Lini tutakuwa na state documents

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Wadau habari ya mdahuu.

naenda kwenya mada moja kwa moja. Tanzania imekuwa nchi ya ajabu sana hali hii ya kuutumia akili ya mtu moja bila kuwa na state document itakayolindwa na vyombo vya ulinzi na usalama bila bila kujali nani anaingia ikulu itakoma lini?

Maana tunashuhudia vimbwanga vingi mno mengine hata yanakiuka katiba ya nchi kiukweli hali hii mbele ya safari itatupoteza kabisa badala ya kufuata katiba ya nchi tutakuwa tunafuata akili ya mtu moja lakini tungekuwa na state document angelazimishwa na vyombo vya usalama na ulinzi wa nchi kuwa kushinda uchaguzi ni jambo moja na wakati ukiwa state house kuna namna inakupasa kufanya tofauti na ahadi zako

Mimi nikijaribu kuwaza kuhusu yanayotendeka nchini naona mbeleni tutakumbana na mkwamo mkubwa sana hapa simlaumu mtu yeyote kwa kuwa hatukuwa na kitu kama hicho ikulu unamlaumu nani.

Kuna watu wanaitwa spine doctors watu wa kufikiri kwa niaba ya nchi na mawazo yao ndo yanayofuatwa na ndiyo dira ya nchi. Hili ni kundi muhimu sana ambalo halifungamani na chama chochote cha siasa. Wao chama chao ni nchi kwanza ndo maana kwa wenzetu kuna assassination ya rais maana yake umezingua, umeenda kinyume na state document.

Document hiyo ina kila kitu kuanzia imani ya nchi kwa maana ya mfumo wa siasa mfano communism, capitalist nakadhalika na juu yake inajengwa kanuni za kufikia a good end ikiwa iko tested theoreticaly and practicaly. ili kila moja anayegombea ajue kwa nje nchi inafuata siasa ipi na ukifanikiwa kuukwa ukuu wa nchi unaenda kusimamia nini.

Wanajamvi ebu tujadiliane ili kama kuna watengeneza sera wa serikali humu waeze kuchukua point kadhaa.

Karibuni kwa mjadala
 
''state document itakayolindwa na vyombo vya ulinzi na usalama'' ni mdudu gani?

Hii nchi nadhani ujinga unaongezeka lakini kibaya zaidi wajinga hawajijui kama ni wajinga!
 
Kuna mambo katika nchi huwezi kwenda behond that lakini hapa kwetu sio katiba sio nini kwa jinsi tulivyoshuhudia awamu hii tuna katiba mbovu sana ambayo inampa rais anavyotaka na hafungwi kufanya anayowaza ni hatari sana
 
State document ni kitu muhimu sana kwa nchi. Inampa kiongozi policy na procedure muhimu za kufuata kufanikisha maendeleo, Haki na Matumizi mazuri ya siasa.
 
Maoni yako haya yamedhihirisha nilichokiandika kuwa kuna wajinga lakini hawajui kama ni wajinga!
wewe una matatizo makubwa ya kufikiri kuniambia mimi mjinga haihalalishi ujinga wangu huenda indhirihirisha ujinga wa kwako maana nimefafanua vizuri kwa kifupi na maneno ya kueleweka na ninavokuona wewe uko empty kabisa hata hujawahi sikia kitu kama hicho ingawa uko uko sehemu nyeti sana
 
State document ni kitu muhimu sana kwa nchi. Inampa kiongozi policy na procedure muhimu za kufuata kufanikisha maendeleo, Haki na Matumizi mazuri ya siasa.
hapo kwenye matumizi mazuri ya siasa ndo imesababisha matatizo makubwa hapa kwetu
 
mwalimu nyerere aliwahi sema siasa safi ni msingi wa maendeleo hapa kwetu kwa sasa inafanywa siasa chafu isiyounganisha watu tunapataje maendeleo?
 
Nadhani inaitwa ilani ya uchaguzi, hiyo ndio agenda ya serikari yoyote inayochukua madaraka

Vyombo vya ulinzi na usalama havina mandate ya kuendesha nchi kwenye siasa za uchaguzi, serikari iliyochaguliwa ndio yenye jukumu hilo.

Kupitia raisi na baraza la mawaziri wao ndio wanaamua dira ya nchi sio vyombo vya usalama.

Jukumu la vyombo vya ulinzi ni usalama wa nchi, the intelligence part ni kushauri hatua za serikari kuchukua ambazo viongozi wenye mandate wanaweza kufuata au kukataa huo ndio utaratibu wa serikari duniani.

Kwenye dunia ya kwanza vyombo vya ulinzi wana mbinu zingine za ku influence serikari kwenda kwa mtindo wao either kupitia ushauri wa kitaalamu wenye ushahidi au pressure tactic za media, pressure groups and swaying public opinion; mara nyingi wanafanikiwa hila sio zote.

Ndio maana huko juu kwenye kazi za ulinzi kwa wenzetu ukikuta mtaalamu ujue sio tia maji tia maji kabisa.

Lakini vyombo vya ulinzi havina mandate ya ku set dira ya nchi at their wishes, popote duniani.
 
Nadhani inaitwa ilani ya uchaguzi, hiyo ndio agenda ya serikari yoyote inayochukua madaraka

Vyombo vya ulinzi na usalama havina mandate ya kuendesha nchi kwenye siasa za uchaguzi, serikari iliyochaguliwa ndio yenye jukumu hilo.

Kupitia raisi na baraza la mawaziri wao ndio wanaamua dira ya nchi sio vyombo vya usalama.

Jukumu la vyombo vya ulinzi ni usalama wa nchi, the intelligence part ni kushauri hatua za serikari kuchukua ambazo viongozi wenye mandate wanaweza chakua au kukataa huo ndio utaratibu wa serikari duniani.

Kwenye dunia ya kwanza vyombo vya ulinzi wana mbinu zingine za ku influence serikari kwenda kwa mtindo wao either kupitia ushauri wa kitaalamu wenye ushahidi au pressure tactic za media, pressure groups and swaying public opinion; mara nyingi wanafanikiwa hilo sio zote.

Ndio maana huko juu kwenye kazi za ulinzi kwa wenzetu ukikuta mtaalamu ujue sio tia maji tia maji kabisa.

Lakini vyombo vya ulinzi havina mandate ya ku set dira ya nchi at their wishes.
Huwa kuna mutual relationship kati ya sera na vyombo vya ulinzi hata hapa kwetu kwa nje unaona na sera zinasema wanajeshi hawana vyama lakini ukweli hauko hivo wao kwa nchi hii ni walinzi wa ccm ingawa wanajaribu sana kujificha utwajua siku ccm ikiwa imekabwa kwenye uchaguzi. Hii kitu kilijengwa siku nyingi kwa siri kubwa. Hii ndo inayotutafuna sisi hatuwezi kufanya mabadiliko kwa kuwa hawa wako upande fulani kama wangekuwa hawan upande tungeweza kusonga mbele.
Kwa hiyo kuhusu document ni imani ya nchi ambayo lazima ilindwe kwa nguvu zote mfano ujamaa au ubepari lazima kuna mutual relation ship ndo maana western europe na maerkani walikuwa wanafanya assassination ya viongozi mbalimbali duniani wanaopropagate ujamaaa
 
Kuna mambo katika nchi huwezi kwenda behond that lakini hapa kwetu sio katiba sio nini kwa jinsi tulivyoshuhudia awamu hii tuna katiba mbovu sana ambayo inampa rais anavyotaka na hafungwi kufanya anayowaza ni hatari sana
Najaribu kufikiria mpaka nakunja ndita, nimesoma andiko lako mara mbilimbili lakini sikuelewi kabisa una maana gani!!

Kwa hiyo mkuu Katiba ya nchi na the so called "state document" tofauti yake ni ipi? Na ni document ipi baina ya hizi mbili ambayo itakuwa supreme over the other? Je, una uhakika Katiba ya nchi hii haitamki kuhusu mfumo au imani ya nchi? Hebu nenda kaisome tena Katiba maana inavyoonekana hujui hata maudhui ya Katiba ya nchi hii yakoje.

Toa mfano mmoja tu wa nchi yenye "state document " na utoe maudhui ya "state document" angalau kwa muhtasari labda nitakuelewa.

Je, ni mamlaka ipi hutunga au kutengeneza "state document"?

Wasomi wa kale wameielezea Katiba ya nchi kama sheria mama; hakuna sheria nyingine juu yake, na/au kinzani kwake itasimama salama bila kutenguka Kwa kiwango ilichokinzana na Katiba. Hii ni kwa sababu Katiba hutungwa kwa mujibu wa maoni ya watu (wananchi) wa nchi nzima siyo kwa maoni ya bunge, kamati, au baraza, au hoja ya mtu binafsi etc kama ilivyo kwa sheria zingine ndogo etc.

Je, hiyo document hutungwaje?
 
Huwa kuna mutual relationship kati ya sera na vyombo vya ulinzi hata hapa kwetu kwa nje unaona na sera zinasema wanajeshi hawana vyama lakini ukweli hauko hivo wao kwa nchi hii ni walinzi wa ccm ingawa wanajaribu sana kujificha utwajua siku ccm ikiwa imekabwa kwenye uchaguzi. Hii kitu kilijengwa siku nyingi kwa siri kubwa. Hii ndo inayotutafuna sisi hatuwezi kufanya mabadiliko kwa kuwa hawa wako upande fulani kama wangekuwa hawan upande tungeweza kusonga mbele.
Kwa hiyo kuhusu document ni imani ya nchi ambayo lazima ilindwe kwa nguvu zote mfano ujamaa au ubepari lazima kuna mutual relation ship ndo maana western europe na maerkani walikuwa wanafanya assassination ya viongozi mbalimbali duniani wanaopropagate ujamaaa
Vyombo vya ulinzi vinashauri mambo mbali mbali kama ni maswala ya kufuatwa kwa muda mrefu inabidi itungwe sheria yake na kuwe na policy approach (sera) ya muda mrefu. Hivyo ndio wanaweza hakikisha dira wanayo kusudia inafuatwa na serikari itakayoingia madarakani ata za baadae.

Lakini hawana mandate ya maamuzi ya mwisho, ndio maana anapotokea raisi ambae akubaliani nao watatafuta mbinu za kumwondoa kwa namna za democracy au ikibidi planned assassination.

Na sisi tupo mbali sana nao kwa sababu wengi waobaadhi ya nchi za wenzetu (sio zote) kuna nafasi kadhaa za juu kwenye ulinzi tenure zao zinalindwa kweli kweli na sheria kuwatoa ni vigumu, ndio maana wanakuwa bold pale ambapo wanadhani lazma wachukue action.

But there is also a danger hizo nafasi zikiwa ngumu kuzitengukua utakuta wao wanashinda mara nyingi kwa mbinu zao chafu za kulazimisha serikari ndio mzozo wa siasa za UK, na swali lao kuu who runs the nation? politician or civil services kupitia makatibu wakuu.
 
Ila bwana yule alipopewa tu dola aliichanachana hiyo document tena akatafuta vipande vya paper alivyovichana sasa kwa mukthadha huu hana guidance
 
''state document itakayolindwa na vyombo vya ulinzi na usalama'' ni mdudu gani?

Hii nchi nadhani ujinga unaongezeka lakini kibaya zaidi wajinga hawajijui kama ni wajinga!
Unaweza ukanitajia sera ya taifa iliyo wekwa na inayo tekelezwa tokea taifa lilipoundwa?
 
Maoni yako haya yamedhihirisha nilichokiandika kuwa kuna wajinga lakini hawajui kama ni wajinga!
Ni kweli mkuu hasa viongozi wetu wanaotoa dhahabu na kugawa kwa mabeberu alafu leo wanaanza kujidai wanaijali nchi... Hasa viongozi wetu wanajidai wema kumbe ni wezi wa mali za umma.

Kweli hawa viongozi wa serikali ni wajinga na hawajui kama ni wajinga.
 
Back
Top Bottom