenye masuala ya msingi.ona tunavyoaibika sasa.

Actually hapa kama mtu anataka kufanya siasa analiingiza jeshi, kwa sababu ndilo jambo linaloonekana kupendwa na wananchi wengi -angalau kwa hapa JF tu-

Cooler heads need to prevail.

Bado uchumi wetu unaugulia vita vya Idi Amin mpaka leo. But in that case the war was justified kwa sababu Amin alishafikia point of no return.

Kwenye hili la Malawi hatujafikia hiyo point bado.
 
Diplomasia gani kaka!!? serikali iseme tu ukweli kuwa kwa sasa magari mengi ya jeshi ni mabovu na hawaja serice muda mrefu, wanatumia kivuli cha diplomasia kukarabati miundombinu ya kivita yakiwemo magari, tyre ,na vifaru.

Sasa kama magari mabovu mnataka jeshi liende kusema nini?

Magari yetu mabovu hatuwezi vita?
 
wanajeshi hawatoi tamko. Jeshi linapewa amri na wanatekeleza. Mfano wakiamriwa wakawaue wanachadema lazima watekeleze amri. Wakiamriwa kuingiza powertillers nchini inatekelezwa
Na inawezekana wakapewa amri ya kutoa tamko! Nakumbuka waliwahi kuamriwa kufungua kampuni ya biashara ya madini (MEREMETA) na wao wakafanya kweli! Tatizo ni kuwa mtoa amri huyu wa kwetu ana hiari... aweza kukana kutoa amri mambo yakiharibika.
 
nadhani ungesoma na ungeelewa comments za kiranga usingeendelea kuuliza uliza...,

na kwa kuongezea,, mamlaka za usalama wa raia(ulinzi wa ndani) ziliomba kwa amiri jeshi mkuu nguvu ya jeshi iongezwe kipindi cha uchaguzi.., sasa jeshi likatoa tamko(baada ya kuamriwa kuongeza nguvu kipindi cha uchaguzi)...,

sasa, kwa case hii ya sasa, hawawezi kutoa tamko kwa sbb bado hawajapewa hiyo mandate na amiri jeshi mkuu, jeshi lina kitu kinaitwa chain of command, ndio maana msemaje wa jeshi, tanzania nzima ni mmoja tu

Pia kuna vitu vinaitwa war(hostility) indicators..., mojawapo ni matamko unayoyataka ww..., tanzania haiwezi kuwa upande wa aggressors(waanzilishi) wa vita maana siku hizi mapesa ya kufidia kuvamia nchi ya watu ni staggering,,, diplomacy ikishindwa case inapelekwa security council, membe atatea hoja na kutoa ushahidi kwamba malawi amevamia maeneo ya tz na tunataka atoke otherwise mtutu wa bunduki.., asipotoka, security council itapiga kura, na kibali kikitoka tunaingia front..,

Usione watu wapo kimya, jeshi lina watu wasomi sana na wenye weledi.., hawatoi matamko ovyo,

Wewe kua na amani, watu wamejipanga vizuri sana na bahati 'mbaya' kama diplomacy itashindwa, trust me, lilongwe will fall in a month.., bendera za tz zitapepea blantyre, mzuzu, etc
 
Actually hapa kama mtu anataka kufanya siasa analiingiza jeshi, kwa sababu ndilo jambo linaloonekana kupendwa na wananchi wengi -angalau kwa hapa JF tu-

Cooler heads need to prevail.

Bado uchumi wetu unaugulia vita vya Idi Amin mpaka leo. But in that case the war was justified kwa sababu Amin alishafikia point of no return.

Kwenye hili la Malawi hatujafikia hiyo point bado.
naamini tunalitengea jeshi letu tunalitengea fedha za kutosha na liko tayari kwa lolote mda wowote.jeshi halitakiwi kuamini katika diplomacy(hiyo ni notion ya politicians)
Mbona nasikia majeshi ya malawi yanavinjari Nyasa?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Hizi busara za vikao vya mbege chini ya migomba.

Mbege ni kinywaji cha heshima we *****. Sasa wewe unayekunywa mataputapu unaona unavyo mbwelambwela hapa! Bila shaka wewe ni manusura wa ile dhoruba ya mburahati wiki mbili zilizopita. Bado akili yako haijarudi mahali pake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom